Wakuu waliotumia boom kutoboa kimaisha watupe uzoefu waliwezaje? Au it's impossible

Wakuu waliotumia boom kutoboa kimaisha watupe uzoefu waliwezaje? Au it's impossible

Michael Mlay

Member
Joined
Aug 24, 2022
Posts
57
Reaction score
84
Habari zenu wakuu,wakubwa shikamoni

Straight to the point,Niko mwaka wa tatu chuo x, niliingia na mipango mingi sana nilivyotoka advance ya kusave boom ili ikiwezekana nifungue biashara kwasababu home hali ndo hivyo maisha sio mazuri sana

Tunapewa elimu tu mtaji utajua mwenyew na sababu nyingine najua mnaelewa degree nyingi ziko mtaani wakuu hazina kazi, kwahiyo nikasema nijibanebane duuh lakini naona nagonga mwamba kabisa mwaka wa pili nilifanikiwa ila bado sikufikia malengo,

Sasa niko mwaka wa tatu semester ya kwanza bado maboom 3 ,ushauri wenu wakuu kama kunamtu alifanikiwa kupitia boom atupe uzoefu kidogo.Nawasilisha

SPIRITUAL WORLD drive fresh world
 
Una nia ya Mafanikio?

Kama una nia, Je, wewe unatabia ya kusave sehemu ya boom walau ukimaliza uwe hata na 5M?
 
Kuna mmasai mmoja alituambia aliweza kujenga nyumba ya vyumba vitatu kwao kwa kutumia boom

Mimi nilishindwa kabisa kusave na bado lilikuwa likikata naomba hela nyumban
 
Utoboe kimaisha kwa hela ya boom? Hiyo si hela ya kula tu?
 
Mimi Nilikuwa nabana breakfast so nakuja kula lunch....ambayo ni juice ya jero na andazi la jero ... total 1000
Na nlifanikiwa

But a few moment later nlipata utapia mlo[emoji23][emoji23]
 
Anzia hapohapo chuoni kuizungusha, zamani walikuwa wanauza ubuyu, pipikifua na kashata
Ila kwa sasa ni teknologia, uza flash drive, SATA drive, vocha za mitandao , chargers za simu na ikiwezekana kuwa agent wa miamala ya mitandao.
 
Back
Top Bottom