Nimesoma comments zote sijaona mchambuzi aliyesifiwa hata mmoja.
Nikanote kitu kuwa watanzania wengi bado tumegubikwa na vitu hivi
1.Chuki ,
Comments zimejieleza sana namna vijana hawa wanaojitafutia riziki halali wanavyoandamwa.
2.Wivu ,
Kutokana na nchi yangu ilivyojaa wajuaji wengi kila mmoja anatamani angekuwa ni yeye ama ndugu zake.
Mimi wachambuzi wangu ni hawa
a)Eddo kumwembe
ni mmoja ya watu ambao wamesafiri na kwenda nchi nyingi na kujionea mechi kubwa kubwa live, huku akiwa ni bonge moja la mwandishi wa makala za kimichezo na hata kuchambua bado yupo vizuri.
b)Ramadhan Mbwaduke
Huyu anajua sana binafsi namuelewa mno tuacheni chuki.tena huwa anajitahidi kutoegama upande wowote.
c)Amri kiemba
Ni mmoja wa wachambuzi tegemeo kwangu kiasi kwamba wakati mwingine asipokuwepo huwa naona waliobaki siwaelewi
d) George Ambangile
Huyu yeye anapenda kuchambua sana mechi za ulaya, na kiukweli kwangu yupo vizuri na anaijua kazi yake
e)Oscar Oscar
Unaweza kushangaa, lakini ukweli ukiacha masihara yake na posts zake huko X jamaa linajua sana tu tena huyu huwa ni mkweli mara nyingi wachambuzi wengi huziogopa klabu kwa kile kinachoonekana ni fitina lakini huyu he is the best
f) Ally Mayay
Unamuacha wapi huyu jamaa na kudai hajui kuchambua vizuri?
Je, wachambuzi wa Taifa la Denmark, Norway, Turkey,Trinidad and Tobago unawajua?
Au ukizijua ligi kubwa tano maarufu na hao akina Michael Owen na Gary Neville basi umemaliza kazi? acheni mambo zenu.
g)Ally Kamwe,
Dogo kipindi hajapewa shavu na Yanga na kubadili majukumu ni moja ya watu nawakubali mno kwenye kuanalyse , tena ni mtulivu mno anachambua na kueleweka.
Wapo wengi sana wanaojua ila Kuna muda ukisema ukweli basi unaweza jenga chuki na maboss wa vilabu kwani utaonekana snitch hivyo na baadhi ya wachambuzi wanatembea na upeo huohuo this is Tanzania.
h) Alex Kashasha (RIP)
Kwahiyo huyu naye mmemdumb? kweli watu mna chuki, huyu akiwa TBC, yeye na Enock Bwigane, unakuwa kwenye darasa la mpira.
Sema waTZ wengi wanadai hawaangaliagi au kusikiliza TBC ngoja ninyamaze.
My take:
Uchambuzi siyo utabiri hasa kwenye mechi ambayo haijachezwa, kumbuka mchezaji mmoja anaweza kubadili mechi nzima na uchambuzi wako ukaonekana haufai.