Wakuu ushauri wenu ni muhimu, nimefilisika

P
Pole mkuu
 
Awamu hii kila goti litapigwa mbaya zaidi jamaa kasha tamka hana mpango wa kuondoka
 
Huu ndio uanaume
 
Kupanda na kushuka Ni kawaida katika maisha..
Muombe MUNGU akupe njia za kutokea..na ukiamua kumtegemea Yeye Basi umtegemee usiende Tena kwa waganga wa kienyeji.
Fanya kazi kwa bidii kulingana na mipango utakayoiweka...mwambie Mungu abariki kazi za mikono yako.
 
Hatar sana!
 
Sure!
 
Cjui umri wako. Cjui uzoefu wako kwenye game la biashara. Ila kwenye haya mambo unavyoyatazama sivyo yaonekanavyo.
Nina mifano ilyokuwa hai kwenye hili, shukrani kwa Mshanajr kwa ushauri yakinifu.
Mtu yeyote anayeamini amini sana Mungu na ushirikina, akiwa masikini siwezi kushangaa.

Mentality yake tu, epistemology yake tu, imejikita kwenye umasik8ni.
 
Pole sana. Kwanza fanya hivi kaa kimya kama nusu saa au lisa tafakari uweza wa Mungu, uzima ulio nao huna ulemavu, unapumua, una viungo vyote(Tabasamu). Mshukuru Mungu piga magoti hapo ulipo sali/swali hata kwa dakika 10 omba msahama kwa Mungu.

Baada ya hapo fikiria njia ya kutokea, tafuta kitu cha kufanya, kwanza fikiria biashara yeyote hata kama ni ndogo ila sio saaana mfano unaweza tafuta familia 3 mpaka 10 za kuwaletea fresh fruits , samaki fresh na vyakula vingine kila wiki au kwa muda fulani , unawapelekea vile vya high quality grade 1 unakwenda sokoni mwenyewe na baharini(unauzoefu kidogo) nunua vile vyakula vizuri sana kama mbogamboga fulani hivi ambazo mtaani hazipo sana , matunda kama zabibu, machungwa mazuri kama ya SA, Apple n.k ukiwa na familia 10 na ukaweza kuzihudumia vizuri kabisa unaweza pata njia ya kusonga. Hii biashara inaweza kuwa nzuri kwako kwa sababu kwanza hukai na bidhaa ndani usema ziharibika wewe unakusanya oda unaenda sokoni na baharini unaleta kwa mteja. Jenga uaminifu, jali muda na heshima kwa mteja.

Huu ni ushauri wangu tuu unaweza tizima biashara zaidi ya hii.

Zaidi: Mrudie Mungu fanya ibada vizuri kaa na familia yako karibu, mfarijianeni na mchape kazi saaaana usikeshe kwenye majumba ya ibada, vijiweni, kwa waganga ukidhani ndio utafanikiwa , sali/swali kwa muda wa ibada ,tumia muda vizuri sana pale penye nafasi piga kazi sana na usiangalie nyuma, shindana na nafsi na akili (zina tabia ya kubishana sana)

Achana na waganga na imani za kishirikina utahadhibiwa na Mungu na unaweza potea kwenye huu ulimwengu kirahisi sana.

Mwisho Mungu ni wetu sote, naomba akukumbuke na familia yako, naomba akupe wepesi na uvumilivu na msamaha.

Kila la kheri kaka.[emoji120]
 
Cjui umri wako. Cjui uzoefu wako kwenye game la biashara. Ila kwenye haya mambo unavyoyatazama sivyo yaonekanavyo.
Nina mifano ilyokuwa hai kwenye hili, shukrani kwa Mshanajr kwa ushauri yakinifu.
Unavyoyatazama haya mambo nalo ni tatizo.

Mshana Jr. naye ni mlozi tu aliyeshindwa hoja hapa.
 
Pole Sana mkuu.Hizo ni moja ya stage za maisha.Am sure ukija inuka Tena, hutoanguka Tena.Usisahau pia kumuomba Sana MUNGU akufungulie Milango iliyofungwa
 
Mtu yeyote anayeamini amini sana Mungu na ushirikina, akiwa masikini siwezi kushangaa.

Mentality yake tu, epistemology yake tu, imejikita kwenye umasik8ni.
Fafanua mkui Kiranga? Je unatakiwa kuamini nn ili ufanikiwe au usiwe masikini.
 
Cjui umri wako. Cjui uzoefu wako kwenye game la biashara. Ila kwenye haya mambo unavyoyatazama sivyo yaonekanavyo.
Nina mifano ilyokuwa hai kwenye hili, shukrani kwa Mshanajr kwa ushauri yakinifu.
Luis elezea basi na sisi tupate kujua what is inside ulimwengu wa fedha unamambo na sayansi zake nyingi sana
 
Kiauhalisia biashara nyingi si rahisi sana hasa mwanzoni,kikubwa unachotakiwa kukifahamu ni kwamba ni vyema wakati unaanzisha biashara uwe umejiandaa kisaikolojia wewe kama mjasiriamali maana biashara inapofeli ni kwamba wewe mmiliki binafsi ndo umefeli lakini si biashara imefeli,wakati unanzisha lazima ujiandae kuhustle kweli kweli hasa mwanzoni hivyo ukijiandaa kisaikolojia changamoto yeyote utakayokutana nayo unayojua ni part of the process hivyo ni kujichukualia somo kwenye kila changamoto unayokutana nayo,wajasiriamali wengi tuna kwama hapa,HATUJIANDAI KISAIKOLOJIA.
Kikubwa nachokiona ulichokosea mwanzoni na kazi yako ya Udalali ni KUKATA TAMAA,Usingetakiwa kukata tamaa maana ndiyo kazi yako iliyokupatia vyote ulivyokuwa navyo na hii inarudi pale pale kwamba hukujiandaa kisaikolojia kwamba sometimes mambo huwa yanakwenda na kuna muda yanakwama,nini tunachotakiwa kufanya pindi mambo yakiwa yanaenda vizuri na nini tunachotakiwa kufanya pindi mambo hayaendi vizuri.Ukiwa mtu wa kukata tamaa huwezi kutoboa na biashara yeyote,chagua kitu kimoja pambana nacho kufa na kupona hata miaka 10 iko siku itajipa tuu,,sio leo unahili unaona haliendi sawa kesho unalingine.Katika biashara kuna kipindi hufikia ambacho faida unayoitengeneza kwa mwezi mmoja ni faida uliyokuwa unatengeneza kwa mwaka mzima kwa miaka kazaa iliyopita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…