Wakuu nasikia G Malissa katekwa heti,si alikuwa nje ya Nchi,imekuaje Tena?

Wakuu nasikia G Malissa katekwa heti,si alikuwa nje ya Nchi,imekuaje Tena?

Malisa GJ Leo alikuwa safarini kutoka Marekani ambapo amekuwa kwa zaidi ya miezi tisa (9), tangu alipoenda kuiwakilisha nchi yetu kama mtanzania pekee aliyechaguliwa na Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani kwenda kupata mafunzo ya uongozi. Fursa ambayo hujitokeza kwa watanzania wachache sana kama ilivyowahi kutokea kwa aliyekuwa Rais wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Alipofika Nairobi- Kenya asubuhi ya leo, alishindwa kuendelea na safari kutokana na kuwepo kwa mgomo wa wafanyakazi unaondelea katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta. Hivyo aliamua kusafiri kwa usafiri binafsi mpaka Namanga ambao ni mpaka kati ya nchi yetu na Kenya ili kuingia nchini kupitia Arusha.

Aliwasili Namanga majira ya saa tisa(9) mchana na kwenda kwa maafisa uhamiaji ili kugongewa hati ya kusafiria (Passport) na hatimaye kuingia nchini kama utaratibu unavyotaka.

Baada ya kufika kwa maafisa uhamiaji hao, walichukua hati yake ya kusafiria na kumwambia kuwa haisomeki kwenye mfumo (system) hivyo wao hawana namna ya kufanya mpaka mkuu wao (in- charge) aje ndio anaweza kuona kwenye mfumo.

Kutokana na kadhia hiyo, na kwa kuwa aliambiwa Mkuu huyo hayupo kwa muda Malisa GJ aliendelea kukaa katika ofisi hizo za uhamiaji akisubiri Mkuu huyo kuja na kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi.

Cha kushangaza ilipofika saa moja jioni, alichukuliwa na gari ambalo si la Polisi jeupe Double Cabin na kupelekwa kituo cha Polisi Longido. Hata hivyo gari hilo halikukaa sana likaondoka kuelekea uelekeo wa Arusha.

Mpaka natoa taarifa hii hakuna taarifa kamili za aliko Malisa GJ na nini ni sababu ya kukamatwa kwake. Aidha simu zake zote zimezimwa tangu alipokuwa anatolewa Namanga.

Nitoe rai kwa Polisi na Uhamiaji kumwachia huru mara moja au kuhakikisha wanatoa taarifa kwa umma za aliko Malisa GJ na sababu ya kukamatwa kwake. Kama haitoshi kuhakikisha anapewa haki zake za kisheria ikiwemo kuonana na mawakili wake na haki ya Mawasiliano.

Dickson Matata (Wakili)
31/8/2026
Arusha-Tanzania.
 
Yani hali ilivyo saivi ni kheri utembee na kimguu cha kuku… watakukamata ila angalau utakuwa umeondoka na wawili watatu sio mbaya…
Red flag ya kwanza alipofika hapo uhamiaji ni kuambiwa hati yake haisomi kwenye system..

Huyu kijana ameniuma basi tu sina la kufanya
 
  • Thanks
Reactions: ---
Una Roho kama watekaji,
Hivi Elnino si inakuja, kwa nn isiwasombe nyie wote shubaramit!
kama nyinyi ndio mlishauri arudi maana unaonekana uko karibu zaidi, basi ni wapuuzi nyinyi
huyo fala kulopolopo kwake ilikuwa tiketi ya kuishi huko halafu kawasikiliza nyinyi vilaza
 
Kwahiyo unataka kusemaje? Hivi ni kilopo lopo yu alikua anatetea haki za raia?
Acheni kujifanya miungu watu, imo nanyi siku yenu, yaja.
Hio nchi wala hata siishi nilishaikana wala usihofu
lakini kwenye siasa za bongo nina ufahamu kuona huyu ni mjinga na yule yuko sawa
Yaani utoke hapa uende nje ya nchi kufanya kampeni dhidi ya serikali bila kuwa na plan B , huu ni uzwazwa, tukisema ujinga wake tunaonekana tuna roho mbaya
 
yaan USA ilimchagua kumpiga kitabu wanajua lzma kinachoendelea tz wakamuacha arudi tena kwa kulazimisha alf na police hawaoni huo ni mtego wanaruka nae, naona mwisho tafadhali iwe tu asee
 
yaan USA ilimchagua kumpiga kitabu wanajua lzma kinachoendelea tz wakamuacha arudi tena kwa kulazimisha alf na police hawaoni huo ni mtego wanaruka nae, naona mwisho tafadhali iwe tu asee
hakuna mtego hapo, kwa kuwa bado ni raia tanzania, hana ujanja na US hawana muda kutetea watu weusi wa africa
Ni kama recho dangwa anaishi kwa vibali halafu analopolopo, sijui leo yuko wapi masikini
 
Hio nchi wala hata siishi nilishaikana wala usihofu
lakini kwenye siasa za bongo nina ufahamu kuona huyu ni mjinga na yule yuko sawa
Yaani utoke hapa uende nje ya nchi kufanya kampeni dhidi ya serikali bila kuwa na plan B , huu ni uzwazwa, tukisema ujinga wake tunaonekana tuna roho mbaya
You are making some sense.
 
yaan USA ilimchagua kumpiga kitabu wanajua lzma kinachoendelea tz wakamuacha arudi tena kwa kulazimisha alf na police hawaoni huo ni mtego wanaruka nae, naona mwisho tafadhali iwe tu asee
Polisi lazima Wateme BUNGO ,wameingia CHA KIKE.
 
Sasa huyu naye anarudi Bongo usawa huu wakati anaona kinachoendelea kwani alisahau nini?

Kashindwa kuongea na connections zake za State Department kuchukua ukimbizi aangalie upepo kwanza?

Au ndiyo anataka kupambana kutoka ground?
Kwa nchi ilipo fikia ni vyema kabla ya kupanua mdomo wako ujihakikishie kuwa uko salama kiasi gani kwanza.
Sasa hivi huyu mama Hana tofauti na kagame.
Kwanza hao Wana harakati walio jazana hapo Kenya hawapo salama hata kidogo.
 
Back
Top Bottom