Wakuu ushauri wenu ni muhimu, nimefilisika

Wakuu ushauri wenu ni muhimu, nimefilisika

P
Unashangaa nini mbona sisi mzee wetu alikua akimiliki mpaka sheli na gereji miaka ya 90,Hajakaa vizuri akala mzinga na gari yake kwa mawazo,,hajatulia akavamiwa na majambazi risasi 4 ziliingia mwilini mwake Mungu akasaidia yuko hai mpaka leo ila kilema hapo akazidi kufilisika. japo ana pesa tudogo za kula na kuvaa lakini sio yule waliokuwa wanamfahamu uko nyuma.
Pole mkuu
 
Awamu hii kila goti litapigwa mbaya zaidi jamaa kasha tamka hana mpango wa kuondoka
 
Haupo peke yako mkuu mimi nimekuja hadi kuomba msaada wa laptop humu wakati zamani nilikua na uwezo wa kununua hata laptop 10 kwa mara moja,kuhusu gari hapo ndii usiseme...kubali matokeo kwani hapo sio kituo hilo ni tukio tu..
Kwenye universal laws naona kosa jingine umelifanya siku ya jumapili umevunja sheria inautwa THE LAW OF CORRESPONDANCE (sheria ya usawa& ulinganifu). Amini Dunia yetu ya nnje ni matokeo ya Dunia yetu ya ndani.kitu kikubwa kinaundwa na vitu vidogo vidogo..
Show gratitude for what you have,shukuru kwa kile ulicho nacho kwani usiposhukuru ulimwengu utakunyang'anya usicho kithamini..Jumapili umeshindwa kukithamini kile kidogo ulicho nacho ukaamua kukitoa chote manaake hujaweka usawa..hakikisha unavyosaidia kuna kitu kitu unabaki nacho..
Mimi nilipoteza marafiki,mpenzi,majirani mpaka baadhi ya ndugu nilikata tamaa nikatamani kujiua si unajua sisi wahehe tena,badae nilivyogundua sina nilichopungukiwa mwilini nipo safi nikajiona fala nikawa tayari kufanya kazi yoyote bila kijari elimu wala nafasi nillikuwa nayo hapo nyuma..Mungu si athumani bado yupo pamoja nami.
Note: nilizikamata pesa nikiwa na umri mdogo 20 namiliki maduka mawili,kiwanja kimoja na pagala moja,gari ya kutembelea,navyosema gari sio vits,paso,duet,starlet..hakuna maisha matamu kama opportunity inakuja kukiwa na preparation.
Nikukumbushe tu kwamba hakuna ulichopoteza ila umejifunza
Huu ndio uanaume
 
Kupanda na kushuka Ni kawaida katika maisha..
Muombe MUNGU akupe njia za kutokea..na ukiamua kumtegemea Yeye Basi umtegemee usiende Tena kwa waganga wa kienyeji.
Fanya kazi kwa bidii kulingana na mipango utakayoiweka...mwambie Mungu abariki kazi za mikono yako.
 
bro umeanguka mara 1..thomas edison alianguka mara 10000..hapo unazidi kukomaa..ginapozidi basi ujue mwanga ndo unakaribia...NB;inaeza kua vita ya kiroho kukufanya uwe na hali mbaya kiuchumi,,wakitoka hapo wanapiga ndoa afu wanapiga afya..asee wachawi noma sana..omba sana mzee kama ni vita ya kiroho
Hatar sana!
 
Haupo peke yako mkuu mimi nimekuja hadi kuomba msaada wa laptop humu wakati zamani nilikua na uwezo wa kununua hata laptop 10 kwa mara moja,kuhusu gari hapo ndii usiseme...kubali matokeo kwani hapo sio kituo hilo ni tukio tu..
Kwenye universal laws naona kosa jingine umelifanya siku ya jumapili umevunja sheria inautwa THE LAW OF CORRESPONDANCE (sheria ya usawa& ulinganifu). Amini Dunia yetu ya nnje ni matokeo ya Dunia yetu ya ndani.kitu kikubwa kinaundwa na vitu vidogo vidogo..
Show gratitude for what you have,shukuru kwa kile ulicho nacho kwani usiposhukuru ulimwengu utakunyang'anya usicho kithamini..Jumapili umeshindwa kukithamini kile kidogo ulicho nacho ukaamua kukitoa chote manaake hujaweka usawa..hakikisha unavyosaidia kuna kitu kitu unabaki nacho..
Mimi nilipoteza marafiki,mpenzi,majirani mpaka baadhi ya ndugu nilikata tamaa nikatamani kujiua si unajua sisi wahehe tena,badae nilivyogundua sina nilichopungukiwa mwilini nipo safi nikajiona fala nikawa tayari kufanya kazi yoyote bila kijari elimu wala nafasi nillikuwa nayo hapo nyuma..Mungu si athumani bado yupo pamoja nami.
Note: nilizikamata pesa nikiwa na umri mdogo 20 namiliki maduka mawili,kiwanja kimoja na pagala moja,gari ya kutembelea,navyosema gari sio vits,paso,duet,starlet..hakuna maisha matamu kama opportunity inakuja kukiwa na preparation.
Nikukumbushe tu kwamba hakuna ulichopoteza ila umejifunza
Sure!
 
