Wakuu nifanyeje nilijue draft?

Wakuu nifanyeje nilijue draft?

February Makamba

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2020
Posts
2,151
Reaction score
2,983
Wasalaam wakuu.

Nimejaribu njia nyingi, kuangalia tutorials,Kucheza online, kudownload checkers, kucheza na watu lakini mara nyingi naishia kula za uso tu.

Hivi hakuna app ya kunifunza strategies step by step?

Kila siku nachekwa kijiweni hadi naona aibu kuomba mechi.
 
Anzia chini,

Kisha njoo na watu wa level yako,

Kisha panda waliokuzidi kidogo halafu tafuta mabingwa.

Kanuni kubwa ni kucheza kete za mwenzako.
Kucheza na Akili yake.

Fikiria Kuwa yeye akicheza Ile Mimi nitacheza hii.

Fikiria hata michezo minne mbele
 
Umeona?mpaka sometimes huwa nahisi draft ni kama kujua lugha au kuendesha baiskeli usipolijua utotoni inakuwa ngumu sana kulimasta ukubwani...ila ukishalijua hata usipocheza miaka 10 ukirudi inakuwa kama unakumbushia tu

Draft ukubwani utaishia kujua level za chini, hasa ukishakuwa na majukumu.

Kama uko vizuri unaweza ukafika moderate level, lakini ni kazi sana.
 
Wasalaam wakuu.
Nimejaribu njia nyingi,kuangalia tutorials,Kucheza online,kudownload checkers,kucheza na watu lakini mara nyingi naishia kula za uso tu...​
Daah upo Kama Mimi pamoja na kufaulu hesabu za shule kutoka msingi mpaka kuja kuwa Mhandisi eti hesabu za draft zimenipiga chenga.

Nimejaribu kufuatilia kwa kuangalia wataalamu wanavyocheza bado naona maruweruwe tu. Nimebaki kuwa mtazamaji tu na kusikiliza maneno ya kwenye draft ndiyo starehe yangu iliyobaki.

Sijui nianzie wapi ili niweze kumaster huu mchezo.
 
tafuta kuku mweusi nakuja popote ulipo

draft la vijiweni lazima pia uwe mbabe wa maneno, maneno mengi yanamtoa mpinzani kimchezo, pia yanakupa ujasiri
 
Wasalaam wakuu.
Nimejaribu njia nyingi,kuangalia tutorials,Kucheza online,kudownload checkers,kucheza na watu lakini mara nyingi naishia kula za uso tu..
Hivi hakuna app ya kunifunza strategies step by step?
Kila siku nachekwa kijiweni hadi naona aibu kuomba mechi.
Tafuta pesa aisee, draft linakusaidia nini?
 
Kuna vitu vingine unaweza kuhisi hujaelewa kinachoulizwa hasa ni nini! Ina maana draft hili hili la kupanga visoda/vizibo vya chupa za maji au kuna draft lingine?
 
Back
Top Bottom