Waje pia mashambani walime mahindi gunia wauze elfu ishirini. Wamwage kemikali ardhini miaka michache baadae ardhi isizalishe waondoke zao.
Waje pia wapewe ziwa Victoria samaki kilo auzwe elfu tatu, wavue wakombe kila kitu hadi mayai ya samaki. Miaka minne mbele ziwa libaki na majitaka hamna viumbe.
Waje pia migodini wafukuze wabongo wote wakae wao, kwanini wabongo watajirike. Inabidi sote tuwe masikini kama mleta mada.
Wachina pia waanzishe makampuni ya utalii, wabongo wafukuzwe. Wamiliki wa hoteli kwanini wanauza one meal 50,000? Waje Wachina wajenge mahoteli 5 na dinner iwe elfu tano tu na maji ya kunywa bure.
Kwanini unaona Kariakoo ndio wanapata faida peke yao, kwenye sekta yako unahisi Wachina hawawezi fanya kwa bei nafuu zaidi? Unaonaje ukawaachia wao wewe ukajishughulisha na kukata viuno.