Cjui umri wako. Cjui uzoefu wako kwenye game la biashara. Ila kwenye haya mambo unavyoyatazama sivyo yaonekanavyo.
Nina mifano ilyokuwa hai kwenye hili, shukrani kwa Mshanajr kwa ushauri yakinifu.
Mtu yeyote anayeamini amini sana Mungu na ushirikina, akiwa masikini siwezi kushangaa.

Mentality yake tu, epistemology yake tu, imejikita kwenye umasik8ni.
 
Pole sana. Kwanza fanya hivi kaa kimya kama nusu saa au lisa tafakari uweza wa Mungu, uzima ulio nao huna ulemavu, unapumua, una viungo vyote(Tabasamu). Mshukuru Mungu piga magoti hapo ulipo sali/swali hata kwa dakika 10 omba msahama kwa Mungu.

Baada ya hapo fikiria njia ya kutokea, tafuta kitu cha kufanya, kwanza fikiria biashara yeyote hata kama ni ndogo ila sio saaana mfano unaweza tafuta familia 3 mpaka 10 za kuwaletea fresh fruits , samaki fresh na vyakula vingine kila wiki au kwa muda fulani , unawapelekea vile vya high quality grade 1 unakwenda sokoni mwenyewe na baharini(unauzoefu kidogo) nunua vile vyakula vizuri sana kama mbogamboga fulani hivi ambazo mtaani hazipo sana , matunda kama zabibu, machungwa mazuri kama ya SA, Apple n.k ukiwa na familia 10 na ukaweza kuzihudumia vizuri kabisa unaweza pata njia ya kusonga. Hii biashara inaweza kuwa nzuri kwako kwa sababu kwanza hukai na bidhaa ndani usema ziharibika wewe unakusanya oda unaenda sokoni na baharini unaleta kwa mteja. Jenga uaminifu, jali muda na heshima kwa mteja.

Huu ni ushauri wangu tuu unaweza tizima biashara zaidi ya hii.

Zaidi: Mrudie Mungu fanya ibada vizuri kaa na familia yako karibu, mfarijianeni na mchape kazi saaaana usikeshe kwenye majumba ya ibada, vijiweni, kwa waganga ukidhani ndio utafanikiwa , sali/swali kwa muda wa ibada ,tumia muda vizuri sana pale penye nafasi piga kazi sana na usiangalie nyuma, shindana na nafsi na akili (zina tabia ya kubishana sana)

Achana na waganga na imani za kishirikina utahadhibiwa na Mungu na unaweza potea kwenye huu ulimwengu kirahisi sana.

Mwisho Mungu ni wetu sote, naomba akukumbuke na familia yako, naomba akupe wepesi na uvumilivu na msamaha.

Kila la kheri kaka.[emoji120]
 
Cjui umri wako. Cjui uzoefu wako kwenye game la biashara. Ila kwenye haya mambo unavyoyatazama sivyo yaonekanavyo.
Nina mifano ilyokuwa hai kwenye hili, shukrani kwa Mshanajr kwa ushauri yakinifu.
Unavyoyatazama haya mambo nalo ni tatizo.

Mshana Jr. naye ni mlozi tu aliyeshindwa hoja hapa.
 
Pole Sana mkuu.Hizo ni moja ya stage za maisha.Am sure ukija inuka Tena, hutoanguka Tena.Usisahau pia kumuomba Sana MUNGU akufungulie Milango iliyofungwa
 
Mtu yeyote anayeamini amini sana Mungu na ushirikina, akiwa masikini siwezi kushangaa.

Mentality yake tu, epistemology yake tu, imejikita kwenye umasik8ni.
Fafanua mkui Kiranga? Je unatakiwa kuamini nn ili ufanikiwe au usiwe masikini.
 
