Wakuu haya Madini Yana thamani yoyote hapa Tz?

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
12,463
Reaction score
27,556
Nimeyaona sehemu yapo Kwa wingi. Nahitaji mtu aliye serious na uhakika tutete naye.

Ni hayo mekundu hako kengine kana mng'ao sana zaidi ya shaba na ulanga.

Mimi nimebobea kwenye dhahabu na shaba na hata ulanga ila hii sio ulanga Wala shaba.

Nimejaribu ku search mtandaoni nakutana na Red spinels na Ruby sasa Bado sijajua ni uhakika au ?

Soko lipo uhakika pia?

Ahsante sana
 
Yanayo sema mambwaa wetu madarakani wanayagawa kama nyeti zao kutokana na kukosa akili na ubunifu. Kwa ujumla, Afrika si maskini bali ina umaskini wa watu wanaojitambua. Hatuna tofauti na wanyama porini tunapochimba madini wakati wao daima ni maskini.
 
Sijakuelewa kabisa hata kidogo mkuu.
 
Mkuu ni ngumu kuyaelewa kutokana na picha yenyewe labda ungetolea maelezo ya mahali/namna umeyapata labda ni kutoka kwenye mwamba au umeokota mtoni.

Nafikiri madini yanatofautiana sana namna ya kuyapata, Sasa unaweza kutumia njia hiyo kujua aina ya madini.
 
Mbona yana sukari sukari hayo ? Kwa kifupi kama yapo hivyo hayana dili hayo inatakiwa yawe clear kabisa yasiwe na sukari sukari


Yawe clear kama haya ☝
 
Labda ukichimba Kwa chini ndo yapo clear lakini hapa ni juu juu tu ya mwamba
Yeah ukichimba chini ndio yapo clear, halafu sio kwamba yana thamani sana lakini yakiwa clear unapata hela yakianzia kilo moja . Huwa yanatumika kutengenezea taa za magari, pikipipiki nk ni dili nzuri yanapatikana wapi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…