Wale 'Team Mungu Mtu Chama' niambieni leo amecheza nini dhidi ya Coastal Union FC kwa Mkapa?

Leo chama alikuwepo je, tumepata ushindi wa kirahisi?
 
Mpira wa kasi na nguvu ndio pira halisi la afrika na yule mbrazili ndio kauleta pale simba[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Kumbukeni kuwa wapinzani wa Simba nao ni binadamu na wanafanya mazoezi ya kutosha.

Coastal Union jana walikuwa katika kiwango bora kabisa na walijituma na kufuata maelekezo ya Mwalimu.

Goli la Jana la Simba limepatikana kwa utulivu wa Chama.
Swala la kufanyiwa Sub ni la kawaida kwa mchezaji yoyote yule.

Ila Chama bado anahitajika Simba na sio jambo zuri kumsema vibaya, uchezaji wale wa taratibu umetoa matokeo mazuri sana kwa timu.

Katika mechi za mtoano mnakumbuka alivyofanya kazi kubwa kule Angola.
Goli la mapema lilifungwa na Chama.
Goli la Pili alilofunga Israel Mwenda pia Chama pia alihusika kulipika.

Goli la tatu la Phili ni assist ya Chama.
Mpeni heshima yake huyu Mwamba wetu.

Kama kasi basi msajirini Kisinda msimu ujao maana mkataba wake unaisha.

Mtoa Mada naona siku mbili hizi una hasira flani kutokana na mazingira yaliyo kupata. Usijali mambo yatakaa sawa.
 
Mchango wa Chama kwenye timu hauwezi kuwa mkubwa zaidi ya wengine wote, hayo ni mawazo mgando tu, hakuna timu ya kumtegemea mtu mmoja, ni ushamba mkubwa sana.
 
Uzi ufunguwe sasa maan umemaliza...
 
Tatizo ni mtu mmoja tu huyu jamaa popoma na anapata wafuasi wengi sana utopolo.
Ni kama alivyomsema sana Morrison na akapata support ya utopolo tena sana,lakini baadae utopolo hao hao wakamsajili Morrison.



Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Huu ushabiki wenu ni wa kindezi kweli. Yaani Simba kushinda kwa goli moja
imekuwa wachezaji wabovu? Je, Bayern Munich iliyoDUROO tena nyumbani ndio utaisemaje? Acheni upopoma. Gemu linabadilika kila leo.
 
Mleta uzi na wanaokunga mkono mnasahau kua Always FORM is TEMPORARY, STANDARD is PERMANENT. Yaan Chama kasha set Standard yake na hizo ups and downs kwa mechi na mechi ni kawaida kwa mchezaji, kila mchezaji ana style ya kucheza ambavyo hata kocha hawezi mmbadilisha maana ndo yupo hivyo yaan ameumbwa hivyo mfano chama hana kasi ndio ila anakitu ambacho kwenye hii Ligi hakuna na ameset STANDARD hapo yaan ana utulivu wa hali juu sana pamoja na accuracy passing yake ni kubwa mno. Hata kwa mechi ya jana japo hakuwa na form nzuri kama baadhi ya wachezaji wengine alitengeneza nafasi kwa Sadio Kanoute ambayo ilikua very clear akashindwa kufunga. Pia nawakumbusha tu kama nafasi alizotengeza Chama kwa msimu huu tu zingukuwa converted kuwa magoli yaan angekua na assist 20++ mpaka sasa kwenye ligi kuu tu.
CHAMA IS MASTER.
 
Huyu jamaa aliyeanzisha uzi huu anapenda sana kuchafua watu.
Kwenye siasa yupo
Kwenye michezo yupo
Kwenye mziki yupo
Kila kona yupo, ilo mradi awachafue wengine.
 
Awali Nilikuwa sielewi lengo lako kuhusu Chama lakini baada ya huu Uzi Sasa nimekuelewa. Ni kweli kuna watu wanaamini bila Chama kuwemo kwenye Mechi Simba haishindi. Na Mimi Jana nimeona mchango wake kama ni mkubwa Sana basi haizidi 7%.
Lakini pia najiuliza Mechi alizokuwepo kocha Mkuu mpya Chama hakucheza au alitolewa dakika 30 tu za mwanzo. Ghafla Kocha kaondoka Chama amepangwa. Kama mfumo unaotumika ni wa kocha Mkuu kama ilivyo kawaida ya timu kubwa hii imekaaje? Au tunadanganywa Kocha Mkuu kaondoka?
 
Uchambuzi makini kabisa
 
Simba ijiendeshe kisasa, iache kusajili wachezaji ambao umri umeenda.

Iache kungangania wachezaji kisa kuogopa wataenda Yanga
Waaache waendelee ili wajifute kwa mikono yao wenyewe kwenye ramani ya soka
 
Hasira za nini tena[emoji3][emoji3][emoji3]

Acheze ila asishobokewe kama yey ndie masia aliyekuja kutuokoa wana msimbazi toka utumwani..
Yaani hivyo mnavyoparuana sisi utopolo Huwa tunapata raha sana[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wachezaji hawakuwa na pressure kwasababu walijua kua wanacheza na tawi lao.
 
Chama Hana tatizo, tatizo bado kocha hajaingia kwenye mfumo wa chama🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…