Wakuu, ninahitaji msaada wa kitabibu hasa daktari wa watoto

Wakuu, ninahitaji msaada wa kitabibu hasa daktari wa watoto

Albizo

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
284
Reaction score
208
Habari za asubuhi wadau wa Afya, natumaini mko salama.
Niende straight kwenye mada.

Mwanangu wa kike anaumri wa miezi mi4, sasa takribani mwezi na wiki2 zilizopita alitokewa na vipele kama vi4 chini ya kwapa kuelekea mgongoni.

Vipele hivyo ni kama vimevujia damu na chaajabu havimuumi ila kama vinaongezeka. Kuna mdau nilimuuliza akaniambia huenda ni Hemangioma sijui. Sasa Nilivyogoogle nimeona picha za ajabu na nimepaniki sana. Awali tulikua tunajua vitaisha vyenyewe.

Naomba ushauri kwa maspecialist wa watoto na kama kuna tiba au namna yoyote ya kurudisha hali ya zamani.

Natanguliza shukran zangu za dhati.

chungjo.jpg
 
Sawa, ushauri wangu nenda hospitali.
Ukutane na madaktari wa Ngozi.

Huko utapata Tiba na Ushauri zaidi.
 
Ni Hemangiomas kweli, fanya umwone Daktari wa watoto akutoe wasiwasi ulioupata google.

Huwa vinapoteaga vyenyewe.

ningekushauri uwe una piga picha kujua ukuaji wake.

na pia itakusaidia kuona mabadiliko na kama mtoto atahitaji matibabu ya haraka au asubirie tu vipotee vyenyewe.
 
Nashukuru mkuu. Nitampeleka hospitali kama nilivyoshauriwa.
Hivi huwa vinamadhara yeyote kwa mtoto?
 
Nashukuru mkuu. Nitampeleka hospitali kama nilivyoshauriwa.
Hivi huwa vinamadhara yeyote kwa mtoto?
Madhara inategemea imetokea sehemu gani mwili...mfano usoni...uwezekano wa alama ya kudumu kubakia baada ya matibabu...wengine zinakuwa kubwa sana...kiasi cha kuhitaji matibabu...onana na Daktari kwa maelezo kamili
 
Back
Top Bottom