Wakuu nawezaje kupata kazi ya CASINO hapa Dar

Planeti

Member
Joined
Jun 4, 2020
Posts
86
Reaction score
93
Ndugu zangu maisha kwa kijana mimi yamekuwa changamoto. Natamani nirudishe mpira kwa kipa lakini imani inanijia kesho ni bora kuliko leo. Nisikate tamaa.

Najua ni wengi tunapita katika kipindi kigumu, tupige moyo konde tusije jiingiza kwenye dili haramu tukajikuta kwny mikono salama..

Nimekaa nikawaza, nikajaribu kutafuta kazi za casino, lakini sina pa kuanzia. Narudi kwenu ndugu jamaa na marafiki..

Kwa yeyote mwenye A B C za kazi za casino asisite kunishirikisha ..

Asanteni
 
Cassino kuna kazi halali za hapa duniani,ila mbinguni utapasikia tu(sina hakika lkn)
 
Wewe ni jinsia gani??tuanzie hapo kwanza.
 
Bro its better uanze kuuza kagaranga huko kasino utaishia kua chawa tu.
 
Nenda pale Princess Cassino, au Rigrend Cassino watakupa utaratibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…