nyanda madirisha
JF-Expert Member
- Apr 1, 2019
- 411
- 727
Napita tu hapa maana naona kama pananihusu kwa mbaaali sana maana nina deni kule lkn nimetoa chochote tayari.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi napeleka mwaka huu.kusema ukweli huyu mwanamke ninaye ishi nae nilimchukulia kwa dada yake na kuamua kuanza maisha na yeye.
Basi bhana ilitokea msiba nyumbani kwao ikabidi tuende wote, na baada ya msiba kuisha ikabidi mambo mengine yaendelee ikiwepo kikao kuyahusu maisha yangu na yeye lakini kwa busara zao wakaniambia niende nikapambane siku nikipata kidogo niende nacho ili wakanitajie rasmi kiasi cha mahari,
Hiyo ni inferiority complex yako tu.Huu uzungu ndo unawaponza wengi, mila na desturi zetu ziheshimiwe...
Huo ni mfumo dume tu, kwani mwanamme halelewi?Mahari ni Utamaduni ,ina maanisha usione vyaelea vilitunzwa mpaka unakutana nae ,alizaliwa akalelewa alisomeshwa aliuguzwa alipoumwa akakua akasaidiwa aanze maisha Sasa wewe unakutana nae yupo ready na maisha labda kaanza kujitegemea na wewe tayari umeanza kujitegemea ni rahisi kusema mmepandana muanze maisha pamoja kwa tamaduni za Africa mtahesabika nyie wahuni tu mmechukuana mnafanya uzinzi tu hamtapata baraka za wazazi ne je mtoto wa watu akikufia utamzika mwenyewe ,akikuambia wazazi wake wanaumwa utaenda kuwaona wazazi wake wewe kama nani .Jamii za watu wa Ulaya na America nyingi ndio hazina hizo mambo ya mahari sababu kubwa zimekomaa na maisha ya kibepari na Serikali zao zina pesa kusaidiana mahitaji binafsi ya watu sio lazima ndugu wahusike kwa Africa tamaduni na Serikali hazijimudu kihivyo ,tamaduni za kiafrica zinaishi kindugu ,zinauguzana ,zinasaidiana zinafurahi na kuhuzunika pamoja ,harusi kwa Africa ni jambo la kindugu na kijamii ,mahari ni sehemu ya tamaduni za Africa hata kama mmeona ulaya peke yenu itawabidi mje Africa kutimiza matakwa ya kitamaduni ,hata makanisani mkitaka mjifungishe ndoa mtaulizwa kama mmemalizana na mambo ya tamaduni zenu kama mahari na wakati mwingine mahari sio lazima.pesa inaweza ambiwa lete blanket ,lete mashuka let ng'ombe ,mbuzi au kuku unajua maana yake? Vijana wengi wa siku hizi wakitajiwa hivyo husema wapigiwe hesabu hivyo vitu shs ngapi ,wazee wanaojua mila hukataa pesa hutaka kama blanket ulete blanket kwao blanket ni kumbukumbu ya kumuaga mtoto wait kuliko pesa ambayo watatumia itaisha na haitakuwa kumbukumbu nzuri ya kuagana na binti yao
cc JoannahMahari imepitwa na wakati.
Inashusha utu wa mwanamke, inamfanya mwanamke awe ananunuliwa kama ng'ombe.
Kitu muhimu watu wajenge familia tu.
Hiyo familia ya huyo mwanamke imeelewa hilo.
Afrika, mwanaume ndio anao, ndie anatoa mahali nasikia India wanawake ndio wanatoa mahari sina uhakika, mfumo wa maisha unayoishi wewe utakuwa wa ughaibuni wa kibepari jamii ya kibepari wanawake wana Mali, familia zote zina Mali, ughaibuni ubeparini maisha ya ndoa yako tofauti na Afrika.Huo ni mfumodume tu, kwani mwanamme halelewi?
Huu ni utamaduni wa kumuuza mwanamke, kumfanya bidhaa. Ni utamaduni unaoshusha utu wa mwanamke.
Ndiyo maana wanaume wengi wa Kiafrika wanamuona mwanamke ni kama mali yao.
Wanaona wamemnunua kwa mahari ati.
Kaanza umuha wake yaani huyo ni shida😅😅😅😅😅😅
Hii mentality ni moja ya sababu Afrika inakuwa masikini.Africa ,mwanaume ndio anao , ndie anatoa mahali nasikia India wanawake ndio wanatoa mahali sina uhakika , mfumo wa maisha unayoishi wewe utakuwa wa ughaibuni wa kibepari jamii ya kibepari wanawake wana Mali ,familia zote zina Mali ,ughaibuni ubeparini maisha ya ndoa yako tofauti na Africa ,ni kweli ughaibuni hakuna mfumo dume ndoa kinachoangaliwa ni nyie kupendana si ajabu mtoto wa Bill gate kuolewa na mfanyakazi wa kampuni ya simu hapa Tz ,Africa wanawake wanafuata security iliyoko kwa mwanaume wewe huoni wanawake wenyewe wanaubariki huo mfumo dume hata wazazi wakiozesha mtoto huuliza huyo mkwe anafanya shughuli gani hawaulizi.kama.eti anakupenda kweli mnapendana kweli ,Africa wanaume ndio walioshika uchumi kwa.asilimia.kubwa huku Africa hata kama mwanamke ana nguvu za uchumi ataangushwa na ukoo wake ambapo wengi watakuwa maskini watapenda mtoto wao aolewe na mwanaume mwenye uwezo kiuchumi amtunze vizuri binti yao na awe msaada kwa ukoo utakapohitajika ni mambo ya mfumo wa maisha kwa.nchi.maskini za kiafrica ,tamaduni na.mila sio biashara kama unavyojaribu kubainisha
This logical fallacy is called "appeal to tradition"Huu uzungu ndo unawaponza wengi, mila na desturi zetu ziheshimiwe...
