Unaweza ukapata hata ajali na TZ 11 ikatoka piaInawezekana mkuu tena unaweza usimiliki hata iyo bodaboda ukabakia na TZ 11
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaweza ukapata hata ajali na TZ 11 ikatoka piaInawezekana mkuu tena unaweza usimiliki hata iyo bodaboda ukabakia na TZ 11
Kuna maana gani ya kukaa na mali wkt jahazi lina zama?Kwa utenzi nakupa heko.kuna mshairi anajinasibu nikki mbishi alinifanya niishi kisiwani songosongo miezi miwili bila sent zaidi ya kuskiliza albam yake named sauti yajogoo...sijaona mtu aliekushauri vyema zaidi ya kukutia majonzi na pole za kinafki..hapo usiuze kiwanja bali kubali kuishi daraja la chini na ufanye haso za kibabe na uso wa mbuzi fanya kazi za kujizalilisha beba hata taka ila usifeli
Watu mnadhani haya mambo ni story eh...mi niliwahi kuwa na ndinga 3 (prado,xtrail, na gx110) pamoja na gari ya kazini nissan hardbody yaani ilikua ukija kwangu unaweza changanyikiwa ukikuta zote nne zimepark mpaka mtaa mzima nilikua naonekana don....ila upepo ukacheza na sina ndinga hata moja saizi nakomaa kijasiliamali baada ya kutumika kwenye ajira na kupigwa kisulisuli...na sijawahi acha kumshukuru Mungu kwa niliyoyapitia na nilipo sasa.Kumiliki BMW mpaka bodaboda ni kweli? Au ndo ngano za kiswahili.
Kweli kupanda na kushuka ndo huku ila ingekuwa vizuri ukatupa sababu zilizofanya ushuke maana siamini kama uliamka asubuhi ukajikuta una chochote ila na sisi tupate cha kujifunza.Watu mnadhani haya mambo ni story eh...mi niliwahi kuwa na ndinga 3 (prado,xtrail, na gx110) pamoja na gari ya kazini nissan hardbody yaani ilikua ukija kwangu unaweza changanyikiwa ukikuta zote nne zimepark mpaka mtaa mzima nilikua naonekana don....ila upepo ukacheza na sina ndinga hata moja saizi nakomaa kijasiliamali baada ya kutumika kwenye ajira na kupigwa kisulisuli...na sijawahi acha kumshukuru Mungu kwa niliyoyapitia na nilipo sasa.
Mi siwezi sema nimeshuka sababu ya kutokua na gari saizi ila mfumo wa maisha ndio umebadilika na utarudi sawa soon or later sababu moja ya vitu vilivyochangia upepo kubadilika ni kuchoshwa na kazi za watu na kuamua kukomaa kijasiliamali kufanya kazi zangu mwenyewe baada ya ajira kuisha kwa mapenzi ya maboss ambao nao ni waajiriwa wenzangu..hii hutokea kwa wengi tulio na hulka ya kijasiliamali sababu mafanikio kwenye ujasiliamali yanahitaji kujifunza sana kwa kukosea. Ila kwa anaeniona kwa jicho ambalo si la kijasiliamali ataona nimefeli.Kweli kupanda na kushuka ndo huku ila ingekuwa vizuri ukatupa sababu zilizofanya ushuke maana siamini kama uliamka asubuhi ukajikuta una chochote ila na sisi tupate cha kujifunza.
Mi siwezi sema nimeshuka sababu ya kutokua na gari saizi ila mfumo wa maisha ndio umebadilika na utarudi sawa soon or later sababu moja ya vitu vilivyochangia upepo kubadilika ni kuchoshwa na kazi za watu na kuamua kukomaa kijasiliamali kufanya kazi zangu mwenyewe baada ya ajira kuisha kwa mapenzi ya maboss ambao nao ni waajiriwa wenzangu..hii hutokea kwa wengi tulio na hulka ya kijasiliamali sababu mafanikio kwenye ujasiliamali yanahitaji kujifunza sana kwa kukosea. Ila kwa anaeniona kwa jicho ambalo si la kijasiliamali ataona nimefeli.Kweli kupanda na kushuka ndo huku ila ingekuwa vizuri ukatupa sababu zilizofanya ushuke maana siamini kama uliamka asubuhi ukajikuta una chochote ila na sisi tupate cha kujifunza.
AiseeKwanza pole ndugu yangu, pili hayo unayoyapitia nami yananikuta vivyo hivyo toka kumiliki gari hadi kumiliki sendos 2.
Kwanza nakushauri ni kaa chini na shem (hawa ndiyo wa kwanza kujenga / kuharibu) mpe ukweli mshauriane muanze upyaaaaaaaaa. Hapa utapata pa kuanzia.
Usiuze kiwanja bro kamwe ni heri ugange njaa ipo siku yatarudi tu.
Anza mitikas km unaanza upya kabisa,yaani vuruga kila kitu (hapa madeni kuwa km hauna hali ngumu kila mtu anajua) hawa wa maden usihangaike nao labda yale ya assets.
Komaa na bihashara na lengo moja hakika utasimama tena.
Usisahau kumuomba sana Mungu bro.
Pia jipe Moyo Hauko Pekee Ako unaepita hali hiyo.
Watu tumemiliki bmw x3 leo hii dereva boda boda nayo naunga unga.
