Wakuu hivi kuvuta umeme nguzo Moja Bei gani

Nenda tanesco watatuma watu wao Kuja kusavei na kuchora ramani yao na makadilio ya gharama, Mimi mwaka 2021 zilihitajika nguzo mbili mpaka umeme kunifikia, nilipewa control number nikachajiwa 670k. Nadhani ww kwa nguzo Moja pesa ni chini ya hapo
 
Nenda tanesco watatuma watu wao Kuja kusavei na kuchora ramani yao na makadilio ya gharama, Mimi mwaka 2021 zilihitajika nguzo mbili mpaka umeme kunifikia, nilipewa control number nikachajiwa 670k. Nadhani ww kwa nguzo Moja pesa ni chini ya hapo
Sawa mkuu
 
Najiuliza hapa Bei ya kuvuta umeme nguzo Moja ni Bei Gani Kuna jamaa wameniambia 1m hivi ni kweli wakuu au wanataka kunipiga maana sielewi taratibu mnaojua mnijuze wakuu@Tanesco
Fuata hatua za nikonekti. Ukipita za mkato utaumia.

Nguzo 3 nililipa 600,000
 
Mkuu nitakujibu kulingana na uzoefu wangu kwani nimetoka kuweka umeme kwenye nyumba yangu nyingine hapa dar gharama zilikuwa ni tz shilingi 520,000 pamoja na service line kama ni mkoani sijui coz naskia kuna baadhi bado wapo kwenye mpango wa rea🙏
 
Ilikua nguzo ngapi mkuu
 
Nimelipia hivi karibuni na wamekuja kuunganisha ,nimetoa laki tatu ila ni karibu bila ga nguzo ...Sijajua kama nguzo wanahesabu kwa sababu walikuja kufanya tathmini na kuangalia aina ya wiring iliyowekwa kwanza.
Kama ni mjini, na ni nguzo moja TANESCO wanakula 300,000 (Control number,)

Hapo Wiring ni juu yako. Na kama utawatoa TIP waharakishe kazi ni wewe.

Kwa kijijini, Nguzo moja bei ni hiyo hiyo. Ila kama ukibahatika nyumba yako ikawa eneo ambalo kuna mradi, utapewa kwa 27,000.

Mradi maana yake huwa kunakuwa na nguzo kadhaa zinaletwa ili kuwapa watu wa mtaa mzima umeme. Ila unatakiwa kufanya mchongo na watu wa nguzo wakuwekee nguzo karibu.
 
Sawa mkuu
 
Nikonekti ni ufisadi mtupu, haifanyi kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…