Haya Mimi nahitaji kujuaCDS ndio nini
Inakwambia vipi mkuu. Pole
Wakuu, Habari,
Leo nlikuwa napitia kwenye Ukuraasa wa Vodacom, nikakuta wameandika mambo mazuri kusu haya mambo ya hisa, nikaona si vibaya kushirikisha.
Hapa chini ndicho walichoandika;
=> Bila shaka kila mmoja anafahamu kwamba kampuni ya imekaribisha wawekezaji kwa kuuza asilimia 25 ya hisa
=> Tuanze kwa kufahamu hisa ni nini?
=> Kwa lugha rahisi kabisa hisa inawakilisha sehemu ya umiliki katika biashara.
=> Ukisikia mtu anasema ana hisa Vodacom kwa mfn. ni kwamba anamiliki sehemu ya mtaji wa kampuni ya Vodacom.
=> Soko la hisa ni nini? Hili ni soko la kawaida kama Soko Matola ila hili linahusisha bidhaa za kifedha.
=> Tambua kwamba hisa ni kama bidhaa nyingine zinavyouzwa sokoni kama Vitunguu au Maharage
=>Kuna aina tofauti za hisa, hisa za wamiliki, hisa za kawaida, hisa za kampuni na hisa za waanzilishi.
=> Hisa za kawaida humilikiwa na watu wengine katika kampuni, huwa wengi japo kila mtu anamiliki kidogo x2
=> Soko la hisa pia lina wanunuzi na wauzaji ambao wanakutanishwa na kufanya biashara ya hisa
=> Kwa hapa TZ linaitwa Soko la Hisa la Dar es Salaam na linasimamiwa na Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana
=> Soko la hisa kama masoko mengine lina madalali, kama somebarry anavyoongea na dalali aweze kuuza nyanya
=> Kwenye soko la hisa madalali wanaitwa “Brokers” kisheria ndio wana uhalali wa kushiriki 1 kwa 1 kwny soko
=> Brokers” hutoa ushauri khs maamuzi ya kununua/kuuza hisa, unahitaji kuwasiliana nao kabla hujanunua hisa
=> Umeshawahi kuwasikia George Soros, Warren Buffet ambao utajiri wao umetokana na kuwekeza katika hisa?
=> Faida za hisa ni kuwa utapata gawio, utaongeza kipato na hutumika kama dhamana kuombea mikopo.
=> Hisa zinaweza kuwa kama urithi kwa watoto wako kwa maana kwamba zinahamishika.
=> Sasa tutakueleza kwanini uwezeke katika hisa za Vodacom Tanzania PLC.
=> Vodacom ina mikakati madhubuti ambayo itakuwezesha kupata faida, pitia Vodacom investor relations - About us kufahamu.
=> Uuzwaji wa hisa za Vodacom umeanza tarehe 9 Machi na utaenda hadi tarehe 19 Aprili 2017
=> Hisa moja ya Vodacom inauzwa kwa Tsh 850 na kiwango cha chini cha umiliki ni kuanzia hisa 100.
=> Vodacom Tanzania tunauza hisa milioni 560 zenye thamani ya Tsh 476 bilioni.
=> Tuna jumla ya watumiaji 7m wa M-Pesa ambao kwa mwezi hufanya miamala inayofikia Tsh 2.6 trillioni
=> Vodacom ina wateja 12m na umiliki wa soko wa 31% na kufanya kuwa mtandao wenye soko kubwa zaidi.
=> Vodacom ina mtandao bora wa mawasiliano uliosambaa kwa asilimia 89 Tanzania nzima.
=> Vodacom Tanzania ndiyo kampuni ya simu yenye mafanikio kuliko yoyote katika sekta ya mawasiliano.
=> Uwezekezaji wa Vodacom umewesha matibabu kwa kina mama 2,000 waliokuwa na ugonjwa wa Fistula.
=> Zaidi ya Wanafunzi 6,000 wamesaidiwa kupitia masomo ya mtandao “digital learning”.
=> Zaidi ya kina mama 7,931 wamepatiwa mikopo isiyo na riba ili kuwawezesha kiuchumi.
=> Fomu za maombi zinapatikana matawi yote ya Benki ya NBC pia unaweza kuipata hapa
=>Tunawakaribisha Watanzania wote wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea kuwekeza Vodacom Tanzania PLC.
