Walanguzi wa Kariakoo wanasumbua sana Shati la Tsh 5,000 unauza 30,000?

Najiuliza tu mchina akijua bei za awali unadhani atauza jinzi elfu 5 wakati watu walikuwa wananunua 18k(hakuna mfanyabiashara asiependa faida kubwa)

Vipi kama mchina akiwa yeye ndio yupo pekee(monopoly) beinza ajabu haziwezi kurudi.

Najaribu kuwaza suluhu, serikali ingeweka system, tukawa na viwanda vya kutosha mbona bei zingekuwa poa, kuliko hii kumkaribisha mchina sehuleni kabisa, nchi inajifia hii taratibu kabisa...
Wachina wamewezaje kwanini sisi tushindwe hapo ndipo unapoona hatuna serikali ya kutoongoza kwenye maendeleo, ila tunawachangia kodi zetu wale bata.
 
Kila nikifikiria usumbufu wa mawinga naona bora Wachina tu japo ndio hivyo kwa uwepo wao uchumi wa viwanda utabakia ndoto za mchana tu.
 
Mchina akiwa Monopoly halafu aanze kuuza bei za ajabu itabidi tumfukuze waje hata Waturuki au Wabangladesh.
 
Akiwa Monopoly halafu aanze kuuza bei za jabu itabidi tumfukuze waje hata Waturuki au Wabangladesh.
Tutakuwa hatujamaliza tatizo,
Hapa kutatua tatizo serikali ingeweka mipango kabambe tuwe na viwanda vingi sana, tuwe na nishati ya kutosha kwa bei rahisi sana, miundo mbinu mizuri barabara, treni ya umeme isambae kila kona, usafiri wa ndege kwa bei rafiki..mzigo unafika kwa mteja wa mwisho kiurahisi na gharama za uzalishaji na usafirishaji zinakuwa ndogo mnooo
 
Hayo yameshindikana, acha tuishi kwa ubaya ubwela tu.
 
Tupe Mchimbo ha Wachina Hayo na Sisi na uzee wetu tukapate
 
Nonsense! Watu wanaongea uhalisia wewe una-panic
 
Wachina walio wengi wanakwepa vitu vingi na pia wana back up kubwa huko juu ndo maana mnaona wanauza vutu rahisi na wanauza lonya…vip kuhusu mall yao ya Home City pale mliman na iliokua Mikocheni vipi hizo bidhaa ubora wao, mwiko buku ila ukigeuza nyama kilo moja siku 2 umevunjika.

Wabongo wenzetu kwel unaweza sema wanaweka faida kubwa ila gharama wanazopitia ni kubwa pia mfano; nilikua na jamaa mmoja alkua anafungua hardware kkoo store ilkua ghorofani kodi ni 3M per month na kkoo wanachukua 12 month kodi sawa na 36M, showroom ama duka sas lile kodi ilkua 1M kwa mwaka 12M… hapo TRA hawajafika, bandari hujamalizana napo, wafanyakazi, huduma za kawaida kama usafi kkoo ni 40k per month, ulinzi na gharama zngine tusizo zijua hawa watu wanapagawa biashara kkoo n ngumu msichukulie mambo poa.

Nilkutana na mchina mmoja wa viatu yeye ana meza kaweka mbongo nje kama machinga alaf mzee anashika order, store iko manzese ana mzigo mbwa haruki sas analipia 20k kama machinga ataacha kuuza kitonga, ama mtu ana mareject ama unaitwa no look kaleta huku kama dampo kwa mpk hapa gharama buku 4 kadeti ataacha kuuza 7k unakuata kaingiza pcs 10-15 elfu…

Pia nilchogundua watu wengi wanaolia na wachina kwamba ni bora hawajui vitu wachina wengi wanaleta mbangu…mfano nguo ndo maana kuna watu wanaojiita vuja x na sijui x sportswear wameamua kuwin market kwa lonya jeans 15 hyo ukitanua mguu tu imechanika, ama jeans inachuja ukiifua mara mbili tu nyeus imekua brown. Kupenda kitonga wewe chagua mwenyewe tu usipinge biashara za watu umeshindwa kuingia kwa aziz kunua jeans nenda vunja utapata ila kuaminishana wachina wanatusaidia miaka ya mbeleni wakitake over watoto tuliowasomesha watakuja kuwa ndo wabeba cargo wao.

Rahisi ina gharama yake.
 
Kikubwa wafanyabiashara wa huku wajue kujiongeza panapokua na ushindani , watoke kwenye ufanyaji biashara kama enzi hizo watu bado hawajafunguka,,,,,,
 
Dah kula kwako ndo mwengine aumie dah.......faida sawa lazima mfanyabiashara apate ila sio kwa hilo gap wanaloweka
Lazima nile kidogo, ndio biashara ilivyo.
 
Hyo Tv ya lakii 6 nch60 kampuni samsung ukiwasha inaandika wisdom Tv… narudi pale pale wapenda vitonga hawajui vitu hawajui mambo.

Viatu mfano airforce wakina sportswear wanauza kuanzia 25k..ila nenda kwa mama ama kwa 4G kkoo ana quality kwa jumla anauza kuanzia 70k-110k na ukiangalia na hy ya 25k ama 40 unaona kabsa n kifo na usingizi nlshawahi kuagiza airforce pc moja china quality ya juu niliinunua 85 elfu na nilrdhka nlvyoipokea sio haya maboksi tunayoita viatu huku.

Hvyo vitu vya rahis ata kwa wabongo wenzetu vipo ila ni uchafu kiuhalsia sas washamba wa mambo ndo matetemekea ngozi nyeupe unachotakiwa kujua mchina anakupa kutokana na mfuko wako una pesa ngap? Chunguza ndo uongee.
 
Kikubwa wafanyabiashara wa huku wajue kujiongeza panapokua na ushindani , watoke kwenye ufanyaji biashara kama enzi hizo watu bado hawajafunguka,,,,,,
Kujiongeza ili ukimbizane na soko kwa hapa tanzania ni vitu vitatu kwa ninavyoona mimi,

1.Ukwepe kodi.
2.Uwe na connection yakukufanyia favour kwnye mambo yako. (Connection kubwa kwa wenye mamlaka).
3.kudeal na lonya, reject ama no look look

Sas kama ni sahihi kwa uchumi wa taifa na huduma kwa jamii ni sawa haya.
 
Hayo machimbo yapo wapi kwa huku Mpigamiti Liwale?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…