Wale tuliolelewa na mama wa kambo tuje hapa tuongee

Wale tuliolelewa na mama wa kambo tuje hapa tuongee

Beira Boy

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2016
Posts
19,976
Reaction score
32,195
Aman iwe nanyi wapendwa katika bwana

Husika na kichwa cha habari hapo juu

Kuna wale ambao kutokana na sababu mbali mbali hatukupata kulelewa na mama zetu wazaz bali tulilelewa na mama zetu wa kufikia yaan wa kambo

Mimi nimelelewa na mama wa kambo aisee yaan kila day ilikuwa na kichapo had tumekuja kukua ndo tukaanza kuvimba vimba lakin tumekula kichapo sana

Ninachoshuru yule mama kumbe alikuwa anatupa akili pasipo yeye kujua maana yeye alikuwa anajua anatutesa

LONDON BABY
 
Kawaida yao huwa wanapenda watoto wao zaidi wewe mwingine utapata shida lazima...wachache sana wanaopenda wote
 
Nakumbuka kuna siku alinichapa kwa style ya kichwa chini miguu juu nikiwa nimening'inia kwny dari nimefungwa kamba kosa lenyewe sasa la kipuuzi wakati huo nilikuwa na miaka 8
 
Mi nimekula msoto Sana Sana asbh nilikua nabeba ndoo za Maji mpk nijaze pipa ndio niende shule na Maji yalikua mbali kdg so saa 10 ucku naamka,sometimes nachongewa kwa mdingi nachezea kichapo havi na mengine Mengi ila namshukuru yule mama alinipa ujasiri wa kupambana na haya maisha![emoji120]
 
Rafiki yangu aliniambia mama wa kambo aliweka mkazo lazima awe anapeana zamu za kupika na house boy. Amefika university alikuwa mpishi mzuri si pilau, chapati, mchuzi wewe taja tu. mengine yanakuwa ni life gift
 
Mhh,nilipata msoto balaa. Nilikuwa nalisha kuku,ng'ombe,kukamua,kufanya usafi banda,nk. Yote kumi, nikawa napewa msosi kidogo mno,nakula mwenyewe nje,wakati wadogo zangu wanaangalia TV. Ilikuwa inanunuliwa glucose ya kuku,inawekwa kwenye maji yao,kuna siku nikaamua kuilamba,maana nilikuwa na njaa. Ila mzee wangu alikuwa poa sana, ila alikuwa mtu wa safari,sikuwahi kumweleza,nisje nikaharibu maisha yao. Sijawahi kusema hili,hapa mambo wazi
 
Rafiki yangu aliniambia mama wa jambo aliweka mkaka to lazima awe anapeana zama za kupika na house boy. Amefika university alikuwa mwisho mzuri si pilau, chapati, mchuzi wewe taja tu. mengine yanakuwa ni life gift
Mpe pole sana mkuu
 
Mm alinilea vizuri bahati nzuri alikuwa mtu wa dini sana ndiyo maana
 
Mi nimekula msoto Sana Sana asbh nilikua nabeba ndoo za Maji mpk nijaze pipa ndio niende shule na Maji yalikua mbali kdg so saa 10 ucku naamka,sometimes nachongewa kwa mdingi nachezea kichapo havi na mengine Mengi ila namshukuru yule mama alinipa ujasiri wa kupambana na haya maisha![emoji120]
Yako na yangu ni sawa kabisa,Utajaza pipa na usipojaza Baba alishalishwa za kulishwa utapigwa kama mbwa aliekosa kwao.
 
Napenda mnavyofunguka bila kutegemea mwisho wa siku muwe verified tuwajue maana mnataman kujulikana ila sijui uoga au nn. Leo mnataja mama wa kambo ,kesho shule mnazosomea etc watu tunaunga picha tu
 
Mi nilikaa kwa mjomba,,mke wake alinitesa sana,,,, wana pesa sana ila mchana hatuli ,,na nilikua na yy tu hawakua na mtoto ,mchana hakuna kula ila yy anakunywa juice na matunda na bites mi ananiambia kwangu hatulagi mchana,,,,uzuri nilienda tu kusalimia nilijuta kwenda,,, nilikaa miezi miwili ila niliona miaka
 
Back
Top Bottom