Cjui umri wako. Cjui uzoefu wako kwenye game la biashara. Ila kwenye haya mambo unavyoyatazama sivyo yaonekanavyo.
Nina mifano ilyokuwa hai kwenye hili, shukrani kwa Mshanajr kwa ushauri yakinifu.
Luis elezea basi na sisi tupate kujua what is inside ulimwengu wa fedha unamambo na sayansi zake nyingi sana
 
Kwanza nianze kwa kumshukuru muumba wa mbingu na nchi kwa kuzidi kutupa afya makini sote kwa mapenzi yake.

Naamini siku zote Mungu hatupi tunachotaka bali unachostahili nimekulia maisha ya kijijini yenye uchumi wa kati yaani Nusu shibe robo mlo mmoja kwa miaka mingi takribani 16ya kuzaliwa.

Nimepitia vingi japo nimeishi kidogo sana uhalisia wa shida na hustles za kibabe sijapita sana zile za kutisha ama kupambana Nusu roho kutaka tengana na mwili ni ups and Downs za kidunia Tu ndio nimepitia zaidi

Nisijielezee sana nachoomba apa zaidi ni Ushauri kwa sasa ndio naingia 30 kwenye maisha yangu sina mengi ya kujutia zaidi ya kushukuru kwa Neema chache nilizopatia na kulaumu ndugu kwa kutamani umasikini.uwe na mimi.

Baada ya shule niliendelea na hustles za mtaani mdogo mdogo hatimaye nikaanza kujikimu na vijisenti vidogo kusaidia ndugu wenye uhitaji Simu zilikua hazikauki nikaendelea kupambana miaka ikasogea nikawa dalali wa viwanja na mashamba namimi nikaweza bahatika kumiliki kiwanja mjini.

Mambo yakaendelea nikanunua kagari kadogo kakutembelea nikaona umri usinibane nikamwita mwenzangu kuishi pamoja nikafanya Mambo ya mahari na miamala mingine ya kiutamaduni basi siku zikasogea.

Mungu akajalia familia ikakua tukapata na mtoto wa kiume nikafungua na kaduka mke akawa anauza siku zikazidi kusonga.

MAMBO YANABADILIKA
Mishe za mtaani zikaanza kua ngumu gari ya kutembelea nikaifanya Tax dereva kawa kwikwi nikawa naendesha mwenyewe Mambo yakazidi kua tyiti tairi zinakwisha, service inahitajika na trafiki wananikamata daily utazania wanatumwa kwangu tu

Udalali ukawa mgumu na mambo yakawa mazito basi nikawaza kufanya biashara zingine angalau niokoe jahazi.

Nikauza gari baada ya kupata wazo la uvuvi nikatengeneza mitumbwi kwa kushirikiana na jamaa mwingine hapa tuliingia partnership ya biashara tugawane faida baada ya kurudisha mtaji.

PICHA INAANZA KUUNGUA.
Biashara ikawa haieleweki leo unapata faida ya laki ndani ya wiki unakuwa una hasara ya laki kadhaa imani ya kupata ikashamiri nikaanza kukopa naweka pesa kuongeza mtaji.

NAZIDI KUPOTEA
Nikaanza kukodisha mitumbwi ya mashine unalipia mashine na mtumbwi 400k kwa mwezi hapo unaweka mafuta, unanunua mitego ama ndoano + chambo kusudi kazi ianze kazi inakuwa kama ni kubahatisha leo faida laki tatu ukirudi siku ingine faida kidogo ama hasara laki 2.

MAMBO YANAHARIBIKA ZAIDI
Kazi za uvuvi zinahitaji ushirikina uliotukuka ni SIRI watabisha ila ndio Ukweli nikaanza kushiriki na kutoa pesa kwa wategaji waweke Mambo kwa bibi sawa. hapa Mambo yakawa yanaenda Nusu Nusu yaani ile Mungu saidia sina imani na kesho lakini unafanyaje ushaambiwa ndio lazima.ufanye kusudi ufanikiwe kama wenzio.

Bwana wewe Mambo yakazidia ugumu nikaanza kuhama mialo WAPI bila bila mikopo ikaongezeka nikashindwa kulipa mingine marafiki wakapotea kwa madeni na wengine baaada ya kubadili lifestyle kuhamia visiwani.