Hakuna mpango wowote wa kesho?Dah, ndugu yangu pole sana, mbona wewe una ahueni kwenye hiyo biashara ya uvuvi? Mimi nilishafanya hiyo biashara ya kukodi mitumbwi huko swea nikapoteza pesa nyingi sana
Nimekuja kufilisika kabisa kabisa kwenye operation sangara kipindi kile mpina anasimamisha magari ya samaki na kupima undersized, nilikua naingiza sio chini ya laki 5 faida kwa week, saivi nipo nyumbani kwa wazazi hata Mia sina vibarua navyo Tatizo, nahangaika tu ajira hamna pamoja na kua fluent kwenye English na computer applications lakini hata ajira ya kukata majani haipo.
Mimi na wewe tupo kama rika, umenipita miaka miwili tu, Mungu atisaidie kwa kweli.
Bela, ng'ope ndimuya mlioni 1 su munuve.. Nyongise.Haupo peke yako mkuu mimi nimekuja hadi kuomba msaada wa laptop humu wakati zamani nilikua na uwezo wa kununua hata laptop 10 kwa mara moja,kuhusu gari hapo ndii usiseme...kubali matokeo kwani hapo sio kituo hilo ni tukio tu.
Kwenye universal laws naona kosa jingine umelifanya siku ya jumapili umevunja sheria inautwa THE LAW OF CORRESPONDANCE (sheria ya usawa& ulinganifu). Amini Dunia yetu ya nnje ni matokeo ya Dunia yetu ya ndani.kitu kikubwa kinaundwa na vitu vidogo vidogo.
Show gratitude for what you have,shukuru kwa kile ulicho nacho kwani usiposhukuru ulimwengu utakunyang'anya usicho kithamini..Jumapili umeshindwa kukithamini kile kidogo ulicho nacho ukaamua kukitoa chote manaake hujaweka usawa..hakikisha unavyosaidia kuna kitu kitu unabaki nacho.
Mimi nilipoteza marafiki,mpenzi,majirani mpaka baadhi ya ndugu nilikata tamaa nikatamani kujiua si unajua sisi wahehe tena,badae nilivyogundua sina nilichopungukiwa mwilini nipo safi nikajiona fala nikawa tayari kufanya kazi yoyote bila kijari elimu wala nafasi nillikuwa nayo hapo nyuma..Mungu si athumani bado yupo pamoja nami.
a moja,gari ya kutembelea,navyosema gari sio vits,paso,duet,starlet..hakuna maisha matamu kama opportunity inakuja kukiwa na preparation.
Nikukumbushe tu kwamba hakuna ulichopoteza ila umejifunza
Thank you chief kwa ushuhuda kufilisika kuishiwa na kufulia sikia tu kwa wengine omba mungu yasikukutePole sana chief lakini usikate tamaa kwani huo ni mzunguko tu wa gurudumu la maisha,leo uko juu na kesho uko chini. Nimepitia hayo unayopitia sasa kwani maisha yalinipiga mpaka nijarudi nyumbani kwa mzazi wangu nikiwa na mke pamoja na mtoto.
Nimefanya Kazi zote za halali kutafuta hela japo sikuwahi kuajiriwa,,nilijifunza kupika Chapati,maandazi, kutengeneza juice nk. Bahati mbaya hata hizo biashara nazo zikawa zinakufa,mara Chapati zimedoda,juice haiuzi mpaka ina chachuka nk.
Nikaanza kuingiwa na hofu huenda nimerogwa ndiyo maana mambo yangu hayaendi,maradhi nayo yakawa hayaishi kwa mke na mtoto kiasi kwamba hela ikiingia tu inatoka mpaka nikahisi UTI , typhoid na nduguze hujua nikipata pesa. Mwaka jana mwezi wa 4 nilikua na mtaji wa elf 50 ambao ulikua unanifanya niishi mjini.
Nimepelekwa mpaka kwa waganga wawili kucheck shida ilikua nini japo sina Imani nao, wote wakanipa story 1 tu kwamba nyota yangu imechafuliwa ndiyo maana biashara zangu haziendi. Muda mwingi nilikua najiuliza maswali magumu kwamba nimekwamia wapi? Nikagundua kuna makosa nilifanya kwenye biashara zangu kuu ndiyo yaliyo niangusha. Pia baishara zote zilizofuata zilikua za ku-kurupuka kuokoa jahazi lililotoboka lisizame.
Njia ya kutoka utakutana nayo tu,kama umewahi kuamka asubuhi huna hela mfukoni,vocha kwenye sim,mtoto analia njaa hakuna mkaa ndani bado usikate tamaa kwani kuna kesho iliyo bora. Kama una asset unazoweza kuuza na kupata hela ya kutosha make sure kwanza unajua utaenda kufanya nini.
Kama unaweza kuvuka border nahisi utakua uamuzi bora kabisa,Ila ukafanye mishe kwenye nchi zenye uchumi mkubwa kuliko za east Africa, South Africa,ulaya hutakosea. Niliuza baadhi ya assets zangu mwezi wa 6 mwaka jana nikaanza mishe za kuja South Africa na ninashukuru nimepata mabadiliko chanya makubwa sana tu. Nimekua nafanya cross border trade kwa miaka karibia 10 ,ilibidi nirudi tu kwa sababu ndiko nilikopatia hela mara ya kwanza.
Mungu akutie nguvu na familia yako usiione kama mzigo bali motivational factor ya wewe kutafuta maisha bora zaidi. Kila la heri.