mng'ato
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 29,200
- 49,076
Kufa kufaana mkuu,hahah.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Dah! Maisha haya
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kufa kufaana mkuu,hahah.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Dah! Maisha haya
Kwanza pole ndugu yangu, pili hayo unayoyapitia nami yananikuta vivyo hivyo toka kumiliki gari hadi kumiliki sendos 2.
Kwanza nakushauri ni kaa chini na shem (hawa ndiyo wa kwanza kujenga / kuharibu) mpe ukweli mshauriane muanze upyaaaaaaaaa. Hapa utapata pa kuanzia.
Usiuze kiwanja bro kamwe ni heri ugange njaa ipo siku yatarudi tu.
Anza mitikas km unaanza upya kabisa,yaani vuruga kila kitu (hapa madeni kuwa km hauna hali ngumu kila mtu anajua) hawa wa maden usihangaike nao labda yale ya assets.
Komaa na bihashara na lengo moja hakika utasimama tena.
Usisahau kumuomba sana Mungu bro.
Pia jipe Moyo Hauko Pekee Ako unaepita hali hiyo.
Watu tumemiliki bmw x3 leo hii dereva boda boda nayo naunga unga.
Kule Swea kuna rafiki yangu akinishawishi sana khs hio bizness yeye anaishi huko Luchelele ila nilijivuta vuta sana ku-fanya p/ship nae,hayo mambo ya Mpina ndio yalivuruga kila kitu,mshkaji ilibidi aliende visiwani huko kuendeleza mishe hizo ila naona bado mambo yake hayako njema.Dah, ndugu yangu pole sana, mbona wewe una ahueni kwenye hiyo biashara ya uvuvi? Mimi nilishafanya hiyo biashara ya kukodi mitumbwi huko swea nikapoteza pesa nyingi sana
Nimekuja kufilisika kabisa kabisa kwenye operation sangara kipindi kile mpina anasimamisha magari ya samaki na kupima undersized, nilikua naingiza sio chini ya laki 5 faida kwa week, saivi nipo nyumbani hata Mia sina vibarua navyo Tatizo, nahangaika tu ajira hamna pamoja na kua fluent kwenye English na computer applications lakini hata ajira ya kukata majani haipo.
Mimi na wewe tupo kama rika, umenipita miaka miwili tu, Mungu atisaidie kwa kweli.
Hapana mkuu, mimi vingi vimeniangusha, hila afya ndiyo ilianza kunifilisi
Wao wenyewe wana hali ngumu balaa mkuu,wabongo hawanaga tamaduni za kwenda kuomba msaada wa matatizo ya kisaikolojia,utashangaa tu amekua chizi ghafla hapo ndo unaelewa hali tete.Mkuu hao wanasaikolojia hawahitaji wapiga deki kwenye ofisi zao unistue?
Dah! Kumbe na penyewe unapajua? Utakua ulisoma SAUT, huko kumenitafunia pesa hatari, nilienda mpaka visiwani sengerema kule kupiga hizo mishe, nimekaa sana pale mwaloni kirumba nilikua nasafirisha dagaa mpaka Iringa Dodoma ila hii paranja ya mpina ndio imenifilisi kabisa sababu unakamatwa mzigo wa million 3 leo, kesho million 2 hivyo hivyo mpaka unabaki emptyKule Swea kuna rafiki yangu akinishawishi sana khs hio bizness yeye anaishi huko Luchelele ila nilijivuta vuta sana ku-fanya p/ship nae,hayo mambo ya Mpina ndio yalivuruga kila kitu,mshkaji ilibidi aliende visiwani huko kuendeleza mishe hizo ila naona bado mambo yake hayako njema.
Dah! Kumbe na penyewe unapajua? Utakua ulisoma SAUT, huko kumenitafunia pesa hatari, nilienda mpaka visiwani sengerema kule kupiga hizo mishe, nimekaa sana pale mwaloni kirumba nilikua nasafirisha dagaa mpaka Iringa Dodoma ila hii paranja ya mpina ndio imenifilisi kabisa sababu unakamatwa mzigo wa million 3 leo, kesho million 2 hivyo hivyo mpaka unabaki empty
Wengi wamefilisika, wengine wamepoteza maisha, wengine wanasota magerezani, yaani watu kama wakina njiwa pori na wenyewe waleguswa.
Acha ku-bet mzee baba.
