Wale ambao toka ujiunge jf hujawahi kukutana na member yoyote

Nimekutana nao wengi sana na tumefanya mengi sana.
 
I dont meet and talk to strangers. Huwa tunamalizana hukuhuku kwenye comments
Kuna biashara lazima uonane na member,kule kwenye jukwaa la kilimo na biashara. Vinginevyo huwezi fanya biashara mtandaoni mfano unahitaji mazao au shamba la kununua au kukodi au gari,lazima muonane tu.
 
Humu najuana na Maxence Mello kwa kuonana ingawa ilikuwa kitambo sana na nilikuwa siijui JF. Nilivomuona na marafiki zake na classmates wake kadhaa ndo nikapata kuifahamu. Mwingine ni jamaa mstaarabu sana nilikutana nae kwenye daladala niko nimesimama akacomment kitu kwenye uzi nikasoma comment then nikaingia na kuscroll down nikawa nimemfahamu, sikumwongelesha kabisa.
 
Niliwahi kumuhuisi dada mmoja niliyemuona njia panda ya ulaya, jinsi nilivyomuona, swaga na kwa mbaali nikaona anaperuzi JF, nikajisemea huyu anaweza kuwa Lara1....

Niliishia kuhisi....sijawahi hata kwa bahati mbaya kumkuta mtu anaperuzi JF, achilia mbali kukutana au kufahamiana na mtu yeyote.....ingawa nimeanza kufuatilia hii forum kabla ya kuitwa Jamii.
 
Wengine humu ni mafundi wazuri mbona wanakuja home tunenda kwao unaogopa nini ?wemgine wapo kibiashara. Nilishawai letewa mzigo toka USA na jf member hapa nikaufuata ofisini kwake. Nikabeba mzigo sikuuliza eti mwenye ID fulan JF yupo hapa.

Labda nyie mnaofuata madem. Umenikumbusha serikali wakati fulani walikamata condom fake wakaenda kuzichoma watu wengi wali panick.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…