PostGE2025 Wale tuliokuwepo tuliokuwepo kwenye tukio la Oktoba 29 tujitokeze kutoa ushahidi

PostGE2025 Wale tuliokuwepo tuliokuwepo kwenye tukio la Oktoba 29 tujitokeze kutoa ushahidi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
"Nilikuwa naomba kwa wale wote ambao wanaamini kwamba walikuwepo kwenye tukio la Oktoba 29 wale wenye ushahidi tutokee kwa wingi tutoe ushahidi kwa hii tume ambayo ipo kwa ajili ya kufanya upelelezi. Kama mnavyojua Oktoba 29 wale ambao tulikuwepo tulishuhudia mauaji yalitokea..."

"Hii ni kwa ajili ya kutaka kujenga nchi yetu kwa matukio yaliyotokea tarehe 29 Oktoba 2025 yasije yakatokea tena kwa wakati mwingine... ushahidi utakaoutoa uwe wa kweli ushahidi utakaoutoa uwe wa kujenga nchi yetu Tanzania yetu ni moja amani yetu ni moja."
 
Sijaelewa hii maana yake nini kwani wale waliokua wanaua watu kwa kuwapiga risasi za kichwa wamefikishwa wapi? Tunapotezeana muda kwa mambo ya kijinga, hii maana yake nini?
 
Safi sana
Nyinyi wa mitandaoni bakini humuhumu mlikishana matopetope
Maana mlikuwa chini ya uvungu hio siku
Mjifunze ushuhuda kwa wale wa kweli, ambao bila kutoka hata chapati na chai haioni hio siku
 
Safi sana
Nyinyi wa mitandaoni bakini humuhumu mlikishana matopetope
Maana mlikuwa chini ya uvungu hio siku
Mjifunze ushuhuda kwa wale wa kweli, ambao bila kutoka hata chapati na chai haioni hio siku
Wewe ulitoka wapi?
 
Sijaelewa hii maana yake nini kwani wale waliokua wanaua watu kwa kuwapiga risasi za kichwa wamefikishwa wapi? Tunapotezeana muda kwa mambo ya kijinga, hii maana yake nini?
Ule ushahidi wa tume ya kwanza wameupeleka wapi?
Watu walijitokeza kutoa ushahidi hadi tume ikakataza watu kurekodi au kuripoti yanayosemwa na baadhi ya mashahidi kutishwa.
Sasa tume ya pili ni kupoteza Muda tuu.
 
... Lord do let me walk alone ..... Your promise is True ...When my heart is tired and wearied ... I just need to know you are near
 
Wale waliouliwa kwa risasi ndio waliokuwepo kwenye matukio! Na ndiyo wangetoa ushahidi.
Waliobaki Polisi ilitoa Cufew ya kutotoka nje kuanzia saa12 jioni wasingeweza kushuhudia kinachoendelea zaidi ya kusikia milio ya risasi!
Zaidi ya hapo Wauaji ndiyo wanajua!
 
Back
Top Bottom