Wale Graduate mlioweza kujiajiri mlitumia mbinu (njia) kuweza kujiajiri?

Wale Graduate mlioweza kujiajiri mlitumia mbinu (njia) kuweza kujiajiri?

Mayor Slum

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2017
Posts
760
Reaction score
1,150
Kutokana hili tatizo la ajira kuzidi kuongezeka hapa nchini na kuacha baadhi ya Graduate wakizagaa tu mtaani, kuzurula mtaani, kukaa nyumbani tu naomba mtu anisaidie kutupa njia au mbinu mlizotumia kuweza kujiajiri.

Graduate wengi sana wapo mtaani kwa sasa hawajaweza kujiajiri, wengine bado wanasumbuliwa na mawazo (stress) zaidi ya mwaka wa tatu sasa hivi. Je, nyie mlioweza kujiajiri mlianzaje hadi mkafanikiwa kujiajiri ?

Ni njia (mbinu) gani mlitumia hadi mkaweza kujiajiri?

++Kama vile kupata mtaji(mlianza na mtaji wa shingapi?)

++Biashara mlizo anza nazo

+++Changamoto

+++ Kukwepa aibu na mengineyoo


Naomba mtuambie jinsi mlivyo fanya hili litasaidia sana graduate waweze kupata fikra mpya na waweze kujiajiri huku wanatafuta ajira wengine wajiajiri kabisa kuliko kukaa tu nyumbani, kuzurula mtaani, kushinda kwenye mitandao.
 
Mzee mimi niliajiriwa na private company nimefanya kazi kama miaka 3 hivi ila hali ikazidi kuwa mbaya, baadaye nikapiga kazi chini nikaanza biashara ya mazao nilipiga root moja kisha wahindi wakashusha bei nikaachana nayo nikaanzisha biashara nyingine nilisota kama miezi 9 hivi mambo yakaanza kujiset yenyewe ila changamoto kuu ilikuwa capital.
 
Ni njia (mbinu) gani mlitumia hadi mkaweza kujiajiri?
++Kama vile kupata mtaji(mlianza na mtaji wa shingapi?)
Graduates nendeni mkajiajiri kwenye kilimo, acheni ubwege.

Mtaji wako mkubwa ni nguvu zako na elimu yako. Mashamba yapo ya bure kabisa ktk mikoa ya Katavi, Tanga, na Tabora. Yaani sijui mnataka nn tena?
 
Graduates nendeni mkajiajiri kwenye kilimo, acheni ubwege.

Mtaji wako mkubwa ni nguvu zako na elimu yako. Mashamba yapo ya bure kabisa ktk mikoa ya Katavi, Tanga, na Tabora. Yaani sijui mnataka nn tena?
Kilimo Sikuhizi ni Kama kubet due to the price fluctuation na ukizingatia graduates wana low capital na experienced. Kwa wanaoweza wafanye ila kama hujui chochote kuhusu Kilimo Anza kufanya research kwanza Ndo ukalime na ujipange Laa sivyo hatari
 
Kilimo Sikuhizi ni Kama kubet due to the price fluctuation na ukizingatia graduates wana low capital na experienced. Kwa wanaoweza wafanye ila kama hujui chochote kuhusu Kilimo Anza kufanya research kwanza Ndo ukalime na ujipange Laa sivyo hatari
Sasa kuliko kukaa bure huku wakiomba hata pedi na boksa toka kwa shemeji zao ni bora wakawa wanajishughulisha
 
Kutokana hili Tatizo la Ajira kuzidi kuongeza hapa Nchi nakuacha baadhi ya Graduate wakizagaa tu mtaani ,kuzulula mtaani , kukaa nyumbani tu naomba mtusaidie kutupa njia au mbinu mlizotumia kuweza kujiajiri

Graduate wengi sana wapo mtaani kwa sasa hawajaweza kujiajiri , wengine bado wanasumbuliwa na mawazo (stress) zaidi ya mwaka wa tatu sasa hivi je nyie mlioweza kujiajiri mlianzaje hadi mkafanyikiwa kujiajiri ?

Ni njia (mbinu) gani mlitumia hadi mkaweza kujiajiri?
++Kama vile kupata mtaji(mlianza na mtaji wa shingapi?)
++Biashara mlizo anzanazo
+++Changamoto
+++ kukwepa aibu na mengineyoo


Naomba mtuambie jinsi mlivyo fanya hili litasaidia sana graduate waweze kupata fikira mpya na waweze kujiajiri huku wanatafuta ajira wengine wajiajiri kabisa kuliko kukaa tu nyumbani , kuzulula mtaani, kushinda kwenye mitandaoni.
Hakuna mbinu maalumu kikubwa ni Commitment. Kama huna hakuna unacho weza kukifanya. Inahitajika sana kujitoa mhanga.

