Quoted "
CDS au "Central Depository System" ni mfumo wa kompyuta unaotomiwa na CDSC kuweka akaunti za hisa kwa njia ya kielectroniki. Akaunti hizi huwa zimefunguliwa na wamiliki hisa kwa hivyo, mara kwa mara, CDS hutumika kubadilisha hisa kutoka akaunti moja hadi nyingine wakati hisa zinaponunuliwa na kuuzwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.
Hivyo basi, kila mmiliki hisa katika kampuni zilizosajiliwa katika DSE ni lazima awe na akaunti ya CDS illi kuweza kushiriki katika kununua na kuuza hisa."