Kwanza, uhakika upi ulionao kwamba hana? Mmepima wote na kujihakikishia kuwa kweli hana? Kama ndiyo, basi unaweza kuacha tu bila changamoto.
Lakini kama ni yeye kakuambia tu, basi fikeni wote kwenye kituo vha afya kwa uchunguzi na uhakika zaidi.
Unaweza kuacha kuitumia baada ya kujiridhisha.
Kuhusu madhara, PEP haina madhara yeyote serious. Kichefuchefu, kuumwa kichwa, nk.
Cha kufahamu ni kuwa PEP ni matumizi ya dawa ya kufubaza virusi kwa muda mfupi (mathalani mwezi mmoja). Dawa za ARV hazina madhara makubwa zikitumika kiusahihi, vinginevyo zingeshazuiwa. Wapo watu wanaopata athari, lakini ni kwa kiwango kidogo sana.