Wakuu huu mwaka 2025 unapoenda sehemu iwe barber shop, restaurant etc, kabla yakupata huduma ni bora ukauliza kwanza bei yalinikuta

Wakuu huu mwaka 2025 unapoenda sehemu iwe barber shop, restaurant etc, kabla yakupata huduma ni bora ukauliza kwanza bei yalinikuta

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
2,971
Reaction score
9,437
Niliwahi kuingia barbershop moja humu ndani kuna full kiyoyozi huduma si mchezo masaa mawili kinyozi anakunyoa hana haraka.

Nikanyoa si unajua tena wadada wa barber shop kaka uso wako una mafuta sana ngoja tukusafishe uso, nikatoka nimeg’aa ile mbaya, ikaja bill macho yalinitoka 45000.

Uzuri nilikuwa na pesa mfukoni, sikubishana kwa kuwa sikuuliza hapo awali. Kuanzia siku hiyo nikawa na adabu.
 
Pole sana mkuu.
Naamini vinyozi na madada wa saluni watakusikia, ila kama wanaona umewakosea na wanafikiria kukuteka nayo sawa tu.
 
Back
Top Bottom