Wakuu huyu 'Mama Ntilie' anapataje faida? Naona kama nimefaidi zaidi Ugali mboga 7

daa
 
Vyakula vya mama ntilie sio vya kuzoea sio vyakula salama kabisa, ukiachilia mbali uchafu na uchakachuaji unaofanyika mf utumiaji wa amila, kuoshea maji ya mtaloni kuna mambo ya ushirikina sana, wemgine hutemea mpak makohozi kwenye chakula ili mambo yaende sawa.....kuna mambo ya ajabu sana kwa mama ntilie
 
Nimelipa 1500

Nimekula

Ugali
Dagaa wa mwanza
Samaki Kibua
Mlenda
Bamia
Maharage
Matembere
Kila kimoja kinajitegemea havijachanganywa.
Nafikiri ungemuuliza yeye,afu 1500kama kubwa vile,huku kwetu ni buku tu wali nyama,maharage na vegetable vivyo hivyo ugali nyama,dagaa,vegetable n.k
Huyo anaetoza 1500 anapata super profit
 
Nafikiri ungemuuliza yeye,afu 1500kama kubwa vile,huku kwetu ni buku tu wali nyama,maharage na vegetable vivyo hivyo ugali nyama,dagaa,vegetable n.k
Huyo anaetoza 1500 anapata super profit
ushirombo mchele si analima mwenyewe. nyama mbuzi zake anachinja mkuu
 
mamaaa, makohozi tena?
 
Nimelipa 1500

Nimekula

Ugali
Dagaa wa mwanza
Samaki Kibua
Mlenda
Bamia
Maharage
Matembere
Kila kimoja kinajitegemea havijachanganywa.
Anakupenda huyo bila shaka anataka uwe mwandani wake subili muda si mrefu, mwenzio katerekeza familia sababu ya supu
 
Mshana Jr

jamaa ananitisha huko juu. hebu dondosha hekima zako hapa. Ulozi upo hadi kwenye mambo nyeti kama misosi mkuu.
Mwache mdogo wangu kalala kwenye lindo. Ni hivi unapewa bamia moja, mchicha kidogo, samaki kibua wanatoa feri wanajua jinsi wanavyo bargain, ugali wanakupa umeshapigiwa mahesabu. Mimi nina mama ntilie pale kwangu. Nyama minofu miwili, mchicha au mboga yoyote kidogo, maharagwe na mchuzi kidogo. At the end of the day kama wateja wamekuja anapata faida elfu 3 tu baada ya kunilipa mimi za pango na kulipa alipokopa kuanza biashara asubuhi. Upo. Akirudi nyumbani mme kanuna wakati yeye kabeba mandoo na mtoto mgongoni. Kesho yale yale halafu mnakuja humu mnatunanga wanawake hamjui maisha tunayoishi. Mnawaangalia hao mabishoo lakini mnasahau mama na dada zenu wanaoteseka kusomesha wadogo zenu bila msaada wa waume zao wanaolewa na kujidundika madawa.
 
maneno yamechanganyikana na machozi.
nimeelewa mama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…