Pre GE2025 Wakuu wa shule kumchangia fedha ya kuchukua fomu ya Urais Rais Samia 2025, hiki ni "kituko" cha kufungia mwaka

Pre GE2025 Wakuu wa shule kumchangia fedha ya kuchukua fomu ya Urais Rais Samia 2025, hiki ni "kituko" cha kufungia mwaka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kama mdau wa Elimu na maendeleo ya kijamii, taarifa za wakuu wa shule kumchangia Mama Samia fedha za kuchukua fomu ya Urais kabla ya mchakato husika kuanza linaleta ukakasi na maswali mengi juu ya uwezo wa kupambanua mambo wa hawa viongozi walioaminiwa kusimamia elimu ya watoto wetu.

Je, kiongozi wa umma anaruhusiwa kuonyesha msimamo wake wa kisiasa hadharani?

Je, wamejuaje kama Rais Samia atagombea 2025?

Je, wana uhakika gani chama chake kitampitisha?

Kulikuwa na haraka gani kufikia hili azimio kipindi hiki ambacho hata mchakato haujaanza?

Tuamini kuwa hili nalo ni sehemu ya kujipendekeza? Kama ni kujipendekeza, wanawezaje kupandikiza ujasiri na kujiamini kwa walimu wanaowasimamia na watoto wetu? View attachment 2847719
Duh!!! Hili nalo lakushangaa!!
 
Isije kuwa walimu wawili wamekaa wakajiongopea huo uongo.kuna haja ya kupiga kula ili kujua wangapi wanaunga mkono hilo.
 
Nyerere, Mkapa, Magufuli n.k. wote hao walikuwa walimu. Naona wewe ni mbwabwajaji kama walivyo Wabwabwajaji kama wewe.
Kujificha kwenye kivuli cha Mwl. Nyerere na wengine hakuwafanyi walimu wote waonekane weredi. Kwa mtazamo wako, hiki walichokifanya kwa wakati huu unaona ni sahihi? Kumbuka kuwa aliyetokea mbele ya kamera ni kiongozi na anasema ni moja ya azimio la kikao chao cha TAHOSSA (Umoja wa wakuu wa shule Tanzania) na yeye ndo muweka hazina wao. Kwa lugha rahisi, Wakuu wa shule wote wamekubaliana yafuatayo kuhusu azimio hilo:-

1. Mwezi huu wa 12 mwaka 2023 ni sahihi kwao kujichagulia mgombea wa mwaka 2025 ambaye hata hatokani na umoja wao bali chama cha siasa

2. Ni sahihi kwao kama watumishi wa umma kuonyesha hisia zao hadharani za mlengo wao wa kisiasa

3. Hawaoni sababu ya kusubiri chama husika kimtangaze mgombea ndipo wamuunge mkono? Wanajuaje kama chama kitampitisha?

Wao kama "wasomi" wanaotakiwa kufanya maamuzi kwa umakini, wanapeleka ujumbe gani kwa jamii kujitokeza hadharani mapema yote hii?

Je, likitokea kundi lingine la wakuu wa shule wakatangaza kumchangia fedha ya kumchukulia fomu ya urais Tundu Lisu, wataachwa salama? Madaraka yao wataachwa nayo?

Ifikie hatua mamlaka za uteuzi wa watu kama hawa wanaosimamia mambo ya msingi ya kijamii wateua watu makini na weledi kuliko kujaza wanasiasa wanaowaza teuzi za juu kila kukicha
 
Back
Top Bottom