Mchochezi
JF-Expert Member
- Feb 29, 2012
- 10,962
- 7,830
Mimi naaamini kabisa, Atletico De Madrid atapambana na hatofungwa leo dhidi ya Juventus.
Ninajivunia safu imara ya ukuta ikiongozwa na Kamanda Kepteni Diego Godin. Licha ya umri wake mkubwa bado ana utulivu mkubwa sana awapo uwanjani. Pia golikipa Jan Oblak ni mhimili mwingine linapokuja suala la ulindaji wa goli. Leo nategemea kuona The best attacking team Vs The best defending team.
Mechi ya aina hii inanikumbusha UCL ya mwaka 2010, Inter Milan ya Mourinho Vs Barcelona ya Guardiola katika hatua ya Nusu Fainali, mechi ya kwanza pale Italia, wanashinda Inter wanashinda 3-1. Mechi ya marudiano pale Nou Camp, Barca alihitaji ashinde 2-0 ili asonge mbele.
Inter walipaki basi la aina yake, dk ya 15 Thiago Motta wa Inter akala umeme, wakabaki watu 10 uwanjani dhidi ya Barca ya Xavi, Iniesta, Messi, Ibrahimovic. Mechi iliisha kwa Barca kushinda 1-0 na Inter wakaingia fainali kwa aggregate 3-2.
Hivyo mechi ya leo naifananisha sana na mechi ile ya Inter Vs Barca. Leo naamini Atletico atashambuliwa sana lakini mwisho wa mchezo watafuzu robo fainali.
Tukutane baadae