NASITISHA BIASHARA YA UVUVI.
nikaamua kuacha uvuvi na kupaki mitumbwi huku deni la niliofanya nae partnership bado anadai pesa yake nikimweleza hali halisi haelewi kabisa nyuma MARAFIKI nao wananidai na sioni dalili ya kuwalipa

NAAMUA KURUDI KUKAA NYUMBANI NA FAMILIA.
Hapa napata ugumu zaidi dukani kwa mwezi faida ni kama 150000 mpaka laki 2 na 30000 elfu, familia ndio tunategemea duka kwa.kila kitu kodi, chakula na mengineyo mtaji ukaanza kupungua mchana na usiku mwisho nashtuka naona pakushika tena panapotea na sijui nifanyeje?

WAY OUT.
Nimewahi kufanya utalii kwa kipindi fulani na kupata pesa nikiwa NYUMBANI nilikokulia nikiwaza KURUDI naanzaje KURUDI mtaani kwa wazazi sina connection na wadau wa hizo Mambo tena nimetoka huko mda naendaga tu kusalimia. NAANZAJE na utalii ni kazi ya msimu!

DUKA liko mbioni kufilisika kabisa mda sio mwingi tena naanzaje na kodi nayo ikiisha tena naendeleaje?

NIUZE KIWANJA?
Woga unaingia biashara mpya nitakayoanza ikibuma MWISHO utakuaje? Wife ndio atakimbia na mtoto arudi kwao! Ama atakimbia aniache na mtoto nimpeleke akakae na Babu na bibi? hapa sijui mbele itakuaje?

MARAFIKI NJE YA Tanzania!
Nilipokua nafanya utalii nilipata friends Korea, Japan na Australia ambao bado tunawasiliana naweza kwenda nchi zao nikapata hosting. Je nikifanikiwa kuuza kiwanja na kupata nauli nikaenda kutafuta maisha mbele itasaidia? Mke na mtoto nyuma Tz inakuaje ?
USHAURI wenu WAKUU,

Wanaonijua hawaamini kama kweli Mambo yote yamenipitia ndani ya mda mfupi hivi nimefikia hatua Hii sina uhakika na kesho wanahisi naigiza lakini ndio hivyo TATIZO bado niko very positive na sijaonyesha kukataa tamaa jumapili nilikutana na mtu . mwenye shida nikamsaidia Asee Wife alinishangaa sana na kuona nimepagawa baada ya kutoa kiasi cha pesa kwa muitaji wakati NYUMBANI hakuna pesa yeyote ya dharura wala msalia mtume.

maisha mtihani ila mimi ni kama napitia MAGAZIJUTO NIKISONGA MBELE NAKOSEA KIDOGO TU NARUDISHWA NYUMA KABISA.

USHAURI NA Uzoefu wenu ni muhimu sana pia msisahau na sala zenu kwani yeye muweza mwenye nguvu hajawahi shindwa na gumu lolote.MAWAZO mengi niliyonayo kama mbadala naona yananichanganya zaidi na siyaelewi kabisa kwani naona kama nikurudi Utoto
Kiauhalisia biashara nyingi si rahisi sana hasa mwanzoni,kikubwa unachotakiwa kukifahamu ni kwamba ni vyema wakati unaanzisha biashara uwe umejiandaa kisaikolojia wewe kama mjasiriamali maana biashara inapofeli ni kwamba wewe mmiliki binafsi ndo umefeli lakini si biashara imefeli,wakati unanzisha lazima ujiandae kuhustle kweli kweli hasa mwanzoni hivyo ukijiandaa kisaikolojia changamoto yeyote utakayokutana nayo unayojua ni part of the process hivyo ni kujichukualia somo kwenye kila changamoto unayokutana nayo,wajasiriamali wengi tuna kwama hapa,HATUJIANDAI KISAIKOLOJIA.
Kikubwa nachokiona ulichokosea mwanzoni na kazi yako ya Udalali ni KUKATA TAMAA,Usingetakiwa kukata tamaa maana ndiyo kazi yako iliyokupatia vyote ulivyokuwa navyo na hii inarudi pale pale kwamba hukujiandaa kisaikolojia kwamba sometimes mambo huwa yanakwenda na kuna muda yanakwama,nini tunachotakiwa kufanya pindi mambo yakiwa yanaenda vizuri na nini tunachotakiwa kufanya pindi mambo hayaendi vizuri.Ukiwa mtu wa kukata tamaa huwezi kutoboa na biashara yeyote,chagua kitu kimoja pambana nacho kufa na kupona hata miaka 10 iko siku itajipa tuu,,sio leo unahili unaona haliendi sawa kesho unalingine.Katika biashara kuna kipindi hufikia ambacho faida unayoitengeneza kwa mwezi mmoja ni faida uliyokuwa unatengeneza kwa mwaka mzima kwa miaka kazaa iliyopita.
 
Back
Top Bottom