Mwache mdogo wangu kalala kwenye lindo. Ni hivi unapewa bamia moja, mchicha kidogo, samaki kibua wanatoa feri wanajua jinsi wanavyo bargain, ugali wanakupa umeshapigiwa mahesabu. Mimi nina mama ntilie pale kwangu. Nyama minofu miwili, mchicha au mboga yoyote kidogo, maharagwe na mchuzi kidogo. At the end of the day kama wateja wamekuja anapata faida elfu 3 tu baada ya kunilipa mimi za pango na kulipa alipokopa kuanza biashara asubuhi. Upo. Akirudi nyumbani mme kanuna wakati yeye kabeba mandoo na mtoto mgongoni. Kesho yale yale halafu mnakuja humu mnatunanga wanawake hamjui maisha tunayoishi. Mnawaangalia hao mabishoo lakini mnasahau mama na dada zenu wanaoteseka kusomesha wadogo zenu bila msaada wa waume zao wanaolewa na kujidundika madawa.