Wakuu, njoo tujielimishe kuhusu hisa za Vodacom

Sasa nikitaka kununua nafanyaje?
Process
Inabidi uwasiliane na Broker, atakupa fomu utajaza kwa kuweka taarifa zako pamoja na picha. Ukishafungua akaunti inaitwa CDS utaweza kuanza kununua hisa. Mwombaji anaweza kutuma maombi ya hisa kupitia menyu ya M-Pesa (kwa kutumia *150*00#). Wateja wa mitandao mingine wanaweza wakatumia Maximalipo kufanya manunuzi yao.
 
Mkuu kama tayari una account unaweza ukanunua Hisa nenda bank NMB nafikiri ndio watakuwa wamechukua uwakala,
ambapo hisa moja ni Tsh. 850.
NBC ndio wamechukua uwakala, but kuna baadhi ya mawakala wamewapa Mabenki mengine uwakala. Mfano Orbit Securities wamewapa Benki nyingine japo na wao still wanahusika.
 
Unaweza sio lazma nbc
Waombaji ambao hawajawa na akaunti ya hisa (CSD) watatakiwa kujisajili ili kupata akaunti waweze kununua hisa. Usajili huo unaweza kufanyika kupitia orodha (menu) ya M-Pesa au Maximalipo.
 
Sisi majaji tuna acc CRDb,naweza kwenda nunua hisa bila husisha benki?
 
Asante lakini kwanini vile vibinti vya pale Mliman city havitoi ushirikiano mpaka tunawaza kuna chezo, unamuuliza mtu maswali muhimu anakwambia kasome Prospectas, wangapi wanajua uelewa wa lugha ya biashara?
Anyway nitajaribu kupata kadhaa nione matokeo yake
mi nwenyewe nineshakumbana nao, nilichoelewa wale hawajui chochote mpaka pale nilipoamua kuonana na Afisa ndio akanipa elimu kidogo.
 
Asante sana mtoa mada.Bila shaka una shule nzuri na ni mwalewa sana.
Mada kama hizi za kujuzana kimaendeleo ndizo zitakiwazo.
Wanajamii someni hiiyo mada, ni muhimu sana kiuchumi awe mtu mmoji au Kalindi. Achaneni na mambo lawa kwa serikali! Kueni wabunifu kwa maendelio yenu
 
Inabidi uwasiliane na Broker, atakupa fomu utajaza kwa kuweka taarifa zako pamoja na picha. Ukishafungua akaunti inaitwa CDS utaweza kuanza kununua hisa. Mwombaji anaweza kutuma maombi ya hisa kupitia menyu ya M-Pesa (kwa kutumia *150*00#). Wateja wa mitandao mingine wanaweza wakatumia Maximalipo kufanya manunuzi yao.
CDS kwa kirefu ni nini?
Ni account ya nini?
Naifungua wapi, kwa garama ya sh ngapi?
Broker pia nampata wapi
Sorry kwa maswali mengi
 
CDS au "Central Depository System" ni mfumo wa kompyuta unaotomiwa na CDSC kuweka akaunti za hisa kwa njia ya kielectroniki. Akaunti hizi huwa zimefunguliwa na wamiliki hisa kwa hivyo, mara kwa mara, CDS hutumika kubadilisha hisa kutoka akaunti moja hadi nyingine wakati hisa zinaponunuliwa na kuuzwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Hivyo basi, kila mmiliki hisa katika kampuni zilizosajiliwa katika Soko la Hisa la Nairobi ni lazima awe na akaunti ya CDS illi kuweza kushiriki katika kununua na kuuza hisa.
Thanks japo tunaongelea DSE
 
Evelyn Salt

Kila wakala anayehusika na kuuza hisa hizo ana hizo fomu na hakuna gharama yoyote kujaza.

Mmoja wa wakala ni Orbit Securities wako Golden Jubilee Towers
 
...bei hiyo ya sh.850 kwa hisa moja ni kubwa sana...haswa ukizingatia bei za hisa kule DSE zimeshuka mno mno...huu si wakati muafaka kuwekeza kwenye hisa maana mfumo wa uchumi kwa utawala huu umevurugika sana....mfano ni hisa za CRDB ambazo mwaka jana kipindi kama hiki zilikuwa sh.400...leo zimeshuka hadi sh.185...hii ni mbaya sana...

...unaweza kununua hisa kwa sh.850 toka voda lakini ukashindwa kuziuza kwa bei ya juu ya hiyo...maana msingi wa faida kwenye biashara ya hisa ni kununua hisa kwa bei ya chini na kuziuza kwa bei ya juu ili kupata faida....vinginevyo hamna sababu ya kununua hisa kama huwezi kutengeneza faida..

..watu watasema hisa ni sehemu ya uwekezaji wa baadae...hili linakuwa kweli endapo mwelekeo wa soko la hisa ni chanya kule DSE...lakini kwa hali ilivyo sasa...soko la DSE liko doro mno...na wa kumlaumu ni JPM...
 
