Wakuu ushauri wenu ni muhimu, nimefilisika

Kuna baadhi ya maandiko humu ndani huwa hata kama nataka kufanya jambo la muhimu sana inanibidi nistop nijifunze dunia ilivyo,usikate tamaa pambana.
 
Pole sana chief lakini usikate tamaa kwani huo ni mzunguko tu wa gurudumu la maisha,leo uko juu na kesho uko chini. Nimepitia hayo unayopitia sasa kwani maisha yalinipiga mpaka nijarudi nyumbani kwa mzazi wangu nikiwa na mke pamoja na mtoto.

Nimefanya Kazi zote za halali kutafuta hela japo sikuwahi kuajiriwa,,nilijifunza kupika Chapati,maandazi, kutengeneza juice nk. Bahati mbaya hata hizo biashara nazo zikawa zinakufa,mara Chapati zimedoda,juice haiuzi mpaka ina chachuka nk.

Nikaanza kuingiwa na hofu huenda nimerogwa ndiyo maana mambo yangu hayaendi,maradhi nayo yakawa hayaishi kwa mke na mtoto kiasi kwamba hela ikiingia tu inatoka mpaka nikahisi UTI , typhoid na nduguze hujua nikipata pesa. Mwaka jana mwezi wa 4 nilikua na mtaji wa elf 50 ambao ulikua unanifanya niishi mjini.

Nimepelekwa mpaka kwa waganga wawili kucheck shida ilikua nini japo sina Imani nao, wote wakanipa story 1 tu kwamba nyota yangu imechafuliwa ndiyo maana biashara zangu haziendi. Muda mwingi nilikua najiuliza maswali magumu kwamba nimekwamia wapi? Nikagundua kuna makosa nilifanya kwenye biashara zangu kuu ndiyo yaliyo niangusha. Pia baishara zote zilizofuata zilikua za ku-kurupuka kuokoa jahazi lililotoboka lisizame.

Njia ya kutoka utakutana nayo tu,kama umewahi kuamka asubuhi huna hela mfukoni,vocha kwenye sim,mtoto analia njaa hakuna mkaa ndani bado usikate tamaa kwani kuna kesho iliyo bora. Kama una asset unazoweza kuuza na kupata hela ya kutosha make sure kwanza unajua utaenda kufanya nini.

Kama unaweza kuvuka border nahisi utakua uamuzi bora kabisa,Ila ukafanye mishe kwenye nchi zenye uchumi mkubwa kuliko za east Africa, South Africa,ulaya hutakosea. Niliuza baadhi ya assets zangu mwezi wa 6 mwaka jana nikaanza mishe za kuja South Africa na ninashukuru nimepata mabadiliko chanya makubwa sana tu. Nimekua nafanya cross border trade kwa miaka karibia 10 ,ilibidi nirudi tu kwa sababu ndiko nilikopatia hela mara ya kwanza.

Mungu akutie nguvu na familia yako usiione kama mzigo bali motivational factor ya wewe kutafuta maisha bora zaidi. Kila la heri.
 
Kwa utenzi nakupa heko.kuna mshairi anajinasibu nikki mbishi alinifanya niishi kisiwani songosongo miezi miwili bila sent zaidi ya kuskiliza albam yake named sauti yajogoo...sijaona mtu aliekushauri vyema zaidi ya kukutia majonzi na pole za kinafki..hapo usiuze kiwanja bali kubali kuishi daraja la chini na ufanye haso za kibabe na uso wa mbuzi fanya kazi za kujizalilisha beba hata taka ila usifeli
 
Kuna maana gani ya kukaa na mali wkt jahazi lina zama?
 
Kumiliki BMW mpaka bodaboda ni kweli? Au ndo ngano za kiswahili.
Watu mnadhani haya mambo ni story eh...mi niliwahi kuwa na ndinga 3 (prado,xtrail, na gx110) pamoja na gari ya kazini nissan hardbody yaani ilikua ukija kwangu unaweza changanyikiwa ukikuta zote nne zimepark mpaka mtaa mzima nilikua naonekana don....ila upepo ukacheza na sina ndinga hata moja saizi nakomaa kijasiliamali baada ya kutumika kwenye ajira na kupigwa kisulisuli...na sijawahi acha kumshukuru Mungu kwa niliyoyapitia na nilipo sasa.
 
Kweli kupanda na kushuka ndo huku ila ingekuwa vizuri ukatupa sababu zilizofanya ushuke maana siamini kama uliamka asubuhi ukajikuta una chochote ila na sisi tupate cha kujifunza.
 
Kweli kupanda na kushuka ndo huku ila ingekuwa vizuri ukatupa sababu zilizofanya ushuke maana siamini kama uliamka asubuhi ukajikuta una chochote ila na sisi tupate cha kujifunza.
Mi siwezi sema nimeshuka sababu ya kutokua na gari saizi ila mfumo wa maisha ndio umebadilika na utarudi sawa soon or later sababu moja ya vitu vilivyochangia upepo kubadilika ni kuchoshwa na kazi za watu na kuamua kukomaa kijasiliamali kufanya kazi zangu mwenyewe baada ya ajira kuisha kwa mapenzi ya maboss ambao nao ni waajiriwa wenzangu..hii hutokea kwa wengi tulio na hulka ya kijasiliamali sababu mafanikio kwenye ujasiliamali yanahitaji kujifunza sana kwa kukosea. Ila kwa anaeniona kwa jicho ambalo si la kijasiliamali ataona nimefeli.
 
ipyax, hili vaga la xenophonia halija kuathiri? mana maduka na offis nyingi za wagen zilopigwa moto
 
Aisee
 
Hakuna mpango wowote wa kesho?
 
Mimi siyo mshauri, Mwisho kauliza akiuza alivyo navyo akimbie huko Korea au Japan, mke na watoto itakuwaje?
Lakini nimepitia message zote sioni mtu kamshauri afanye nini. Pole sio ushauri, na haisaidii hata ukisema au usiposema. Yeye nadhani anahitaji kufahamu zaidi akimuacha mkewe na watoto ni sawa au siyo sawa, nionavyo keshaamua kusonga huko mbele.

Washauri toeni ushauri, nasi tujifunze kupitia kwenu.
 
Uza kiwanja ukajaribu maisha huko ughaibuni, najua utafanikisha tu. Mke na mtoto, wape kitakacho salia, ukifika huko ukumbuke kuwa hudumia.
 
Bela, ng'ope ndimuya mlioni 1 su munuve.. Nyongise.
 
Thank you chief kwa ushuhuda kufilisika kuishiwa na kufulia sikia tu kwa wengine omba mungu yasikukute
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…