Safi sana mkuu,hongera.Nimeacha boss nnamwaka wapil sasa
Muhimu ni kununua nini Mkuu?...mkuu ukiinuka tena vizur epuka sana kununua vtu vya luxury kama gari hali ya kuwa upo ktk hali ya kati kiuchumi,huwa vinaonekana kama asset but ni liability ambayo inakutafuna polepole...naamini moja ya chanzo chko cha kufrisika ni hlo gar lako.
Kama haya uliyoandika ni kweli basis unatakiwa kuokoka, MPE YESU MAISHA YAKO NAYE ATAKUSAIDIA.Kwanza nianze kwa kumshukuru muumba wa mbingu na nchi kwa kuzidi kutupa afya makini sote kwa mapenzi yake.
Naamini siku zote Mungu hatupi tunachotaka bali unachostahili nimekulia maisha ya kijijini yenye uchumi wa kati yaani Nusu shibe robo mlo mmoja kwa miaka mingi takribani 16ya kuzaliwa.
Nimepitia vingi japo nimeishi kidogo sana uhalisia wa shida na hustles za kibabe sijapita sana zile za kutisha ama kupambana Nusu roho kutaka tengana na mwili ni ups and Downs za kidunia Tu ndio nimepitia zaidi
Nisijielezee sana nachoomba apa zaidi ni Ushauri kwa sasa ndio naingia 30 kwenye maisha yangu sina mengi ya kujutia zaidi ya kushukuru kwa Neema chache nilizopatia na kulaumu ndugu kwa kutamani umasikini.uwe na mimi.
Baada ya shule niliendelea na hustles za mtaani mdogo mdogo hatimaye nikaanza kujikimu na vijisenti vidogo kusaidia ndugu wenye uhitaji Simu zilikua hazikauki nikaendelea kupambana miaka ikasogea nikawa dalali wa viwanja na mashamba namimi nikaweza bahatika kumiliki kiwanja mjini.
Mambo yakaendelea nikanunua kagari kadogo kakutembelea nikaona umri usinibane nikamwita mwenzangu kuishi pamoja nikafanya Mambo ya mahari na miamala mingine ya kiutamaduni basi siku zikasogea.
Mungu akajalia familia ikakua tukapata na mtoto wa kiume nikafungua na kaduka mke akawa anauza siku zikazidi kusonga.
MAMBO YANABADILIKA
Mishe za mtaani zikaanza kua ngumu gari ya kutembelea nikaifanya Tax dereva kawa kwikwi nikawa naendesha mwenyewe Mambo yakazidi kua tyiti tairi zinakwisha, service inahitajika na trafiki wananikamata daily utazania wanatumwa kwangu tu
Udalali ukawa mgumu na mambo yakawa mazito basi nikawaza kufanya biashara zingine angalau niokoe jahazi.
Nikauza gari baada ya kupata wazo la uvuvi nikatengeneza mitumbwi kwa kushirikiana na jamaa mwingine hapa tuliingia partnership ya biashara tugawane faida baada ya kurudisha mtaji.
PICHA INAANZA KUUNGUA.
Biashara ikawa haieleweki leo unapata faida ya laki ndani ya wiki unakuwa una hasara ya laki kadhaa imani ya kupata ikashamiri nikaanza kukopa naweka pesa kuongeza mtaji.
NAZIDI KUPOTEA
Nikaanza kukodisha mitumbwi ya mashine unalipia mashine na mtumbwi 400k kwa mwezi hapo unaweka mafuta, unanunua mitego ama ndoano + chambo kusudi kazi ianze kazi inakuwa kama ni kubahatisha leo faida laki tatu ukirudi siku ingine faida kidogo ama hasara laki 2.
MAMBO YANAHARIBIKA ZAIDI
Kazi za uvuvi zinahitaji ushirikina uliotukuka ni SIRI watabisha ila ndio Ukweli nikaanza kushiriki na kutoa pesa kwa wategaji waweke Mambo kwa bibi sawa. hapa Mambo yakawa yanaenda Nusu Nusu yaani ile Mungu saidia sina imani na kesho lakini unafanyaje ushaambiwa ndio lazima.ufanye kusudi ufanikiwe kama wenzio.
Bwana wewe Mambo yakazidia ugumu nikaanza kuhama mialo WAPI bila bila mikopo ikaongezeka nikashindwa kulipa mingine marafiki wakapotea kwa madeni na wengine baaada ya kubadili lifestyle kuhamia visiwani.
