Wakuu Tujifunze Kuendesha Ndege Tuepuke Vifo Vya Kipumbavu

Wakuu Tujifunze Kuendesha Ndege Tuepuke Vifo Vya Kipumbavu

kinachotuponza watanzania sio watu wa kuchangamsha ubongo ukishakuwa mhasibu huwezi hata kufunga dish
 
kinachotuponza watanzania sio watu wa kuchangamsha ubongo ukishakuwa mhasibu huwezi hata kufunga dish
Kwenye... multi tasking au multi skills ni kitu kinachotushinda wabongo...

Mzungu unaweza kumkuta leo ni engineer wa ujenzi kesho kutwa kabadili fani amekuwa Pilot au anafanya kazi shirika la NASA safari za mwezini.

Bongo ukishakuwa mwenyekiti wa mtaa, unataka uwe mwenyekiti wa mtaa mpaka uzeeni
 
Kama ilivyo siku hizi, karibu kila mtaa kuna dereva wa gari au pikipiki. Ni vyema tukajitahidi kujifunza hata basic za ku-control ndege. 😂

Unakuta pilots wamepigana au wamekufa, nyie abiria mnaangalia tu. Mnashindwa hata mmoja kushika controls kwa sababu hakuna anayejua kuendesha ndege. Mwisho wa siku mnakodoleana macho, mchanganyiko wa maombi unaanza: “Yesu wangu, Mtume, Mungu wangu, Ya Rabbi, Ya Allah…” 😂

Ukiangalia kwa mfano wa tukio lililotokea huko Saudi Arabia angani, baada ya pilots kuchambana na hali kufikia hatua ya kuanza kupigana, abiria mmoja alijaribu kushika controls huku pilots wakiendelea kurushiana makonde.

Sasa fikiria kama jambo kama hili lingetokea Bongo kwenye Air Tanzania. Abiria wote wangekaa kimya kwa sekunde chache, halafu kila mtu angeanza kuomba kwa lugha yake. 😂

Tofauti na gari ambalo likipata ajali, impact inaweza kutokea ndani ya sekunde chache, ndege iko angani ikiwa na muda fulani wa kufanya maamuzi na kuchukua hatua. Ndege nyingi za abiria husafiri kwenye altitude ya takribani futi 30,000 hadi 42,000—sawa na karibu kilomita 9 hadi 13 juu ya usawa wa bahari.

Kwa hiyo, kama mambo yamevurugika ndani ya cockpit, iwe ni pilots wamepata tatizo, wamejeruhiwa au kuna hali nyingine ya dharura, angalau abiria mmoja akiwa na basic knowledge anaweza kusaidia kuelewa controls na kuwasiliana na air traffic control.

Wenzetu, utakuta hata madogo wanajua kusukuma Boeing bila masihara. Na wengine wameanza kujifunza kupitia flight simulators tu. 😂

Sisi huku? Ukiona ndege inaanza kuyumba kidogo, mtu anaanza: “Ya Rabbi! Ya Allah! Yesu wangu!” 😭😂
Wewe mjinga Sana, yaani watu wajifunze urubani kisa kuna marubani watauana kwenye ndege ndo wao wapate nafasi ya kuongoza ndege siku hiyo?
Uhaya!
 
Back
Top Bottom