Kuna mtu aliniambia hisa wananunua wazee wenyewe hela benk et kwa kijana mdogo ni bora uzungushe hizo senti zako cuz return ya share ni ndogo sana
 
Wakuu, Habari,

Leo nlikuwa napitia kwenye Ukuraasa wa Vodacom, nikakuta wameandika mambo mazuri kusu haya mambo ya hisa, nikaona si vibaya kushirikisha.

Hapa chini ndicho walichoandika;

=> Bila shaka kila mmoja anafahamu kwamba kampuni ya imekaribisha wawekezaji kwa kuuza asilimia 25 ya hisa

=> Tuanze kwa kufahamu hisa ni nini?

=> Kwa lugha rahisi kabisa hisa inawakilisha sehemu ya umiliki katika biashara.

=> Ukisikia mtu anasema ana hisa Vodacom kwa mfn. ni kwamba anamiliki sehemu ya mtaji wa kampuni ya Vodacom.

=> Soko la hisa ni nini? Hili ni soko la kawaida kama Soko Matola ila hili linahusisha bidhaa za kifedha.

=> Tambua kwamba hisa ni kama bidhaa nyingine zinavyouzwa sokoni kama Vitunguu au Maharage

=>Kuna aina tofauti za hisa, hisa za wamiliki, hisa za kawaida, hisa za kampuni na hisa za waanzilishi.

=> Hisa za kawaida humilikiwa na watu wengine katika kampuni, huwa wengi japo kila mtu anamiliki kidogo x2

=> Soko la hisa pia lina wanunuzi na wauzaji ambao wanakutanishwa na kufanya biashara ya hisa

=> Kwa hapa TZ linaitwa Soko la Hisa la Dar es Salaam na linasimamiwa na Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana

=> Soko la hisa kama masoko mengine lina madalali, kama somebarry anavyoongea na dalali aweze kuuza nyanya

=> Kwenye soko la hisa madalali wanaitwa “Brokers” kisheria ndio wana uhalali wa kushiriki 1 kwa 1 kwny soko

=> Brokers” hutoa ushauri khs maamuzi ya kununua/kuuza hisa, unahitaji kuwasiliana nao kabla hujanunua hisa

=> Umeshawahi kuwasikia George Soros, Warren Buffet ambao utajiri wao umetokana na kuwekeza katika hisa?

=> Faida za hisa ni kuwa utapata gawio, utaongeza kipato na hutumika kama dhamana kuombea mikopo.

=> Hisa zinaweza kuwa kama urithi kwa watoto wako kwa maana kwamba zinahamishika.

=> Sasa tutakueleza kwanini uwezeke katika hisa za Vodacom Tanzania PLC.

=> Vodacom ina mikakati madhubuti ambayo itakuwezesha kupata faida, pitia Vodacom investor relations - About us kufahamu.

=> Uuzwaji wa hisa za Vodacom umeanza tarehe 9 Machi na utaenda hadi tarehe 19 Aprili 2017

=> Hisa moja ya Vodacom inauzwa kwa Tsh 850 na kiwango cha chini cha umiliki ni kuanzia hisa 100.

=> Vodacom Tanzania tunauza hisa milioni 560 zenye thamani ya Tsh 476 bilioni.

=> Tuna jumla ya watumiaji 7m wa M-Pesa ambao kwa mwezi hufanya miamala inayofikia Tsh 2.6 trillioni

=> Vodacom ina wateja 12m na umiliki wa soko wa 31% na kufanya kuwa mtandao wenye soko kubwa zaidi.

=> Vodacom ina mtandao bora wa mawasiliano uliosambaa kwa asilimia 89 Tanzania nzima.

=> Vodacom Tanzania ndiyo kampuni ya simu yenye mafanikio kuliko yoyote katika sekta ya mawasiliano.

=> Uwezekezaji wa Vodacom umewesha matibabu kwa kina mama 2,000 waliokuwa na ugonjwa wa Fistula.

=> Zaidi ya Wanafunzi 6,000 wamesaidiwa kupitia masomo ya mtandao “digital learning”.

=> Zaidi ya kina mama 7,931 wamepatiwa mikopo isiyo na riba ili kuwawezesha kiuchumi.

=> Fomu za maombi zinapatikana matawi yote ya Benki ya NBC pia unaweza kuipata hapa

=>Tunawakaribisha Watanzania wote wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea kuwekeza Vodacom Tanzania PLC.
Kwanini msiuze hisa kupitia voda pesa na pia muwe na app yenye kufanya mambo yote ya hisa na gawio na kuonyesha grafu ya kibiashara ya voda na grafu yenye kuonyesha bei ya hisa kupanda na kushuka kwake
 
Hiyo menu mbona inaitaji sanduku la post hizi huduma za kizamani za hadi mtu uwe na sanduku la post zanini
 
Wakuu, Habari,

Leo nlikuwa napitia kwenye Ukuraasa wa Vodacom, nikakuta wameandika mambo mazuri kusu haya mambo ya hisa, nikaona si vibaya kushirikisha.

