Tatizo ni kwamba Most of graduates tunashindwa kuwa wabunifu,katika kipindi hiki ambacho hata wafanyabiashara hali sio nzuri sana, ni lazima nasisi graduates tutumie akili nyingi pia kwenye kutafuta kazI hasa kama hauna connection. Tunalalamika kwamba kazi zinatolewa kindugu au kirafiki lakini ukijiuliza tu mwenyewe Mfano wewe ndo boss na unatafuta mfanyakazi,anatokea graduate wa kwanza anatafuta kazi lakini humfahamu kabisa,upande wa pili anatokea rafiki yako unaemwamini anakwambia anamfahamu graduate ambae anachapa kazi,muaminifu na pia anawafahamu mpaka wazazi wake,kama wewe ndo boss utamchukua mfanyakazi yupi katika position hiyo ya kazi? DIRECTLY wengi watamchagua huyu wa pili maana hata kama ataleta uharibifu wowote inakuwa rahisi kumpata maana vijana wa sasa hivi nao hatueleweki,Kwa hiyo kwa sisi ambao hatuna connection ni lazima kuwa na vitu vya ziada na pia kuwa ubunifu ili kupata kazi.
NJIA RAHISI NINAYO IONA ILI KUPATA KAZI HASA KWA KIPINDI HIKI.
Unajua katika hiki kipindi kila boss anapokutana na graduate anaetafuta kazi wengi wanakuwa na wasiwasi kwamba huyu mtu nikimwajiri nitamlipa kiasi gani na degree,masters au P.h.d yake.mtihani mkubwa uko hapa na maboss wengi wanashindwa kutuajiri sababu kwanza anajua kwamba hatuna experience,pili hajui tabia yako na tatu hali ya biashara pia sio nzuri sana hivyo ana wasi wasi atakulipa kiasi gani uridhike na masters yako au P.h.d yako.Njia rahisi ya kuli ruka hili kweli kama wewe ni graduate unaetafuta kazi kweli na ni mchapa kazi ni kwa kwa kujitofautisha na graduates wengine wanaohangaika na mabahasha mjini kutafuta kazi,WAKATI wao wanatafuta kazi wewe tafuta kitu unachokipenda hasa vitu ambavyo vitakupatia UJUZI na itapendeza zaidi kama ujuzi huo utakuwa katika field ambayo umeisomea.MFANO kama umesomea mambo ya Computer science na unapenda labda mambo ya kudesign Website,graphics design au software development Tafuta Kampuni zako kama tano ambazo kweli zinadeal na hizo kazi za designing,badala ya kuomba kazi wewe OMBA kujitolea katika moja ya kampuni utakayo pata kati ya hizo tano,Kuwa mbunifu pia kwenye kuomba nafasi hizi za kujitolea,Mfano unaweza ukatafuta hata watu watatu wakajifanya ni wateja labda wanataka huduma ya kutengenezewa website ukaenda na mmoja siku ya kwanza kwenye kampuni ya kwanza ukajieleza wewe ndo umemtafuta na umemleta kama mteja,baada ya siku mbili ukampeleka mteja wako wa pili anajifanya anataka kudesigniwa logo, baada ya siku nne ukampeleka mteja wa tatu alafu siku hiyo hiyo ukaacha na barua yako ya kuomba kujitolea,Haki ukifanya hivyo kwa kampuni zote tano huwezi kukosa hata moja.
WORKING PRINCIPLE
Hapa ninavyosema uombe kujitolea haitakuwa kujitolea kweli kweli kama kweli wewe una nia na ni mchapa kazi kweli kweli,kama kweli unachapa kazi haita pita hata mwezi mmoja asilimia kubwa za makampuni wataanza kukulipa japokuwa haitakuwa sawa na degree,masters au p.h.d yako.Kuomba kwa kujitolea itaifanya kampuni kuwa free kukulipa kutokana na uwezo wake maana sio kla kampuni zinauwezo wa kumlipa mfanya kazi kutokana na elimu aliyo nayo.Hata kama wasipokupa kitu komaa maana UJUZI utakaoupata ndio muhimu kuliko hata mshahara ambao wangekulipa kwa elimu uliyo nayo.Njia pekee ya kutukomboa sisi kama graduates sio kupata KAZI bali kuwa na UJUZI,Baada ya muda ukiona umeiva vizuri na pesa wanayokulipa hauridhishwi nayo YOU CAN MOVE ON na kuanza kufanya hizo shuguli mwenyewe.KIUKWELI biashara unayoweza kuianza bila ya kuwa na mtaji kabisa ni kwa kuwa na ujuzi maana EVEN if utapewa mamilioni ya fedha uanzishe biashara labda ya kuuza products,huwezi kuwa na uhakika 100 percent maana biashara pia zinaweza kufa muda wowote,cha kujiuliza utafanya nini baaada ya biashara kufa?UJUZI ni security yako milele na hakuna yeyote anaeweza kuuchukua au kuku nyang'anya,LET US BE CREATIVE.