CDS ni akaunti ambayo kwa kirefu ni "Central Depository System"
Ni akaunti ya Usajili ili utambulike kama Mnunuzi
Unaifungua kwenye mtandao na hakuna gharama kuifungua
Breaker wapo zaidi ya kumi wengi wapo. Mtaa wa Samora Dar Es Salaam ila yupo wa Serikali anaitwa TIB Investiment kampuni dada ya TIB Bank. Ukihitaji Fomu naweza kukutumia.
Kwanini mkuu?Kwa ufupi mim sishauri mtu anunue share za vods
Kwanini?Kwa ufupi mim sishauri mtu anunue share za vods
Haya Mimi nahitaji kujua
Duh... ngoja nisubirie majibu ya wadau maana ndo nlikuwa kwenye mchakato wa kujisajili.Wiki iliyopita nilijiunga na DSE (soko la hisa la Dsm) kwa simu yangu. Kwa kupiga *150*36# nikafata maelekezo ya kujiunga ili ninunue hisa za vodacom. Nilifanikiwa kujiunga lakini sikununua hisa kwa sababu sikuwa na pesa za kununua kwenye simu yangu. Wakati nilipohitaji kuweka pesa ili ninunue angalau hisa 100 watu wakaribu walinishauri kuwa niachane na mambo ya hisa hizo hazina faida, na baadae nikasikia redioni kuwa ununuzi wa hisa una changamoto. Niwasiliane na mshauri wa uchumi.
Naombeni msaada, ninunue au ndo itakula kwangu. Maana saivi zinakuja sms za kunitaka ninunue
Nadhani kupitia Usajili huo huo wanaweza kukutumia Fomu ukajaza. Njia zote ni sawa angalia utakayo weza na rahisi kwakoKama najisajili kwa kutumia simu (*150*36#) bado ntahitaji kujaza hiyo fomu unayosema unaweza kunitumia??
Sijawahi kujuta tangu nianze kununua hisa na kwa sasa nime nunua za kutosha kwa kuwa ndio biashara ninayoiweza naamini hao walio kushauri uachane nazo hawazijui. Lakini kama ukiwa na WASI WASI kwa kuwa zikiingia sokoni mwezi ujao tar 16 bei ilivyo panda utaiona kupitia simu yako ya kiganjani utagundua wamekukosesha fedha. Itakulazimu kusubiri hadi za Airtel, Tigo, Zantel na Halotel zikitangazwa kwani nazo zitauzwa mwaka huu (kwa mujibu wa sheria ya Bunge 25%)Duh... ngoja nisubirie majibu ya wadau maana ndo nlikuwa kwenye mchakato wa kujisajili.
Hivi unafikri kwanini Wanasema Kwenye Tangazo lao . Kuwa Soko la Hisa Linachangamoto Nyingi. Uwasiliane na Mshauri wako wa Kifedha??mimi naamini kuwekeza kwa kununua hizi hisa kuna faida voda ni linakua sana kuingiza hasara sidhani
return inategemea na performance ya shirika inaweza kuwa kubwa au ndogo au isiwepo kabisa iwe ni hasara....kwa mfano hisa za CRDB sasa hivi hakuna return ni loss tuKuna mtu aliniambia hisa wananunua wazee wenyewe hela benk et kwa kijana mdogo ni bora uzungushe hizo senti zako cuz return ya share ni ndogo sana
Faida ya voda inashuka kila mwaka sana sana mwaka juzi iliporomoka sana kutokana na halotel kuingia kazini, na Airtel Money na Tigopesa kuwa na huduma sawa na za voda.Kwanini mkuu?
mkuu nimetoa sababu kne reply ya mtu hapahapa. icheki plzKwanini?
[emoji15] ikiwa hakuna faida.imekula kwako.hata ile hela yako hairudi?return inategemea na performance ya shirika inaweza kuwa kubwa au ndogo au isiwepo kabisa iwe ni hasara....kwa mfano hisa za CRDB sasa hivi hakuna return ni loss tu
return ni ile faida ndio mnagawana wana hisa....sasa kama hamna faida mtagawana nini mkuu...mtagawana mtaji[emoji15] ikiwa hakuna faida.imekula kwako.hata ile hela yako hairudi?
Quoted "Haya Mimi nahitaji kujua
Bora kibubu.upuuzi huu.labda ile hela yangu wangerudisha tukipata hasara hapo sawareturn ni ile faida ndio mnagawana wana hisa....sasa kama hamna faida mtagawana nini mkuu...mtagawana mtaji