Wakuu, Habari,
Leo nlikuwa napitia kwenye Ukuraasa wa Vodacom, nikakuta wameandika mambo mazuri kusu haya mambo ya hisa, nikaona si vibaya kushirikisha.
Hapa chini ndicho walichoandika;
=> Bila shaka kila mmoja anafahamu kwamba kampuni ya imekaribisha wawekezaji kwa kuuza asilimia 25 ya hisa
=> Tuanze kwa kufahamu hisa ni nini?
=> Kwa lugha rahisi kabisa hisa inawakilisha sehemu ya umiliki katika biashara.
=> Ukisikia mtu anasema ana hisa Vodacom kwa mfn. ni kwamba anamiliki sehemu ya mtaji wa kampuni ya Vodacom.
=> Soko la hisa ni nini? Hili ni soko la kawaida kama Soko Matola ila hili linahusisha bidhaa za kifedha.
=> Tambua kwamba hisa ni kama bidhaa nyingine zinavyouzwa sokoni kama Vitunguu au Maharage
=>Kuna aina tofauti za hisa, hisa za wamiliki, hisa za kawaida, hisa za kampuni na hisa za waanzilishi.
=> Hisa za kawaida humilikiwa na watu wengine katika kampuni, huwa wengi japo kila mtu anamiliki kidogo x2
=> Soko la hisa pia lina wanunuzi na wauzaji ambao wanakutanishwa na kufanya biashara ya hisa
=> Kwa hapa TZ linaitwa Soko la Hisa la Dar es Salaam na linasimamiwa na Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana
=> Soko la hisa kama masoko mengine lina madalali, kama
somebarry anavyoongea na dalali aweze kuuza nyanya
=> Kwenye soko la hisa madalali wanaitwa “Brokers” kisheria ndio wana uhalali wa kushiriki 1 kwa 1 kwny soko
=> Brokers” hutoa ushauri khs maamuzi ya kununua/kuuza hisa, unahitaji kuwasiliana nao kabla hujanunua hisa
=> Umeshawahi kuwasikia George Soros, Warren Buffet ambao utajiri wao umetokana na kuwekeza katika hisa?
=> Faida za hisa ni kuwa utapata gawio, utaongeza kipato na hutumika kama dhamana kuombea mikopo.
=> Hisa zinaweza kuwa kama urithi kwa watoto wako kwa maana kwamba zinahamishika.
=> Sasa tutakueleza kwanini uwezeke katika hisa za Vodacom Tanzania PLC.
=> Vodacom ina mikakati madhubuti ambayo itakuwezesha kupata faida, pitia
Vodacom investor relations - About us kufahamu.
=> Uuzwaji wa hisa za Vodacom umeanza tarehe 9 Machi na utaenda hadi tarehe 19 Aprili 2017
=> Hisa moja ya Vodacom inauzwa kwa Tsh 850 na kiwango cha chini cha umiliki ni kuanzia hisa 100.
=> Vodacom Tanzania tunauza hisa milioni 560 zenye thamani ya Tsh 476 bilioni.
=> Tuna jumla ya watumiaji 7m wa M-Pesa ambao kwa mwezi hufanya miamala inayofikia Tsh 2.6 trillioni
=> Vodacom ina wateja 12m na umiliki wa soko wa 31% na kufanya kuwa mtandao wenye soko kubwa zaidi.
=> Vodacom ina mtandao bora wa mawasiliano uliosambaa kwa asilimia 89 Tanzania nzima.
=> Vodacom Tanzania ndiyo kampuni ya simu yenye mafanikio kuliko yoyote katika sekta ya mawasiliano.
=> Uwezekezaji wa Vodacom umewesha matibabu kwa kina mama 2,000 waliokuwa na ugonjwa wa Fistula.
=> Zaidi ya Wanafunzi 6,000 wamesaidiwa kupitia masomo ya mtandao “digital learning”.
=> Zaidi ya kina mama 7,931 wamepatiwa mikopo isiyo na riba ili kuwawezesha kiuchumi.
=> Fomu za maombi zinapatikana matawi yote ya Benki ya NBC pia unaweza kuipata hapa
=>Tunawakaribisha Watanzania wote wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea kuwekeza Vodacom Tanzania PLC.