Walaaniwe wale wote wanaoendelea kupanga kuwanyonya maskini kupitia kodi na tozo

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Ole kwao ambao wananchi hawa maskini waliwapa dhamana ya kuwaongoza wakitegemea kuboreshewa maisha na kinyume chake wanawatesa kupitia kodi na tozo zisizo na maana.

Ole wao kwa kuwa tunajua hizi zote ni lengo lao la kujilimbikizia mali zaidi na utajiri kwa ajili yao na familia zao.

Ole wao wanapolala, ole wao wanapoamka. Ole wao wanaposafiri na ole wao wanapopumzika.

Walaaniwe ofisini, walaaniwe nyumbani. Walaaniwe waingiapo walaaniwe watokapo. Walaaniwe uzimani na walaaniwe ugonjwani.

Wajipalie makaa ya moto vichwani mwao kila wanapojadili na kutimiza matakwa ya kuwanyonya maskini. Wajipalie makaa hayo mchana na usiku pia.
 
Wafanyabiashara wanachuma nchi imeanza matabaka kwa kasi sana
 
Kazi yao kubwa ni kupiga pesa za wananchi
 
Malengo ya hizi tozo za kunyonya wanyonge kuna hila ndani yake, hivyo laana lazima ikamate kunako......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…