Wakuu naumia sana, naombeni msaada wa ushauri

scot mcomic

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2021
Posts
234
Reaction score
383
Habari za sikukuu ya pasaka natumai wote ni wazima waungwana, niende Moja Kwa moja kwenye mada ni kwamba hapa kazini Kuna dada mmoja tulitokea kupendana sana Sasa juzi tukapishana kauli nikatikisa kiberiti mwenzangu kamwaga njiti kabisa.

Nilikuwa nampima tu kwamba tuachane akakubali Sasa nimeweka ngumu lakini naona kabisa nashindwa kibaya Kila saa namuona anavyo chat na majamaa wengine Wanacheka nini.

Kwakweli nje navumilia lakini nachomeka mwenye mbinu yeyote anipe jamani ya kumpotezea unaye mpenda halafu mpo karibu, ushauri pia kukosolewa naruhusu karibuni sana.

 
We nae pasaka yoteee hii badala ufurahii unajipa matress tu..!

Kula nyamaa kula bia maisha ni haya hayaa!
 
Unakuaje na mchuchu kazini? Achana na hizo habari, ni ujinga na unajiweka kwenye risk kubwa sana kuwa na Mpenzi ofisi moja au eneo moja la KAZI
 
Mm mchepuko wangu nilidesh kutoutafuta nawenyewe ukaacha saivi ni mwezi na ninajiona fresh, haunitafuti siutafuti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…