Sio kweli mahali ni kama zawadi tu mahalu zenyewe mara nyingi kipesa kama laki 5 mpaka milioni 2 pesa hiyo ndio thamani ya mtu, toka binti azaliwe mpaka anaozeshwa ilitumika mil 2 na mil 2 wazazi wakipewa itawasaidia nini kiuchumi mahali ni kama Asante au zawadi kuonesha appreciation.Hii mentality ni moja ya sababu Africa inakuwa masikini.
Tumemfanya mwanamke kama bidhaa, si mtu.
Mpaka pengine wazazi wanamuuza binti ili wapate mahari.
Sawa na ng'ombe tu.
Wewe kwanza hujui tofauti ya mahali na mahari, mpaka hapo unanipa shaka kwamba unaweza kujadiliana mambo makubwa ya kifalsafa na mimi.Sio kweli mahali ni kama zawadi tu mahalu zenyewe mara nyingi kipesa kama laki 5 mpaka milioni 2 pesa hiyo ndio thamani ya mtu ,toka bintu azaliwe mpaka anaozeshwa ilitumika mil 2 ,na mil 2 wazazi wakipewa itawasaidia nini kiuchumi mahali ni kama Asante au zawadi kuonyesha appreciation huko ughaibuni unakoishi wanawake wanapenda zawadi sana mabingwa wa kudanga na wanachokiita escort nyie hamuoni kama waafrica wakija ughaibuni kuadapt mfumo wa kuanzisha ndoa na hao wabepari unaowaona Wana mentality bomba kama umejaa utata mtupu, ndugu zangu wameo wazungu Mimi mwenyewe nimeshakuwa na urafiki.na mwanamke mzungu ukweli utabaki ukweli mfumo wa Africa kwa mahusiano.ni bomba kuliko huo mfumo unaotaka kuutetea ,nitajie mifano mitano ya waafrica walio oa na waughaibuni kama ndoa zipo njema hizo unazosema mwanamke anafurahia kuheshimika hajioni kama bidhaa kabla sijakutajia jinsi wanawake wote hulenga mali na jinsi hao wazungu wanavyohusudu kutengana wapate mgao wa mali huoni kama ndoa huko zinageuzwa kitega uchumi unaona ya Africa tu kuwa mwanamke anafanywa bidhaa
Ukiwa maskini oa maskini wenzio bure wenye pepo la umaskini kama wewe kama huwezi lipa mahariMahari imepitwa na wakati.
Inashusha utu wa mwanamke, inamfanya mwanamke awe ananunuliwa kama ng'ombe.
Kitu muhimu watu wajenge familia tu.
Hiyo familia ya huyo mwanamke imeelewa hilo.
SIO kweli.Mmama wa kichaga umbebe mwanae hivi 😂😂😂 utajua hujui
Tatizo lako huwezi kufanya mawazo ya kimantiki na kifalsafa. Unakimbilia assumption kwamba kila kitu kinaendeshwa na uchumi, halafu hata huo uchumi wenyewe una conclude kwa logical fallacy ya non sequitur.Ukiwa maskini oa maskini wenzio bure wenye pepo la umaskini kama wewe kama huwezi lipa mahari
Wazazi popote mlipo usije kubali mwanao aoelewe bila kudume kulipa mahari unamuoza mwanao kwenye shetani mkubwa aliyyejaa mapepo ya umaskini
Kama hela ya mahari mnataka hana mwambieni kabisa wewe pepo uliyejaa umaskini kaoe mipepo mwenzio iliyojaa umaskini kwani hujaiona huko ulikotokea kuwe kijijini kwenu au popote
Kwenda zako huko na mipepo yako ya umaskini hatuitaki mipepo yenu kwenye familia yetu
Amesahau kuwa bado Upo JFKaanza umuha wake yaani huyo ni shida😅😅😅😅😅😅
Hata manabii walilipa mahari maandiko yanasemaMahari ni tamaduni yetu pendwa
wala si utumwa
wala si kumnunua mwanamke
Mahari ni heshima kama zawadi iwa familia. Ya kukutunzia mke wako. .
Mahari haiko Africa tu, ipo kwenye jamii nyingi sana duniani. .
Lipa mahari Linda heshima ya mwanamke na familia yake. .