Wakurya Shikamooni

Wakurya Shikamooni

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
12,706
Reaction score
52,355
Hawa jamaa ni majasiri Sana unakumbuka zile kelele za nishati Safi.

Sasa Kuna maliasili na polisi walijichanganya wakaingia anga za wakurya wanaojishughulisha na biashara ya mkaa kwenye ili pori la kuelekea kisarawe pale.

Aisee walichokutana nacho hawatokaa warudi tena kwenye lile pori.

Yaani kelele zote za nishati Safi ziliishia pale!!😀😀😀

Kumbuka ile story ya Zakaria Tena kwenye utawala wa Jiwe

Wakurya nawapa salute Sana tungekuwa wote tupo Kama hawa jamaa sasahivi tungekuwa mbali sana kimaendeleo

Hawataki mchezo ukiingilia maslahi yao eti unazuia mkaa wakati mpaka Ikulu wanautumia!!

Wakurya Shikamooni nyie ni watu na nusu CCM isingekuwa inanyanyasa watu kiasi hiki Kama tungekuwa na ujasiri Kama wa Hawa jamaa!!
 
Kweli huko ukuriani ni habari nyingine.
Sasa kuna jamaa zangu huko ungonini. Niliposoma ushujaa wa wangoni au wanguni (sijui tofauti yake) nilitegemea wangoni ndio watu hapa TZ wangekuwa wakali kutetea maslahi yao hao wakurya wakasome.

Kinyume chake ni mbingu na nchi. Kuna siku nili wauliza wangoni marafiki zangu, inakuwaje mpo hivyo?

Mmoja wao alisema ni madhara ya Mjerumani kunyonga machifu hadharani huku raia wangoni wakishuhudia.

Toka siku hiyo wangoni wakachagua kuwa wapole wapole maisha yasonge mbele.

Kuna faida raia wakiwa wapole wapole, japo walichofanya wajerumani ni jambo baya sana.

Samahani wangoni marafiki zangu kama nimewakwaza.
 
Kuna polisi jamaa watatu mmoja jirani yangu ilikuwa dili lao ni kuwakamata jamaa wa mkaa. Mwezi uliopita mmoja alikatwakatwa mapanga kama mbuzi au kitimoto. Wengine wawili wakakimbia
 
Back
Top Bottom