Wakuu ushauri wenu ni muhimu, nimefilisika

Wakuu ushauri wenu ni muhimu, nimefilisika

Ushauri wangu.
Kwanza sikupi pole kabisa

nachoweza kukushauri kwanza uza kiwanja then wekeza zaidi kwenye duka na jipambanue kwenye biashara ya duka zaidi na uzidi kujipa muda kwa pesa itakoyobakia kwa baada ya kuuza kiwanja then najua tu utapata wazo bora zaidi.

Usipanic jitahidi kutulia sana ikiwezekana lala mno kwa muda mrefu.

Mostly maisha ni kupambna sana bro.

Am not fit enough katika maisha lakini napenda kujipa muda kwa kila jambo .

Nakumbuka: niliwahi pita kipindi kigumu sana .
Unajua nilichokuwa nafanya.... nilikuwa mtu wa kulala sana na nikiamka Nawaza sana mostly nilikuwa najipa muda katika kila jambo.

Mpaka sasa natambua nikiwa na wakati mgumu tu lazima utaniona mtulivu sana na sinaga papara kwenye maamuzi I mean naweza chukua up a year mpaka kufikia maamuzi na nipo na malengo ya Hadi ten years .

Shemeji yenu hatambui Kama 2030 lazima nimpeleke Dubai kutembea lakini lipo kwenye mpango.

All in all nasubiri Mungu Apitishe niliwazalo na nayoyawaza.
 
Haya maisha asee Mungu asaidie, hii hali naipitia sasa hivi wakati mwaka uliopita nilikua na 7m sio nyingi ila kwangu ni nyingi, sasa hivi hata hela ya kuangalia game ya yanga kwenye kibanda umiza sina.
 
Haya maisha asee Mungu asaidie, hii hali naipitia sasa hivi wakati mwaka uliopita nilikua na 7m sio nyingi ila kwangu ni nyingi, sasa hivi hata hela ya kuangalia game ya yanga kwenye kibanda umiza sina.
Utasimama Tena, kupanda na kushuka ni kawaida kwenye maisha
 
Kwanza pole ndugu yangu, pili hayo unayoyapitia nami yananikuta vivyo hivyo toka kumiliki gari hadi kumiliki sendos 2.

Kwanza nakushauri ni kaa chini na shem (hawa ndiyo wa kwanza kujenga / kuharibu) mpe ukweli mshauriane muanze upyaaaaaaaaa. Hapa utapata pa kuanzia.
Usiuze kiwanja bro kamwe ni heri ugange njaa ipo siku yatarudi tu.
Anza mitikas km unaanza upya kabisa,yaani vuruga kila kitu (hapa madeni kuwa km hauna hali ngumu kila mtu anajua) hawa wa maden usihangaike nao labda yale ya assets.
Komaa na bihashara na lengo moja hakika utasimama tena.
Usisahau kumuomba sana Mungu bro.
Pia jipe Moyo Hauko Pekee Ako unaepita hali hiyo.

Watu tumemiliki bmw x3 leo hii dereva boda boda nayo naunga unga.
Ilikuaje mkuu tupe mkasa
 
Kwanza nianze kwa kumshukuru Muumba wa Mbingu na Nchi kwa kuzidi kutupa afya makini sote kwa mapenzi yake.

Naamini siku zote Mungu hatupi tunachotaka bali unachostahili nimekulia maisha ya kijijini yenye uchumi wa kati yaani Nusu shibe robo mlo mmoja kwa miaka mingi takribani 16ya kuzaliwa.

Nimepitia vingi japo nimeishi kidogo sana uhalisia wa shida na hustles za kibabe sijapita sana zile za kutisha ama kupambana Nusu roho kutaka tengana na mwili ni ups and Downs za kidunia Tu ndio nimepitia zaidi

Nisijielezee sana nachoomba apa zaidi ni Ushauri kwa sasa ndio naingia 30 kwenye maisha yangu sina mengi ya kujutia zaidi ya kushukuru kwa Neema chache nilizopatia na kulaumu ndugu kwa kutamani umasikini.uwe na mimi.

Baada ya shule niliendelea na hustles za mtaani mdogo mdogo hatimaye nikaanza kujikimu na vijisenti vidogo kusaidia ndugu wenye uhitaji Simu zilikua hazikauki nikaendelea kupambana miaka ikasogea nikawa dalali wa viwanja na mashamba namimi nikaweza bahatika kumiliki kiwanja mjini.

Mambo yakaendelea nikanunua kagari kadogo kakutembelea nikaona umri usinibane nikamwita mwenzangu kuishi pamoja nikafanya Mambo ya mahari na miamala mingine ya kiutamaduni basi siku zikasogea.

Mungu akajalia familia ikakua tukapata na mtoto wa kiume nikafungua na kaduka mke akawa anauza siku zikazidi kusonga.

MAMBO YANABADILIKA
Mishe za mtaani zikaanza kua ngumu gari ya kutembelea nikaifanya Tax dereva kawa kwikwi nikawa naendesha mwenyewe Mambo yakazidi kua tyiti tairi zinakwisha, service inahitajika na trafiki wananikamata daily utazania wanatumwa kwangu tu

Udalali ukawa mgumu na mambo yakawa mazito basi nikawaza kufanya biashara zingine angalau niokoe jahazi.

Nikauza gari baada ya kupata wazo la uvuvi nikatengeneza mitumbwi kwa kushirikiana na jamaa mwingine hapa tuliingia partnership ya biashara tugawane faida baada ya kurudisha mtaji.

