Hisha Sorel
Senior Member
- Dec 27, 2017
- 192
- 140
- Thread starter
- #21
Nilihoji kwa muda mrefu.
Halafu rafiki yangu mmoja, nilipokuwa na miaka takriban 20, akaniazima kitabu kinaitwa " The Philosophy of Religion - An Anthology".
Kitabu kimejaa habari za dini. Si za kupinga uwepo wa Mungu tu, bali mpaka arguments za kuonesha Mungu lazima yupo.
Nimekisoma kitabu chote. Na kukirudia sana.Kimekusanya karibu mambo yote kuhusu dini.
Kuna sehemu ilikuwa inaongelea "the problem of evil".
Hapo palikamilisha vizuri safari yangu kusema Mungu hayupo.
Nilishawahi kukiweka kitabu hapa.
Kutoka hapo, sijarudi nyuma.
Hate mimi pia nilisoma kitabu cha THE GOD DELUSION cha professor Richard dawkins, nakumbuka argument yake moja alipo uliza: "kwanini mungu wako we ni sahihi, na kuanza kutaja miungu yote ndani ya historia" . Hii argument niliangaika nayo sana ki-science, hatimaye ikabidi nichague; kujidanganya kwa kuziba masikio na macho; au kukubali ukweli kwamba hakuna ushahidi wa kuwepo kwa mungu.
kwahiyo nakuelewa sana mkuu🤝