Na pia Commitment haiwezi kuwa transfared.
 
Mayor Slum, Mimi sio graduate ila kuna baadhi ya vitu Nimejaribu Wakati bado Nipo chuo. Kutokana na ajira kuwa ndogo ni vyema wanafunzi wa chuo wajiandae mapema kabla hawajamaliza na kuanza kuangaika kazi.
CAPITAL
mtaji kwa Kijana hauanzia na cash ila kama unayo sawa but kama huna capital na una wazo la kufanya kitu tumia kipaji chako kupata hela.

Pia kama unaona kabisa hauna kipaji basi tumia nguvu kwenye kazi halali upate hela ya kufanya biashara.

Kwa mfano, unaweza ukawa day worker kwenye sites za ujenzi just for the short time ili upate pesa ambayo itakuwezesha kupata mtaji, ukipata hata 20000 inatosha.

Kwa mazingira ya chuo biashara ya 20,000 inalipa. Unaweza kununua chocolate K/koo ukapita unauza chuoni ukimaliza pakti 2 una hela yako nzuri umeingiza kwa siku.

Jifunze kutunza pesa kwa kuizalisha usiiweke tu ndani hiyo nayo itakusaidia.

Kadri muda unavyokwenda utajikuta umewekeza kwenye biashara ndogo ndogo ambazo zinakuingizia kipato kwa siku hata 20000-30000.

CHANGAMOTO

Muda wa kufanya biashara na masomo ni kazi mno lakini kuna wale first learner wanaweza kumudu vitu vingi kwa wakati mmoja.
 
Mayor Slum, Kwangu Mimi nakwepa aibu kwa namna hii.

Kwa mfano, mwanafunzi wa chuo ataona aibu kuwa day worker ya ukondakta. But najiuliza wale makonda wa daladala kwani hawana familia?. Mbona unakuta mtu sawa umri wa baba yangu na anafamilia na watoto anasomesha na mbona haoni aibu.
Sasa kwanini mimi kijana nione aibu wakati najua hii kazi nitafanya kwa muda mfupi na nitapata pesa na nitatimiza malengo yangu.

Mimi malengo yangu nayaweka mbele zaidi kuliko kituchochote.

Pia stori za watu maarufu Kama simbachawene alikuwa mpiga debe kabla ya kuwa Waziri.
AY alikuwa analala kwenye kontena la washona nguo kabla hajawa super star .

So wanafunzi wa vyuoni na graduates wote wajue kwamba ili ufanikiwe lazima uanze chini.
Ni wachache Sana wanaofanikiwa kwa raha lakini wengi wameangaika.

Cha msingi malengo yako yawe mbele, na utatimiza unachotaka.
 
Graduates nendeni mkajiajiri kwenye kilimo, acheni ubwege.
Mtaji wako mkubwa ni nguvu zako na elimu yako. Mashamba yapo ya bure kabisa ktk mikoa ya Katavi, Tanga, na Tabora. Yaani sijui mnataka nn tena?
Hawataki kukaa bushi, hamna network huko
 
Mbinu kubwa niliyotumia kupata mtaji kwa upande wangu (na bado naendelea nayo) ni kufanya savings ya kila kidogo ninachopata, mfano mtaji wa kuingia nao mtaani niliupata kwa kufanya savings ya pesa ya chakula (bumu), ilikua kila bumu tunacha 250,000 tunampa mtu mmoja (waliopitia maisha ya bumu wanajua nilikua nabakiwa na kiasi gani hapa na jinsi gani sija enjoy maisha ya chuo.
nilifanikiwa kuingia mtaani na mtaji wangu mzuri tu, ( yaah kwa levo zangu ni mzuri) na kwa sasa maisha ya biashara yanaendelea japo kuna ups and down ila hizo hazinitoi kwenye FOCUS.

kuhusu kukwepa aibu kwakweli mpaka kesho sitojua nimeweza vipi, kwani katika maisha ya kawaida mimi ni mtu wa aibu kupitiliza, biashara ninayofanya muda wote inanifanya niwe na hali ya uchafu ila nimeweza kuimudu hii hali maana najua natafuta mtaji tu, si maisha yangu ya milele, nimejichanganya kijiweni na sijawahi kumsimulia mtu kwamba nina degree 😀 😀😀😀.
lahaulaah biashara ina ng'ara,

NB nimegraduate 2018 hapo mlimani hivyo sina experience saana na maisha ya mtaani.
 
Back
Top Bottom