PICHA INAANZA KUUNGUA.
Biashara ikawa haieleweki leo unapata faida ya laki ndani ya wiki unakuwa una hasara ya laki kadhaa imani ya kupata ikashamiri nikaanza kukopa naweka pesa kuongeza mtaji.

NAZIDI KUPOTEA
Nikaanza kukodisha mitumbwi ya mashine unalipia mashine na mtumbwi 400k kwa mwezi hapo unaweka mafuta, unanunua mitego ama ndoano + chambo kusudi kazi ianze kazi inakuwa kama ni kubahatisha leo faida laki tatu ukirudi siku ingine faida kidogo ama hasara laki 2.

MAMBO YANAHARIBIKA ZAIDI
Kazi za uvuvi zinahitaji ushirikina uliotukuka ni SIRI watabisha ila ndio Ukweli nikaanza kushiriki na kutoa pesa kwa wategaji waweke Mambo kwa bibi sawa. hapa Mambo yakawa yanaenda Nusu Nusu yaani ile Mungu saidia sina imani na kesho lakini unafanyaje ushaambiwa ndio lazima.ufanye kusudi ufanikiwe kama wenzio.

Bwana wewe Mambo yakazidia ugumu nikaanza kuhama mialo WAPI bila bila mikopo ikaongezeka nikashindwa kulipa mingine marafiki wakapotea kwa madeni na wengine baaada ya kubadili lifestyle kuhamia visiwani.

NASITISHA BIASHARA YA UVUVI.
nikaamua kuacha uvuvi na kupaki mitumbwi huku deni la niliofanya nae partnership bado anadai pesa yake nikimweleza hali halisi haelewi kabisa nyuma MARAFIKI nao wananidai na sioni dalili ya kuwalipa

NAAMUA KURUDI KUKAA NYUMBANI NA FAMILIA.
Hapa napata ugumu zaidi dukani kwa mwezi faida ni kama 150000 mpaka laki 2 na 30000 elfu, familia ndio tunategemea duka kwa.kila kitu kodi, chakula na mengineyo mtaji ukaanza kupungua mchana na usiku mwisho nashtuka naona pakushika tena panapotea na sijui nifanyeje?

WAY OUT.
Nimewahi kufanya utalii kwa kipindi fulani na kupata pesa nikiwa NYUMBANI nilikokulia nikiwaza KURUDI naanzaje KURUDI mtaani kwa wazazi sina connection na wadau wa hizo Mambo tena nimetoka huko mda naendaga tu kusalimia. NAANZAJE na utalii ni kazi ya msimu!

DUKA liko mbioni kufilisika kabisa mda sio mwingi tena naanzaje na kodi nayo ikiisha tena naendeleaje?

NIUZE KIWANJA?
Woga unaingia biashara mpya nitakayoanza ikibuma MWISHO utakuaje? Wife ndio atakimbia na mtoto arudi kwao! Ama atakimbia aniache na mtoto nimpeleke akakae na Babu na bibi? hapa sijui mbele itakuaje?

MARAFIKI NJE YA Tanzania!
Nilipokua nafanya utalii nilipata friends Korea, Japan na Australia ambao bado tunawasiliana naweza kwenda nchi zao nikapata hosting. Je nikifanikiwa kuuza kiwanja na kupata nauli nikaenda kutafuta maisha mbele itasaidia? Mke na mtoto nyuma Tz inakuaje ?
USHAURI wenu WAKUU,

Wanaonijua hawaamini kama kweli Mambo yote yamenipitia ndani ya mda mfupi hivi nimefikia hatua Hii sina uhakika na kesho wanahisi naigiza lakini ndio hivyo TATIZO bado niko very positive na sijaonyesha kukataa tamaa jumapili nilikutana na mtu . mwenye shida nikamsaidia Asee Wife alinishangaa sana na kuona nimepagawa baada ya kutoa kiasi cha pesa kwa muitaji wakati NYUMBANI hakuna pesa yeyote ya dharura wala msalia mtume.

maisha mtihani ila mimi ni kama napitia MAGAZIJUTO NIKISONGA MBELE NAKOSEA KIDOGO TU NARUDISHWA NYUMA KABISA.

USHAURI NA Uzoefu wenu ni muhimu sana pia msisahau na sala zenu kwani yeye muweza mwenye nguvu hajawahi shindwa na gumu lolote.MAWAZO mengi niliyonayo kama mbadala naona yananichanganya zaidi na siyaelewi kabisa kwani naona kama nikurudi Utoto
Kwa nilivyosoma na kuelewa .
Biashara uliyoanza nayo HAIKUWA na Misingi na Mizizi .
Niamini nikisema HAIKUWA na hivyo vitu .

Kwa ushauri wangu .
Anza Biashara moja upya na isimamie kisawasawa.
Wanawake wengi/wake zetu si wa kuwaachia biashara na wewe kupambana na Biashara nyingine.

Jipe muda wa Kuanza Biashara upya .
Nature ya maisha nayoijua ni ukipanic unaanza kurukaruka
Leo utafanya Biashara hii na kesho nyingine lakini zote hazina Misingi na Mizizi.

Be positive sana.

Pia<>
Mshirikishe mwenza wako hali halisi na kama ni mvumilivu mtaanza upya.


Usipende sana kuangalia hali halisi ya sasa.
Jifunze kuacha nature iendelee na hali itabadilika Taratibu.
 
Back
Top Bottom