Wale ambao tunaishi na watoto wa watu na hatujapeleka hata 100 ya mahari tukutane huku

Mimi napeleka mwaka huu.
 
Huo ni mfumo dume tu, kwani mwanamme halelewi?

Huu ni utamaduni wa kumuuza mwanamke, kumfanya bidhaa. Ni utamaduni unaoshusha utu wa mwanamke.

Ndiyo maana wanaume wengi wa Kiafrika wanamuona mwanamke ni kama mali yao.

Wanaona wamemnunua kwa mahari ati.
 
Afrika, mwanaume ndio anao, ndie anatoa mahali nasikia India wanawake ndio wanatoa mahari sina uhakika, mfumo wa maisha unayoishi wewe utakuwa wa ughaibuni wa kibepari jamii ya kibepari wanawake wana Mali, familia zote zina Mali, ughaibuni ubeparini maisha ya ndoa yako tofauti na Afrika.

Ni kweli ughaibuni hakuna mfumo dume ndoa kinachoangaliwa ni nyie kupendana si ajabu mtoto wa Bill gate kuolewa na mfanyakazi wa kampuni ya simu hapa Tanzania, Africa wanawake wanafuata security iliyoko kwa mwanaume wewe huoni wanawake wenyewe wanaubariki huo mfumo dume hata wazazi wakiozesha mtoto huuliza huyo mkwe anafanya shughuli gani hawaulizi kama eti anakupenda kweli mnapendana kweli.

Africa wanaume ndio walioshika uchumi kwa asilimia kubwa, huku Afrika hata kama mwanamke ana nguvu za uchumi ataangushwa na ukoo wake ambapo wengi watakuwa maskini watapenda mtoto wao aolewe na mwanaume mwenye uwezo kiuchumi amtunze vizuri binti yao na awe msaada kwa ukoo utakapohitajika, ni mambo ya mfumo wa maisha kwa nchi maskini za kiafrika, tamaduni na mila sio biashara kama unavyojaribu kubainisha.
 
Hii mentality ni moja ya sababu Afrika inakuwa masikini.

Tumemfanya mwanamke kama bidhaa, si mtu.

Mpaka pengine wazazi wanamuuza binti ili wapate mahari.

Sawa na ng'ombe tu.
 
Hii mentality ni moja ya sababu Africa inakuwa masikini.

Tumemfanya mwanamke kama bidhaa, si mtu.

Mpaka pengine wazazi wanamuuza binti ili wapate mahari.

Sawa na ng'ombe tu.
Sio kweli mahali ni kama zawadi tu mahalu zenyewe mara nyingi kipesa kama laki 5 mpaka milioni 2 pesa hiyo ndio thamani ya mtu, toka binti azaliwe mpaka anaozeshwa ilitumika mil 2 na mil 2 wazazi wakipewa itawasaidia nini kiuchumi mahali ni kama Asante au zawadi kuonesha appreciation.

Huko ughaibuni unakoishi wanawake wanapenda zawadi sana mabingwa wa kudanga na wanachokiita escort nyie hamuoni kama waafrica wakija ughaibuni kuadapt mfumo wa kuanzisha ndoa na hao wabepari unaowaona Wana mentality bomba kama umejaa utata mtupu, ndugu zangu wameoa wazungu Mimi mwenyewe nimeshakuwa na urafiki na mwanamke mzungu.

Ukweli utabaki ukweli mfumo wa Africa kwa mahusiano ni bomba kuliko huo mfumo unaotaka kuutetea, nitajie mifano mitano ya waafrika waliooa na waughaibuni kama ndoa zipo njema hizo unazosema mwanamke anafurahia kuheshimika, hajioni kama bidhaa kabla sijakutajia jinsi wanawake wote hulenga mali na jinsi hao wazungu wanavyohusudu kutengana wapate mgao wa mali huoni kama ndoa huko zinageuzwa kitega uchumi, unaona ya Afrika tu kuwa mwanamke anafanywa bidhaa.
 
Wewe kwanza hujui tofauti ya mahali na mahari, mpaka hapo unanipa shaka kwamba unaweza kujadiliana mambo makubwa ya kifalsafa na mimi.
 
Mahari imepitwa na wakati.

Inashusha utu wa mwanamke, inamfanya mwanamke awe ananunuliwa kama ng'ombe.

Kitu muhimu watu wajenge familia tu.

Hiyo familia ya huyo mwanamke imeelewa hilo.
Ukiwa maskini oa maskini wenzio bure wenye pepo la umaskini kama wewe kama huwezi lipa mahari

Wazazi popote mlipo usije kubali mwanao aoelewe bila kudume kulipa mahari unamuoza mwanao kwenye shetani mkubwa aliyyejaa mapepo ya umaskini

Kama hela ya mahari muoaji hana mwambieni kabisa wewe pepo uliyejaa umaskini kaoe mipepo mwenzio iliyojaa umaskini kwani hujaiona huko ulikotokea kuwe kijijini kwenu au popote
Kwenda zako huko na mipepo yako ya umaskini hatuitaki mipepo yenu kwenye familia yetu
 
Tatizo lako huwezi kufanya mawazo ya kimantiki na kifalsafa. Unakimbilia assumption kwamba kila kitu kinaendeshwa na uchumi, halafu hata huo uchumi wenyewe una conclude kwa logical fallacy ya non sequitur.

Ukisikia mtu anapinga mahari, una assume anapinga mahari kwa sababu ya umasikini.

Wakati inawezekana kabisa wanaotaka mahari ndio wanataka mahari kwa sababu ya umasikini.

Nyerere hakuwa masikini, alikuwa mtoto wa Chifu, baadaye akaja kuwa rais wa nchi, lakini alipinga mahari kwa misingi ya kifalsafa na kimantiki.

Ila, naelewa si kila mtu ana uwezo wa kuelewa hilo kwa hoja zangu ambazo ziko sawa na hoja alizozitoa Nyerere.


"Nyerere describes bride price as evil in posthumous bio"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…