Wakuu hivi uchambuzi wa mpira unasomewa?

Wakuu hivi uchambuzi wa mpira unasomewa?

Nimesoma comments zote sijaona mchambuzi aliyesifiwa hata mmoja.

Nikanote kitu kuwa watanzania wengi bado tumegubikwa na vitu hivi

1.Chuki ,
Comments zimejieleza sana namna vijana hawa wanaojitafutia riziki halali wanavyoandamwa.

2.Wivu ,
Kutokana na nchi yangu ilivyojaa wajuaji wengi kila mmoja anatamani angekuwa ni yeye ama ndugu zake.

Mimi wachambuzi wangu ni hawa

a)Eddo kumwembe

ni mmoja ya watu ambao wamesafiri na kwenda nchi nyingi na kujionea mechi kubwa kubwa live, huku akiwa ni bonge moja la mwandishi wa makala za kimichezo na hata kuchambua bado yupo vizuri.

b)Ramadhan Mbwaduke

Huyu anajua sana binafsi namuelewa mno tuacheni chuki.tena huwa anajitahidi kutoegama upande wowote.

c)Amri kiemba

Ni mmoja wa wachambuzi tegemeo kwangu kiasi kwamba wakati mwingine asipokuwepo huwa naona waliobaki siwaelewi

d) George Ambangile

Huyu yeye anapenda kuchambua sana mechi za ulaya, na kiukweli kwangu yupo vizuri na anaijua kazi yake

e)Oscar Oscar

Unaweza kushangaa, lakini ukweli ukiacha masihara yake na posts zake huko X jamaa linajua sana tu tena huyu huwa ni mkweli mara nyingi wachambuzi wengi huziogopa klabu kwa kile kinachoonekana ni fitina lakini huyu he is the best

f) Ally Mayay

Unamuacha wapi huyu jamaa na kudai hajui kuchambua vizuri?
Je, wachambuzi wa Taifa la Denmark, Norway, Turkey,Trinidad and Tobago unawajua?

Au ukizijua ligi kubwa tano maarufu na hao akina Michael Owen na Gary Neville basi umemaliza kazi? acheni mambo zenu.

g)Ally Kamwe,

Dogo kipindi hajapewa shavu na Yanga na kubadili majukumu ni moja ya watu nawakubali mno kwenye kuanalyse , tena ni mtulivu mno anachambua na kueleweka.

Wapo wengi sana wanaojua ila Kuna muda ukisema ukweli basi unaweza jenga chuki na maboss wa vilabu kwani utaonekana snitch hivyo na baadhi ya wachambuzi wanatembea na upeo huohuo this is Tanzania.

h) Alex Kashasha (RIP)

Kwahiyo huyu naye mmemdumb? kweli watu mna chuki, huyu akiwa TBC, yeye na Enock Bwigane, unakuwa kwenye darasa la mpira.
Sema waTZ wengi wanadai hawaangaliagi au kusikiliza TBC ngoja ninyamaze.

My take:

Uchambuzi siyo utabiri hasa kwenye mechi ambayo haijachezwa, kumbuka mchezaji mmoja anaweza kubadili mechi nzima na uchambuzi wako ukaonekana haufai.
 
Mimi nadhani hizi ni course za COACHING kwa ajili ya MAKOCHA wa mpira na si kwa ajili ya wachambuzi wa maswala ya mpira
Hapana sio coaching

Hujaona Football analysis hapo kwenye hizo course?

Tangu lini makocha wakasomea course za analysis (uchambuzi)
 
Nilipomsikia Amri Kiemba kama mchambuzi siku ya tarehe 5 November aliposema tu kwa hali ya mvua Simba wana nafasi ya kupata matokeo na matokeo yake Simba wakapigwa bao 5 basi itoshe tu kusema Tanzania mchambuzi ni mmoja tu Dr Rick Abdullah na ndio maana hachambui hizi mechi za kipuuzi za kina Karia.
Hahahahaahh
 
Nimeacha kuwasikiliza wachambuzi tokea mwaka Jana walivyo idisi yanga kutofika mbali na ajabu tukaenda Tunisia tukawafunga club Africaine na Kisha kunzia hapo tukaanza kuwapiga kila mmoja

Mm nimewacha kbsaa sitaki kiwasikia
 
Unatakiwa ujue misemo Tu..
Double pivot..
Mfumo..
Counter..
Pressing..
Overload / underload
Overlapping / underlapping runs
Low block
Transition
Rest defence
Pressing trap
Offside trap
Occupying
Inverted full-back
Counter pressing
Breaking lines
Bounce pass
Between the lines
Ball orientation

Ukiwa unaongea halafu unatupia hivyo vimaneno kila baada ya sentensi, unaweza hata kupewa usemaji wa timu.
 
Kusoma ni jambo pana, si lazima uingie darasani moja kwa moja.
Mfano mchezaji mstaafu anapata elimu kwa kufundishwa na makocha, experience yake uwanjani, etc.

Dr. Leakey anajua vingi vya soka lakini vingi zaidi vinavyohusiana na soka.
 
Overload / underload
Overlapping / underlapping runs
Low block
Transition
Rest defence
Pressing trap
Offside trap
Occupying
Inverted full-back
Counter pressing
Breaking lines
Bounce pass
Between the lines
Ball orientation

Ukiwa unaongea halafu unatupia hivyo vimaneno kila baada ya sentensi, unaweza hata kupewa usemaji wa timu.
Kuna moja wachambuzi kila siku wanatuoiga changa wanaida "inside 10" sasa unajiuliza kuna outside 10!?? 😂🤣
 
Uchambuzi wa mpira ni kama tu uchambuzi mwingine kama uchambuzi wa mchicha au Michele uwe na jicho la kupambanua kajiwe na mchele
 
Back
Top Bottom