Behaviourist
JF-Expert Member
- Apr 8, 2016
- 39,926
- 95,626
Wakuu nawasalimu katika jina la jukwaa hili.Nina changamoto fulani ambayo ningependa mnisaidie katika haya masuala ya uendeshaji wa magari ya automatic.
Mimi sina mda mrefu tokea nijifunze kuendesha magari na tokea pia nianze kuendesha magari.Kwa hiyo sina uzoefu katika kuendesha magari.Naishi katika mji fulani hapa Tanzania na safari zangu huwa ni kutoka nyumbani kuelekea ofisini,ofisini nyumbani au kutoka nyumbani kwenda bar.Kwa hiyo gari muda wote huwa naendeshia katika gear ya D(Automatic transmission)
Sijawahi kuendesha gari katika maeneo yenye milima mikubwa na ya kutisha na kushuhudia pamoja na kujifunza changamoto zake.Sasa shida inaanzia hapa,wiki ijayo nina safari fulani ya kijijijini.Huko ninakotaka niende ni kilomita 30 kutoka hapa mjini na hilo eneo ni barabara ya vumbi yenye vilima vinavyotisha sana na vyenye kona nyingi.Yaani katika huo umbali wa kilomita 30,asilimia 90 ya barabara hiyo ni kilima cha kutisha na chenye kona nyingi.Gari likiwa linapanda hayo maeneo unaweza kufikiri ya kuwa linataka kubinuka.
Sasa wakuu maswali yangu kwenu ni haya:
1.Je ninaweza kuendesha gari kwenye huo umbali wa vilima wa kilomita 30 kwa kutumia gear namba D peke yake (Automatic transmission)bila ya kubadili kwenda manual?Na kama ninatakiwa kubadili somewhere kwenda manual ni kwa nini?Ina maana automatic transmission haijitoshelezi?
2.Je ninaweza kuiamini gear namba D na nikaitumia kuclear eneo lote la milima katika hiyo safari yangu?Je kuna hasara yoyote kwa gari kwa kuendesha safari nzima ya milima kwa kutumia automatic transmission peke yake bila ya kubadili kwenda manual?Gari ni hizi babywalker.
Shukrani