NASITISHA BIASHARA YA UVUVI.
nikaamua kuacha uvuvi na kupaki mitumbwi huku deni la niliofanya nae partnership bado anadai pesa yake nikimweleza hali halisi haelewi kabisa nyuma MARAFIKI nao wananidai na sioni dalili ya kuwalipa
NAAMUA KURUDI KUKAA NYUMBANI NA FAMILIA.
Hapa napata ugumu zaidi dukani kwa mwezi faida ni kama 150000 mpaka laki 2 na 30000 elfu, familia ndio tunategemea duka kwa.kila kitu kodi, chakula na mengineyo mtaji ukaanza kupungua mchana na usiku mwisho nashtuka naona pakushika tena panapotea na sijui nifanyeje?
WAY OUT.
Nimewahi kufanya utalii kwa kipindi fulani na kupata pesa nikiwa NYUMBANI nilikokulia nikiwaza KURUDI naanzaje KURUDI mtaani kwa wazazi sina connection na wadau wa hizo Mambo tena nimetoka huko mda naendaga tu kusalimia. NAANZAJE na utalii ni kazi ya msimu!
DUKA liko mbioni kufilisika kabisa mda sio mwingi tena naanzaje na kodi nayo ikiisha tena naendeleaje?
NIUZE KIWANJA?
Woga unaingia biashara mpya nitakayoanza ikibuma MWISHO utakuaje? Wife ndio atakimbia na mtoto arudi kwao! Ama atakimbia aniache na mtoto nimpeleke akakae na Babu na bibi? hapa sijui mbele itakuaje?
MARAFIKI NJE YA Tanzania!
Nilipokua nafanya utalii nilipata friends Korea, Japan na Australia ambao bado tunawasiliana naweza kwenda nchi zao nikapata hosting. Je nikifanikiwa kuuza kiwanja na kupata nauli nikaenda kutafuta maisha mbele itasaidia? Mke na mtoto nyuma Tz inakuaje ?
USHAURI wenu WAKUU,
Wanaonijua hawaamini kama kweli Mambo yote yamenipitia ndani ya mda mfupi hivi nimefikia hatua Hii sina uhakika na kesho wanahisi naigiza lakini ndio hivyo TATIZO bado niko very positive na sijaonyesha kukataa tamaa jumapili nilikutana na mtu . mwenye shida nikamsaidia Asee Wife alinishangaa sana na kuona nimepagawa baada ya kutoa kiasi cha pesa kwa muitaji wakati NYUMBANI hakuna pesa yeyote ya dharura wala msalia mtume.
maisha mtihani ila mimi ni kama napitia MAGAZIJUTO NIKISONGA MBELE NAKOSEA KIDOGO TU NARUDISHWA NYUMA KABISA.
USHAURI NA Uzoefu wenu ni muhimu sana pia msisahau na sala zenu kwani yeye muweza mwenye nguvu hajawahi shindwa na gumu lolote.MAWAZO mengi niliyonayo kama mbadala naona yananichanganya zaidi na siyaelewi kabisa kwani naona kama nikurudi Utoto
Kwanza pole ndugu yangu, pili hayo unayoyapitia nami yananikuta vivyo hivyo toka kumiliki gari hadi kumiliki sendos 2.
Kwanza nakushauri ni kaa chini na shem (hawa ndiyo wa kwanza kujenga / kuharibu) mpe ukweli mshauriane muanze upyaaaaaaaaa. Hapa utapata pa kuanzia.
Usiuze kiwanja bro kamwe ni heri ugange njaa ipo siku yatarudi tu.
Anza mitikas km unaanza upya kabisa,yaani vuruga kila kitu (hapa madeni kuwa km hauna hali ngumu kila mtu anajua) hawa wa maden usihangaike nao labda yale ya assets.
Komaa na bihashara na lengo moja hakika utasimama tena.
Usisahau kumuomba sana Mungu bro.
Pia jipe Moyo Hauko Pekee Ako unaepita hali hiyo.
Watu tumemiliki bmw x3 leo hii dereva boda boda nayo naunga unga.
Muhimu ni kununua nini Mkuu?
Kumiliki BMW mpaka bodaboda ni kweli? Au ndo ngano za kiswahili.
Huyu bwege ngoja tumuite afanye mambo kidogo kwa ndugu yetu Kiduku Lilo muone basi mshikaji kupitia namba ya M-PESA