Wakuu depression inanimaliza

Kwema ndugu zangu,

Niende moja kwa moja kwenye mada, nimekuwa napitia hali ngumu ya maisha Niko stressed sana, jobless mpaka naona mtaani nadhalilika mbele ya ndugu jamaa na marafiki. Najitahidi ku fight back ila sio rahisi. Muwe na mchana mwema.
Pole, ila wewe ndio gate keaper wa aliki yako, hivyo, unaweza kuchagua nini cha kuruhusu/kufikiri nk! Naona umeruhusu mawazo ya kifeli na kujikataa! Skia, wwe sio mwenye elimu pekee ambaye hajaajiriwa! Nilikaa 2 yrs baada ya ajira na nikaanza kujitolea kwenye kampuni mpya ya mikopo kwa malipo ya chakula cha mchana! Baada ya miazi kadhaa nikaanza pewa 50k per month! Nilikaa hapo mpaka nilipofikia malipo ya 300k huku nikiitwa meneja mikopo!

Aidha, nikiwa chuo mwaka wa mwisho nakumbuka nilichagua hadi Kampuni ambayo ningependa kufanya kazi na kujipangia mshahara! Kila jambo lina mwanzo wake, hata mafanikio huanzia chini, hivyo usiandamwe na malengo makubwa na ya haraka uliyojiwekea!

Lengo la elimu ni kukupa maarifa, kukuboreshea ufikiri wako na ufanyaji wa maamuzi na si kuajiriwa! Identify ypir goals na anza taratibu, Mungu anabariki jitihada(kazi za mikono).

Nilishauza chips nikiwa chuo mwaka wa 03! Degree/Diploma nk isikupe upofu wa kuona kwamba, wewe ni wa shughuli fulani ama biashara zenye frem zilizo na AC.
 
Umeona ehh
Sasa dawa zake another side effects ni kutaka kujiua!
Sasa 🥹ni kazi kweli kweli walahi!
Tema mate chini usikumbwe walahi [emoji22]
Naijua depression sana na nilikuwa nawasaidia sana watu wenye msongo wa mawazo
Wengi wanawaza kujiua tu yaani amechoka na maisha
Ila dawa ni kuondoka hiyo sehemu uliyopo na kwenda mahali pengine kabisa hata kwa bibi

Utapona kwani utakuwa umeacha yaliyokuwa yanakusababishia mawazo

Hata kama ni mahusiano ndio sababu basi usiyalazimishe sio unaumia kisa mwenzio kashindwa kubadilika

Mkimbie
 
Daaah...poleni sana Wadau, namwomba Mungu awafanyie wepesi katika mapito yenu.
 
Kwema ndugu zangu,

Niende moja kwa moja kwenye mada, nimekuwa napitia hali ngumu ya maisha Niko stressed sana, jobless mpaka naona mtaani nadhalilika mbele ya ndugu jamaa na marafiki. Najitahidi ku fight back ila sio rahisi. Muwe na mchana mwema.
Pole mkuu, badilisha mazingira nenda usikojulikana ukapambane utakuwa na furaha
 
Unaweza kuvuaa Samaki kwenda mafia kukaa siku kumi baharini??

If yes Dm ukapige kazi
Ukipendwa na jini ushakuwa MO dwji

Ukiwa na damu mbaya tunakutoa kafara
 
Poleni sana rafiki zangu, nimesoma comment ni huzuni sana....!!! Mungu aendelee kuwapambania lakini msikate tamaa wala msifikirie kujizuru..... ni kukomaa sana siku moja mungu atafanya heri
 
Unaweza kuvuaa Samaki kwenda mafia kukaa siku kumi baharini??

If yes Dm ukapige kazi
Ukipendwa na jini ushakuwa MO dwji

Ukiwa na damu mbaya tunakutoa kafara
Hivi hizi ni akili za Mtu mzima kweli au ni bangi nibangue?[emoji16]
 
Mbona unajipinga mwenyewe tena...
 
Kwema ndugu zangu,

Niende moja kwa moja kwenye mada, nimekuwa napitia hali ngumu ya maisha Niko stressed sana, jobless mpaka naona mtaani nadhalilika mbele ya ndugu jamaa na marafiki. Najitahidi ku fight back ila sio rahisi. Muwe na mchana mwema.


Tatizo wengi wetu sio wataalamu lakini kukusaidia inategemea sana na umri wako. Je una umri gani?. Lakini pili kukabiliana na vitu kama hivi ni lazima uwe na kitu ambacho ni kikubwa kuliko ubinadamu wetu ambacho ni imani. Nashauri uende kwa viongozi wako wa imani na kuwaeleza matatizo. Lakini la mwisho ujue matatitizo ni kama mvua yanapita. Lakini kama ni kijana inatakiwa kufikiria mwenendo wako mzima na sio tu kutafuta kazi badala yake fikiria vitu kwa upana wake.
 
Pole lakini hakuna kitu kinachodumu ,Mungu ndio jibu lako sali sanabkwa imani na amini kila kitu kitakua sawa
 

kuna msanii wangu pendwa anaitwa Avicii huyu alijiua kwa depression, yaani mpaka unajiuliza kwani huyu alikuwa na shida gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…