Wakuu tunaomba matokeo kombe la Dunia- Huku kwetu hakuna umeme

Wakuu tunaomba matokeo kombe la Dunia- Huku kwetu hakuna umeme

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Wakuu heshima sana.

Huku kwetu madongo kuinama hukuna umeme.

Mitaa ya matejoo,Kambi ya Fisi,Matevesi,Olkeriani,Olkokola,Kaloleni,Ngarenaro,Daraja II,Mkonoo na vitongoji vingi hakuna umeme.

Kwakuwa Sisi waTanzania tumejaa upendo,tunawaomba wale wote waliojaliwa kumiliki majenereta wasisite kutupatia matokeo ya kombe la Dunia huko Qatar 🇶🇦.

Ikiwezekana mturushie hata tupicha.
Hongera sana Mama unaupiga mwingi.
Hongera sana Makamba JR unaupiga mwingi.

Huku kwetu haturuhusiwi kukosoa ni mwendo wa kusifu tu.
Tunaogopa sana kupopolewa na mimaneno ya Katibu Mkuu UVCCM,Kibajaji & Msukuma.
 
Pole sana mkuu, mimi nipo shamba nadhani tungojee updates zaidi
 
Nchi hii imeoza sana.hata kwetu huku umeme wamekata toka Saa NNE asubuhi hadi sasa hawajarudisha.Duh. ufunguzi wa FIFA nimeukosa.Hii awamu ni balaa tupu
 
Hatarii... Hii ndo maana halisi ya CHAMA CHAKAVU...CCM...
MI NAUSHUKURU MBADALA WANGU WA SOLAR...

UMEME HAMNA KOOTEE
 
FT Taifa stars ya Qatar0-2 Equador.

Equador wamenyimwa goli la wazi dk ya pili kipindi cha kwanza,wahuni wa huko kina Elli Sasi na Kayoko wakadai ni offside.
 
Back
Top Bottom