Wakuu hii imekaaje darasa la kwanza masomo nane?

Wakuu hii imekaaje darasa la kwanza masomo nane?

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
2,971
Reaction score
9,437
Wakuu hawa watoto wetu si watavunjwa mabega dogo ameanza shule leo darasa la kwanza masomo nane.

Yaani madafutari 8+ vitabu 8 jumla kumi na sita vyote anatakiwa avibebe kwenye bag, dogo ana miaka mitano tu aiseeh atameza haya masomo yote.

Math
English
Kiswahili
Drawing
Reading
Sport &art
Heath care
Writing
 
Miaka miatano umamuandikisha mwanao darasa la kwanza ili iweje? Mtoto afikishe miaka saba ndipo umwandikishe darasa la kwanza. Chini ya hapo awe anaenda darasa la awali
 
Zama zimebadilika
Brother amini nakwambia kumuanzisha mwanao darasa la kwanza akiwa na miaka mitano humtendei haki na humjengi katika muktadha wa yeye kuja kumudu kuyakabili maisha ipasavyo.

Kujaza masomo yote hayo katika ubongo wa mtoto wa miaka mitano ni sawa na kupakia mzigo wa kubebwa na fuso kwenue kirikuu. Kwanza unamlazimisha aamke mapema mno ili awahi shule, unambebesha begi ziiito limejaa madaftari na vitabu ~ unamuumiza mtoto.

Halafu wanachelewa kurudi nyumbani wamechoka hoi, afanye homework, anasinzia sinzia ovyo.

Watoto wangu wote niliwaanzisha darasa la kwanza wakiwa na miaka saba na baadhi yao miaka nane, sikuwahi kujutia na namshukuru Mungu walifanya vizuri kwenye masomo yao.

Sifuati mkumbo mimi.

B.T.W ni chaguo lako mzazi
 
Back
Top Bottom