Omusolopogasi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2017
- 7,101
- 18,051
Tanzania kuna kasumba. Nilivyomaliza form 6 kwenye 1990s, nilitaka kufanya kazi ya kupiga debe Dar. Basi nikawaona watu wote waliokuwa kwenye business ya aina hiyo niliokuwa nawafahamu. Unajua nini? Wote walinikatisha tamaa na kusema siiwezi kwa vile eti ni msomi. Kila niliyemomba kazi ya aina hiyo, alisema siyo kzi yangu. Mwishoe sikupata japo nilikuwa tayari kuifanya.
Kwangu Mimi nakwepa aibu kwa namna hii.
Kwa mfano, mwanafunzi wa chuo ataona aibu kuwa day worker ya ukondakta. But najiuliza wale makonda wa daladala kwani hawana familia. Mbona unakuta Mtu sawa umri wa baba yangu na anafamilia na watoto anasomesha na Mbona haoni aibu. Sasa kwanini Mimi Kijana nione aibu Wakati Najua hii kazi Nitafanya kwa Muda mfupi na nitapata pesa na nitatimiza malengo yangu.
Mimi malengo yangu nayaweka mbele zaidi kuliko kituchochote.
Pia stori za watu maarufu Kama simbachawene Alikuwa mpiga debe kabla ya kuwa Waziri.
AY alikuwa analala kwenye kontena la washona nguo kabla hajawa super star
So Wanafunzi wa vyuoni na graduates wote wajue kwamba ili ufanikiwe lazima uanze chini.
Ni wachache Sana wanaofanikiwa kwa raha lakini wengi wameangaika.
Cha msingi malengo yako yawe mbele, na utatimiza unachotaka