Uchaguzi 2020 Wakuu wa Mikoa majembe na vimeo kuelekea uchaguzi mkuu

Uchaguzi 2020 Wakuu wa Mikoa majembe na vimeo kuelekea uchaguzi mkuu

Pilitoni

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2011
Posts
1,197
Reaction score
507
Wakuu wa mikoa ya Tanzania Bara huteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa sasa ni jemedari shupavu Dr. John Pombe Joseph Magufuli na kwa upande wa Zanzibar Rais wa Zanzibar huteua na kuwaapisha wakuu wa mikoa ya huko.Tanzania Bara ina mikoa 26 na Zanzibar ina mikoa 5,kwa hiyo Tanzania kwa ujumla ina mikoa 31.

Tuangazie Wakuu wa mikoa 26 ya Tanzania Bara kwa maana ya utendaji kazi wao, kujitoa kwa ajili ya wananchi,kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi, ubunifu katika kazi na katika masuala yote ya kumsaidia Mheshimiwa Rais.
Hii ndio top ten(10) kwa utendaji (mabingwa wa kutatua kero za wananchi)

1. Anthony Mtaka(Simiyu)
2. Paul Makonda(Dar es Salaam)
3. Mrisho Gambo(Arusha)
4. Aggrey Mwanri(Tabora)
5. Marco Gaguti( Kagera)
6. Ally Hapi(Iringa)
7. Adam Malima(Mara)
8. Alexander Mnyeti(Manyara)
9. Evarist Ndikilo(Pwani) na
10. Robert Gabriel(Geita)

Niliowataja hapo juu kusema ukweli wanajitahidi sana kutatua kero na matatizo yanayowakumba wananchi tena kwa njia shirikishi ikiwemo mikutano ya hadhara.

Wafuatao ndio tano mbovu (Wabovu kabisa kiutendaji) na sijui kwa nini hawapigwi chini.Ukiangalia utendaji kazi wao wanazidiwa mbali mno na hata ma DC na wapo wapo tu. Kazi yao ni kupambana na waajiriwa wa serikali wanyonge kama walimu, watendaji wa kata na vijiji n.k. Utashangaa kuona RC mzima anakagua andalio la mwalimu wa darasa la pili au kuingia madarasani kipindi mwalimu anafundisha kana kwamba yeye ni afisa elimu anayefahamu mambo ya shule na mikoa yao ndio inafanya vibaya mno kimasomo kwa mfano Lindi ya Godfrey Zambi.

Badala ya kushirikiana na walimu kutafuta njia bora ya kufaulisha yeye anapita mashuleni kutishia walimu,watafanyaje kazi kwa amani kwa mtindo huo? Mwingine kazi yake ni kukimbizana na kutishia watendaji wa vijiji na kata na wakati mwingine kuwaweka ndani wanyonge hawa. Mbona ma DC na ma DED hukosea sana na nyie ma RC hamthubutu kuwaweka ndani? Mimi ni mwana CCM damu kabisa na wengine niliwatangulia kujiunga CCM nawaambia acheni kuonea watu, tatueni matatizo kwa njia shirikishi na siyo ubabe. Unamtishia mtendaji au mwalimu unategemea atafanya kazi kwa amani? Huwa hatusikii mambo haya ya ajabu kwa Anthony Mtaka na mkoa wake unafanya vizuri katika nyanja zote, nendeni mkajifunze.

Top 5 mbovu
1. Godfrey Zambi(Lindi)
2. Gelasius Byakanwa(Mtwara)
3. Zainab Telack(Shinyanga)
4. Christina Mndeme(Ruvuma) na
5. Loata Sanare(Morogoro)

Wengine ambao sijawataja kwenye top 10 best performers na 5 mbovu wako katikati ila inabidi wajirekebishe.Wakuu wa mikoa wameteuliwa kuhudumia wananchi na siyo kuwafrustrate acheni kutumia madaraka yenu kuwanyanyasa wafanyakazi wanyonge wa nchi hii,wewe unamtishia mtendaji,mwalimu mkuu au headmaster kwa faida gani umeshindwa kumwelekeza tu?

Hawa watu wanaitumikia hii nchi kwa kujitoa sana na kwa matatizo makubwa huko vijijini.Mkitumbuliwa mnaanza kulialia,mjirekebishe.
 
Mtajuana wenyewe huko hayatuhusu sisi, mnakula pesa zetu bure vyeo mnapeana kwa ahsante.
 
Huyo mama wa Ruvuma Mndeme ana afadhali kidogo japo ni kisirani.
 
Pilitoni,
Anyway ni maoni yako tu lakini mkuu wa mkoa bora zaidi ni mama Anna Mgwira (Kilimanjaro) na mbovu zaidi ni yule wa Dar, huyu nashangaa bado yupo kazini ila nafamu ana kazi "nyingine" kwa jiwe.
 
Pilitoni,
Wote ni majembe ndio maana kuna wengine hukuwataja lakini wamemaliza miaka mitano kwenye mikoa yao.
 
Mkuu umetumia vigezo gani kutambua uwezo na umahiri wa utendaji wa viongozi hawa?
 
Back
Top Bottom