WAKUU TIBA GANI INAHITAJIKA ?

WAKUU TIBA GANI INAHITAJIKA ?

MKUYENGE

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2019
Posts
4,107
Reaction score
4,612
wakuu naombeni msaada wa jinsi ya kumsaidia huyu shemeji yangu mdogo wake na mme wa sister kiufupi jamaa alikuwa mzima kabisa tatizo lilimuanza mwaka jana baada ya kuanza kusoma chuo hapo Gongolamboto Kampala.

kiufupi jamaa anamatatizo ya akili ambayo yameanza kumsumbua mwaka Jana mwezi wa 6 kwao wamehangaika sana Kwa wanganga lakini akipona ni kama mwezi alafu anarudia tena hali ya kuwehuka.

hali hiyo imemplekea kushindwa kuendelea na masomo yake ya elimu ya juu.

kwao wamejaribu kuzunguka kutafuta tiba ya kila (aina) zote mnazozifahamu lakini zimeshindwa kumsaidia kabisa ata akikaa VIZURI ni kwa week au mwezi tu anachange.

kilichonisikitisha zaidi ni Leo baada ya hali yake kubadirika week iliyopita asubhi ikanibidi niende nikamjulie hali aliponiona alifurahi sana kutokana na kuwa ni washikaji tukaanza kupiga story akawa kama katulia flani akaanza kuniuliza issues za mpira league yetu EPL matokeo ya team yake pendwa Manchester city na nikwamwambia akafurahi baadae akawa anataka tuondoke wote wakati ulipofika kuwa kachoka kukaa ndani wakamkatalia infact bado hajakaa sawa jamaa alisikitika sana

akaanza kuongea maneno ya ajabu nikamtuliza akakubari niende lakini la muhimu jamaa hajapona kabisa nimeandika kwenu ili mnipe msaada wa kimawazo jinsi ya kumsaidia kama kijana mwenzetu ili arudi katika hali yake ya kawaida.

wenu mtiifu
 
Naona ni wakati mzuri kabisa wa kumgeukia Mungu naye atatenda kwa ajili ya Utukufu wake. Kwani kwake hakuna linaloshindikana hakuna. Mpelekeni kwenye maombi hakika atafunguliwa na kuwekwa huru.
 
Tunatakiwa tujue vitu vifuatavyo

1.Alizaliwa na huo ugonjwa au lah?

2.Ulimuanza lini na ilikuaje?

THEN

kwa upande wangu siamini ushirikina so Nashauri apelekwe hospital kitengo cha magonjwa ya Akili watakupa majibu na cha kufanya.

Wale wengine wana SOLUTION nadhani watakuja...Fata njia zote kikubwa ndugu yako APONE.
 
Hospital wakishindwa MUNGU hashindwi...hata bila kwenda hospital huyu mtoa mada kama ana imani anaweza kwenda kusema kitu na mgonjwa akapokea...

yahitaji imani ndogo sana kama kale ka punje ka mchele.
 
Maneno ya ajabu anayotamka ni kama yapi?
 
Tunatakiwa tujue vitu vifuatavyo

1.Alizaliwa na huo ugonjwa au lah?

2.Ulimuanza lini na ilikuaje?

THEN

kwa upande wangu siamini ushirikina so Nashauri apelekwe hospital kitengo cha magonjwa ya Akili watakupa majibu na cha kufanya.

Wale wengine wana SOLUTION nadhani watakuja...Fata njia zote kikubwa ndugu yako APONE.
hakuzaliwa nao ameanza kuugua mwaka jana tu mkuu
 
Hospital wakishindwa MUNGU hashindwi...hata bila kwenda hospital huyu mtoa mada kama ana imani anaweza kwenda kusema kitu na mgonjwa akapokea...

yahitaji imani ndogo sana kama kale ka punje ka mchele.

Kabisa kabisa MUNGU hashinndwi na hajwahi kushindwa na haitatokea ni Imani yake, ninahuakika huyo kaka atapata uponyaji kabisa.
 
atakuwa ana majini muone mzee khalfan ilala mtaa wa mtwara atasomewa itaisha
 
unapokutana na comment kama hizi usizipuuze sawa mkuu MKUYENGE

zifanyie kazi tena anza na tiba kwa imani then Hospital Visomo/maombi then Hospital...
 
Akili ya mwanadamu inapofika mwisho Mungu ndoanaanzia hapo kuonyesha utukufu wake mpeleke kanisani lipo tumaini kwake
 
wakuu naombeni msaada wa jinsi ya kumsaidia huyu shemeji yangu mdogo wake na mme wa sister kiufupi jamaa alikuwa mzima kabisa tatizo lilimuanza mwaka jana baada ya kuanza kusoma chuo hapo Gongolamboto Kampala.

kiufupi jamaa anamatatizo ya akili ambayo yameanza kumsumbua mwaka Jana mwezi wa 6 kwao wamehangaika sana Kwa wanganga lakini akipona ni kama mwezi alafu anarudia tena hali ya kuwehuka.

hali hiyo imemplekea kushindwa kuendelea na masomo yake ya elimu ya juu.

kwao wamejaribu kuzunguka kutafuta tiba ya kila (aina) zote mnazozifahamu lakini zimeshindwa kumsaidia kabisa ata akikaa VIZURI ni kwa week au mwezi tu anachange.

kilichonisikitisha zaidi ni Leo baada ya hali yake kubadirika week iliyopita asubhi ikanibidi niende nikamjulie hali aliponiona alifurahi sana kutokana na kuwa ni washikaji tukaanza kupiga story akawa kama katulia flani akaanza kuniuliza issues za mpira league yetu EPL matokeo ya team yake pendwa Manchester city na nikwamwambia akafurahi baadae akawa anataka tuondoke wote wakati ulipofika kuwa kachoka kukaa ndani wakamkatalia infact bado hajakaa sawa jamaa alisikitika sana

akaanza kuongea maneno ya ajabu nikamtuliza akakubari niende lakini la muhimu jamaa hajapona kabisa nimeandika kwenu ili mnipe msaada wa kimawazo jinsi ya kumsaidia kama kijana mwenzetu ili arudi katika hali yake ya kawaida.

wenu mtiifu
mkuu nenda pale msikiti wa Tumbi Temeke mtafute mtu aitwa Darwesh naiman atamsaidia ...ana gharama kiac lakin hiyo sentensi ya kwamba muwaache hawatoki....wataibadilisha wataomba kuondoka wenyew ....na hawatarud ....polen sana mkuu.
 
Back
Top Bottom