Hapa chini ndicho walichoandika;

=> Bila shaka kila mmoja anafahamu kwamba kampuni ya imekaribisha wawekezaji kwa kuuza asilimia 25 ya hisa

=> Tuanze kwa kufahamu hisa ni nini?

=> Kwa lugha rahisi kabisa hisa inawakilisha sehemu ya umiliki katika biashara.

=> Ukisikia mtu anasema ana hisa Vodacom kwa mfn. ni kwamba anamiliki sehemu ya mtaji wa kampuni ya Vodacom.

=> Soko la hisa ni nini? Hili ni soko la kawaida kama Soko Matola ila hili linahusisha bidhaa za kifedha.

=> Tambua kwamba hisa ni kama bidhaa nyingine zinavyouzwa sokoni kama Vitunguu au Maharage

=>Kuna aina tofauti za hisa, hisa za wamiliki, hisa za kawaida, hisa za kampuni na hisa za waanzilishi.

=> Hisa za kawaida humilikiwa na watu wengine katika kampuni, huwa wengi japo kila mtu anamiliki kidogo x2

=> Soko la hisa pia lina wanunuzi na wauzaji ambao wanakutanishwa na kufanya biashara ya hisa

=> Kwa hapa TZ linaitwa Soko la Hisa la Dar es Salaam na linasimamiwa na Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana

=> Soko la hisa kama masoko mengine lina madalali, kama somebarry anavyoongea na dalali aweze kuuza nyanya

=> Kwenye soko la hisa madalali wanaitwa “Brokers” kisheria ndio wana uhalali wa kushiriki 1 kwa 1 kwny soko

=> Brokers” hutoa ushauri khs maamuzi ya kununua/kuuza hisa, unahitaji kuwasiliana nao kabla hujanunua hisa

=> Umeshawahi kuwasikia George Soros, Warren Buffet ambao utajiri wao umetokana na kuwekeza katika hisa?

=> Faida za hisa ni kuwa utapata gawio, utaongeza kipato na hutumika kama dhamana kuombea mikopo.

=> Hisa zinaweza kuwa kama urithi kwa watoto wako kwa maana kwamba zinahamishika.

=> Sasa tutakueleza kwanini uwezeke katika hisa za Vodacom Tanzania PLC.

=> Vodacom ina mikakati madhubuti ambayo itakuwezesha kupata faida, pitia Vodacom investor relations - About us kufahamu.

=> Uuzwaji wa hisa za Vodacom umeanza tarehe 9 Machi na utaenda hadi tarehe 19 Aprili 2017

=> Hisa moja ya Vodacom inauzwa kwa Tsh 850 na kiwango cha chini cha umiliki ni kuanzia hisa 100.

=> Vodacom Tanzania tunauza hisa milioni 560 zenye thamani ya Tsh 476 bilioni.

=> Tuna jumla ya watumiaji 7m wa M-Pesa ambao kwa mwezi hufanya miamala inayofikia Tsh 2.6 trillioni

=> Vodacom ina wateja 12m na umiliki wa soko wa 31% na kufanya kuwa mtandao wenye soko kubwa zaidi.

=> Vodacom ina mtandao bora wa mawasiliano uliosambaa kwa asilimia 89 Tanzania nzima.

=> Vodacom Tanzania ndiyo kampuni ya simu yenye mafanikio kuliko yoyote katika sekta ya mawasiliano.

=> Uwezekezaji wa Vodacom umewesha matibabu kwa kina mama 2,000 waliokuwa na ugonjwa wa Fistula.

=> Zaidi ya Wanafunzi 6,000 wamesaidiwa kupitia masomo ya mtandao “digital learning”.

=> Zaidi ya kina mama 7,931 wamepatiwa mikopo isiyo na riba ili kuwawezesha kiuchumi.

=> Fomu za maombi zinapatikana matawi yote ya Benki ya NBC pia unaweza kuipata hapa

=>Tunawakaribisha Watanzania wote wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea kuwekeza Vodacom Tanzania PLC.
Hisa mil560 ?? Nani ana mamlaka ya kuweka idadi ya hisa zinazouzwa mfano voda wakisema wanauza hisa mil 8000 = bil8 kwa sh850 kila hisa huo utakuwa ufisadi kwa pesa za wananchi nisawa mm niwe na biashara ya genge niuze hisa mil 4 kila hisa sh 500 ??? Mm namashaka sana na biashara ya hisa kama siyo ufisadi wa kimataifa na kuzidi kuyanufaisha makampuni kwa kuwanyonya wananchi
 
kuna mahali nilisikia kwamba kama kampuni inapata hasara ,wanaokua wa kwanza kupata hasara au hata kupoteza hisa zao ni wale wenye hisa ndogo katika kampuni husika.naomba kufafanuliwa hapa
 
mimi naamini kuwekeza kwa kununua hizi hisa kuna faida voda ni linakua sana kuingiza hasara sidhani
 
Back
Top Bottom