Ungeangalia Position aliyokuwa Tanzania Prisons kabla na baada ya Game, Ungeelewa kwanini Simba jana kafungwa.
Nafasi aliyopo Simba hato drop chini wala kupanda kwenye matokeo yote ya kushinda au kushindwa.
Hii issue kwa Tanzania Prisons ilikuwa tofauti, angepigwa angekaa kwenye kundi la kushuka bila Play Off.
Baada ya ushindi wa jana kapanda nafasi ya 14, Kabla ya game la Jana ilikuwa inatakiwa ashinde game 2 zilizobaki kurejesha matumaini ya kubaki League kuu.
Game ngumu kati ya hizo 2 ilikuwa hiyo ya jana. Hawa wakongwe wanajuana.
Me sio mshabiki wa Simba, najaribu kuongea kimpira tu.