Wakuu nataka kununua gari kwa Mara ya kwanza na ninaishi mazingira ambayo ni rough kiasi. Naomba kujua ni gari gani dogo linaweza kuvumilia

Hii Toyota Cami ukiipeleka Nyasa jiandae kuhudhuria gereji mara kwa mara.
Mkuu Kutoka Nyasa kwenda Mbinga kuna milima mikali sana na njia za kwenda Mpapa,Matili, Dar Porini mvua ikinyesha hiyo Cami na 4wd yake itakaa.
Barabara ni lami au vumbi?
 
Namshauri anunue RAV 4 OLD MODEL ya mwaka 1997 au 1998/1999!

Iwe ni full time four wheel. Akipata ya Manual nzuri zaidi. Gari inavumilia sana, ila ina urafiki na maji ya uarabuni.
Ninayo moja hapa, kama muanzisha uzi yupo interested, nione through PM
 
Mzee kama kuna gari ya kijinga kwenye utelezi ni gx 100,hio aachane nayo kabisa kwa ushauri wangu.

Naona Escudo massawe/old model itamfaa sana,ina 4wd kali sana ile gari,kuna sehemu hua inapita hata Hizi Suv with Full time 4wd hazisogezi pua yake.
Escudo ni gari hasa. Hakichagui barabara + kina shock up nzuri sana very comfortable
 
Namshauri achukue toyota cami/ terios kid itamfaa kwa sabab
1. Lipo juu
2. Lina 4wd
3. Bei yake sio kubwa( around 9million unapata used from japan)
4. Linatumia mafuta vizuri
5. Lina seat za kukaa watu 4

Habari kaka. Wewe ni dalali/unauza magari?
Natafuta Honda Fit/Vitz nzuri bajeti yangu 4m mpaka 5m.
 
Msaada jamani, hii Toyota cami Beforward na website nyingine za kuuza magari huandika kuwa ina siti 5. Lakini mie nikiingalia naona nne tu. Sasa mliomiliki gari hii, hivi siti zake ni 5 au 4? Hiyo ya 5 inapatikana vipi?
 
Bei za hizo gari zimesimamia ukucha mkuu $4000 -8000
 
Bei za hizo gari zimesimamia ukucha mkuu $4000 -8000
Mkuu nazungumzia used za hapa Bongo maana siku hizi Mark/Cresta/Chaser zile GR90, balloon GR100 na GX100 bei zipo chini akiwa na kuanzia million 4 anapata nzuri.
 
Habari kaka. Wewe ni dalali/unauza magari?
Natafuta Honda Fit/Vitz nzuri bajeti yangu 4m mpaka 5m.
vitz ya 4m -5 ni mamba C

zinapatikana za kutosha

tatizo La wateja wa Jf unahangaika kumtafutia gari ukimtumia anapotea hewani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…