Habari wakuu?
Ndugu zangu mimi naishi Misugusugu Kibaha, hivi karibuni nimeanza kuona dalili za ukame kwenye kampuni ninayofanya kazi, jana nikaona niombe ruhusa kazini ili niingie zangu mtaani kucheki mazingira.
Nyumba ninayoishi kuna vijana wanafanya mishe za ujenzi viwandani, kwenye stori zetu za kila siku hawa vijana walishawahi kunidokezea kuhusu uwepo wa viwanda vingi eneo la Zegereni Kibaha. Sasa siku ya jana nikaamua kuingia maeneo ya Zegereni-Kibaha, eeeh bwana eeeh huku kuna viwanda vingi sana na wenyeji wa haya maeneo wanakuambia viwanda vinajengwa kila kukicha.
Ndugu zangu habari za kutafuta kazi uzisikie tu kwa wenzio, hii kitu sio poa kabisa, jana nimetembea mpaka nikajionea huruma, nimegonga sana mageti ya viwanda, oyaaah Mungu awatie nguvu vijana wanaotafuta ajira kwa mtindo wa kuzunguka viwandani na maofini.
Tufupishe stori, katika kutembea kwangu nikafanikiwa kufika kwenye kiwanda kimoja kikubwa sana, ni kiwanda ambacho kipo kwenye hatua za mwisho za ujenzi lakini kimeshaanza uzalishaji. Askari niliyemkuta getini aliniambia kile kiwanda wanatengeneza mabati na pikipiki, nilizunguka viwanda vingi lakini hiki ndio kiwanda pekee ambacho askari wake aliniruhusu kuingia hadi ndani.
Nilimuuliza kuhusu utaratibu wa kuomba ajira pale kiwandani, alinijibu kuwa kwasasa kazi zinazopatikana pale ni kazi za ujenzi tu, ila kuna taarifa kuwa mwezi wa kwanza au mwezi wa pili mwakani kiwanda kitaajiri watu, baada ya stori za hapa na pale na yule askari nilichukua namba zake za simu nikatembea zangu. Yule askari aliniambia kiwanda kinaitwa KINGLION.
Sasa tuje kwenye lengo la uzi, jamii forums ina wanachama wengi sana, kama kuna mwanachama wa JF una mamlaka au connection KINGLION ZEGERENI - KIBAHA, fanya maarifa unishike mkono nije nikae pale maisha yaende, kiwanda bado kipya kabisa.